Kero kubwa kwenye tendo la ndoa

MusuKuma

Member
Jan 30, 2021
21
75
#SOMO:KERO KUBWA KWENYE TENDO LA NDOA, ZINAZOHARIBU NDOA NYINGI.

Hairuhusiwi kusomwa na walio na umri chini ya miaka 18

AHM Sikiliza Ubongo wa kila mwanadamu unaujua umuhimu wa tendo la ndoa.
Unajua kuwa tendo la ndoa ndio raha kamili ya ndoa, dawa ya kutibu afya ya akili na hisia za wanandoa, na pia ni kiungo muhimu cha kunogesha utamu wa ndoa yao.

Lakini kufanya tendo la ndoa inaweza kuwa raha au karaha kwa mwenzako, kuendana na wewe mwenza wake unachukua hatua zipi ili kumpa raha kamili.

Nimeshuhudia ndoa nyingi zikiingia kwenye migogoro, usaliti, na hata kupelekea wanandoa kudharauliana, yote sababu ya ubovu na karaha wanazokutana nazo wakati wa tendo la ndoa.

Leo nataka niiokoe ndoa yako, kwa kuhakikisha nakukumbusha mambo muhimu yatakayojenga ndoa yako kupitia tendo la ndoa, kwa kuepuka kero zifuatazo.

Mambo yanayokera wakati wa tendo la ndoa.

1: UCHAFU:

Wanaume wengi wamejivika ujinga kuwa suala la kujiweka safi, ni suala la mwanamke.
Lakini wanasahau kuwa wanawake wanavutiwa na wanaume smart, na kiuhalisia wanawake wamejawa na kinyaa, hivyo hufanya wakerekwe zaidi pindi wanapokutana kimwili na wanaume wachafu.

Hakuna mwanamke anayeweza vumilia harufu mbaya, na uchafu, hii huwafanya wapoteze hamu ya tendo la ndoa.

Kwa upande wa wanaume pia, wanachukizwa na wanawake wachafu.
Na hii huwafanya wapoteze kabisa hamu ya kuendelea kufanya tendo la ndoa na huyo mwanamke, na huweza pelekea akaanza usaliti.

NTBR: Hakikisha mwili wako uko safi, kinywa, sehemu za siri, makwapani, nakadhalika.

2: KUTOANDALIWA KIMWILI:

Raha ya tendo la ndoa huzidi kuendana na Ubunifu wa yule unayefanya nae tendo la ndoa.
Baadhi ya wanaume huwa hawatilii maanani suala la kumuandaa mwanamke kabla ya kumuingilia kimwili, wanaona kama wanachelewesha muda.

Wanasahau kuwa kiuhalisia hisia za mwanamke zipo mbali na hujijenga taratibu, hivyo kumuingilia kimwili bila kumuandaa humsababishia maumivu na michubuko kwenye sehemu zake za siri, na hii hugeuka kero na mateso kwake na kumfanya asiwe na hamu ya kukutana na wewe kimwili.
Na pia huweza pelekea akachukia tendo la ndoa au kutokuwa na hamu kabisa.

Unafanya nae tendo la Ndoa, analia, unadhani umemkoleza, kumbe mwenzako analia kwa sababu ya maumivu unayompatia.

Sio wanawake tu ambao wanahitajika kuandaliwa, bali hata wanaume pia.
Kisayansi, mwanaume hatuwezi kushiriki kikamilifu tendo la ndoa endapo ana huzuni, ana msongo wa mawazo(stress), au ana uchovu.
Hivyo Maandazi anayotakiwa kutafanya mwanamke, ni kuhakikisha anamuondoa stress mumewe, uchovu, na huzuni.
Pamoja na kumpandisha hisia kwa kumfanyia mambo ya kimahaba yatakayohamisha mawazo yake kwako.

3: KUTOFIKISHWA KILELENI:

Kufika kileleni ni kiashiria tosha kuwa umemtibu kisawa sawa mke wako, umemnogesha, na kumfanya afurahie raha uliyokuwa unampa.

Baadhi ya wanaume wamekuwa wabinafsi wakati wa tendo la ndoa, huwa wanatimiza haja zao wao tu na wala huwa hawaangalii kama mwenzake amefika kileleni au laah.

Na hii imekuwa kero kubwa kwao, na imekuwa chanzo kikubwa cha usaliti na hata kupelekea wanawake wengi kuwadharau wanaume wao.

4: KUKOSA UBUNIFU:

Tendo la ndoa linahitaji ubunifu, hakuna mwanaume wala mwanamke anayevutiwa na mtu aliyekosa ubunifu.

