(Naomba mods wa stick uzi huu kwa ustawi wa taifa letu)
Naamini timu nzima ya #WachapaKazi wa Magufuli wapo tayari kuchukua kero zetu #Watanzania na kuzifanyia kazi bila kusita.
Hivyo basi, tuweke kero za msingi hapa.
Mimi naanza na hizi;
1. Mpasuko unaosababishwa na tofauti za kiitikadi.
- Tuweke Utanzania mbele kuliko itikadi.
2. Ufisadi wa kutisha
- viporo vyote vya ufisadi vifanyiwe kazi na mfumo uimarishwe.
3. Bei Kubwa ya Umeme
- Mikataba ya umeme ipitiwe.
4. Miundombinu
- Sehemu kubwa ya Tanzania bado haina miundombinu ya barabara, maji, umeme nk.
5. Mazingira
- Mazingira yetu yanaathiriwa sana na kelele za muziki wa ma bar na vilabu, uchafu, ujenzi holela nk.
6. Mfumo wa Uchumi
- Uchumi wetu umeshikiliwa na unanufaisha tabaka fulani la wachache na wageni kutokana na serikali kutosimamia vyema fursa zinazojitokeza.
7. Madawa ya kulevya
- Madawa ya kulevya yanaua nguvu kazi ya taifa letu.
8. (Endelea ........ )