Sisi watumiaji ambao ndio wateja wa daraja la Nyerere Kigamboni tunakerwa na hii tabia ya watendaji hapa darajani.
Nyakati ambazo ni busy asubuhi na jioni, mageti matatu au manne kati ya saba yaliyopo ndio hufanya kazi, jambo linalosababisha foleni na hivyo kudhoofisha lengo la serikali la kuondoa kero za usafiri kwa kuboresha miundombinu.
Nimefanya uchunguzi wa muda mrefu na kugundua kuwa hii imekuwa ni tabia wala sio ubovu wa haya mageti kama ambavyo nilidhani hapo mwanzo.
Watanzania tujifunze kufanya kazi kwa bidii, tuache uvivu na tumuunge mkono kiongozi wetu kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Tunawataka wahusika kuchukua hatua ili kuondoa usumbufu kwa kuhakikisha mageti yote yanafanya kazi muda wote.