Kero hii NHIF hadi lini?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Pale unapokwenda kutafuta tiba na katikàti ya huduma unaelezwa na madaktari husika kuwa: "Kipimo au tiba hii haiingii kwenye NHIF, inabidi ulipie cash."

NHIF mlipoanza huduma hii hili mlilipanga vipi?

Je, ni haki mteja wenu mnamkata pesa kila mwezi na mara nyingi haugui ama kutumia kadi hata miezi sita, vipi mteja wenu huyu anapofikwa na shida kubwa katika ugonjwa anakutana na kikwazo hiki?

Nini hasa tatizo?
Je, ni lini shida hii itaondolewa ili tupate kunufaika na huduma zenu kwa 100% pia kuizidishia thamani kadi yenu ya matibabu?
 
mim ni kifurush cha sitandard.je kinacover nin na nn?
NHIF ni hiari kwa sasa na ina vifurushi ambavyo unalipia mchango wako kulingana na umri, uhitaji na pia ukubwa wa Familia.
 
Mnapojiunga Bima someni zile forms ili kujua ni huduma gani unastahili kupata na ipi haipatikani. Wengi tunasaini tu na kukwepa Yale maelezo mengi. Ukija hosp ukaambiwa hii huduma haipatikani kwa NHIF unaishia kulalamika!
 
huduma za serikali ya wadanganyika nyingi ni za kijambazi....mtanisamehe...nimekosa neno zuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…