Wanaume wanachukia wanaume wasioshughulika kitandani.
Wanawake wanachukia wanawake wasiojua wanachokifanya, wasiojua kuwakoleza na kuwanogesha kisawa sawa.

6: KUBEMBELEZANA:

Kero kubwa kwa wanaume ni kubembelezana kupewa haki yake, na huwa inamuudhi sana pale anaponyimwa kwavisababu visivyo na msingi.
Unakuta mwanamke anamnyima mumewe tendo la ndoa kwa siku 3 mfululizo, eti kisa tu hajanunuliwa dera alilotaka.
Sawa unamnyima, ila unajua kuwa wanaume ni kazi sana kuvumilia hamu ya mwili wake?.
Usijisikie vibaya ukija kusikia anachepuka, jua kuwa ulimsababishia mwenyewe.

5: KUINGIZA MADA ZISIZOHUSU:

Kuna wanawake wamegeuza wakati wa tendo la ndoa ndio wakati wa kukumbushiana mada zinazokera, wakati wa kulaumiana.

Hii humfanya mwanaume apoteze hamu ya tendo lenyewe, au hata kumfanya Ashindwe kulifurahia tendo la ndoa.

Wakati wa tendo la ndoa ni wakati wa kujengana kihisia kwa maneno matamu, na vitendo vinavyojenga misisimko ya kimwili.
Jaribu kuepuka mada zisizohusiana na wakati huo.


Kuna uwezekano mumeo anaishia njiani wakati wa tendo la ndoa, ukaanza kumdharau, au kumsaliti, kumbe tatizo huwa ni wewe.
Unafanya nae tendo la ndoa wakati ana uchovu, stress, huzuni, au uchafu wako, au bughuza zako, kukosa kwako ubunifu, kumbe ndo sababu ya yeye kuwa hivyo.

Kuna uweze kano mumeo anakusaliti au anakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na wewe, kumbe tatizo ni uchafu wako, au kukosa kwako ubunifu, au bughuza unazompa.

Kuna uwezekano mkeo anakusaliti, kumbe tatizo ni wewe, humuandai kabla ya tendo la ndoa, au humfikishi kileleni.

Kuna uweze kano mkeo anakosa hamu ya tendo la ndoa, kumbe tatizo ni wewe, unamuumiza sana wakati wa tendo la ndoa sababu humuandai vizuri.

Naomba jitafakari, na uchukue hatua za kuijenga ndoa yako.

#SWALI

Kwanini watu wengi hasa wanawake wanajiisi kupendwa sana wakati tu wakiombwa tendo na wanaume ? Au upendo ni tendo ama!!

#FUNGUKA TOA HOJA YAKO

MKRISTO MWENZANGU UBADILIKE NENO NDOA LINAHITAJI AKILI SANA ILI KUDUMU.

#Ahm2021new
#Bettermarriage2021
 

grand millenial

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
1,885
2,000
Nanukuu
"
Wanaume wanachukia wanaume wasioshughulika kitandani.
Wanawake wanachukia wanawake wasiojua wanachokifanya, wasiojua kuwakoleza na kuwanogesha kisawa sawa."
Mwisho wa kunukuu.

Labda mimi ndo niwe sijaelewa ila kama ndo ulichomaanisha, basi mkuu wewe utakuwa punga.

No offence.
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,552
2,000
Umesema mengi sana ya maana lakini ukasahau kuwa; Nikiwa na pesa mfukoni hata koni itanyonywa tena kwa kuombwa anyonye. Samahani kwa lugha hiyo ila huo ndo mpango mzima
 

Noelia

JF-Expert Member
May 26, 2017
14,237
2,000
Namba 3 Ni ya kutilia mkazo sana maana hapo ndipo pamebeba maana nzima ya utii kutoka kwa mke kwenda kwa mumewe, inaanza taratibu tu ikikomaa zaidi hapo ndipo utajua kuwa hakuna kiumbe chenye dharau km mwanamke
 

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
5,078
2,000
No 2. Wanawakewalio ndoani wanavumilia sanaYaani wanaume nje wanajikunjua balaa akifika kwa mkewe kisa amemtolea mahali na hawezi kwenda kwingine likimpanda mda wowote atafukunyua idara na kutafta madini akiyapata analala km simba zee huku hajui mwenzie yupoje.
 

Quetzal

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
5,838
2,000
Kweli nimepata Corona hata sisimki nikisikia hizi mada. ...za kunyanduana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom