Nkuba25
JF-Expert Member
- Nov 18, 2015
- 2,341
- 13,021
Habari wa Bodi
Leo nimekutana na kadhia mbaya sana hapa CRDB tawi la Tegeta. Nimefika hapa saa nne kamili (muda wa kugungua tawi siku ya jumapili), na nikafanikiwa kuingia ndani muda huo.
Baada ya kujaza karatasi ya kutolea pesa, nikaelekea counter. Bank Teller akaanza na habari kuwa "subiri komputa ndio inawaka", baada ya kama dakika 10 hivi ananieleza mtandao hakuna, subiri kama baada ya nusu saa.
Nusu saa ikafika, nikaenda tena kwa huyo Teller, akanieleza "subiri kidogo". Zimepigwa danadana za namna hiyo kwa kipindi cha masaaa mawili. Wimbo ukiwa "subiri kidogo". Baadae wananieleza "inabidi uende mlimani city kama una haraka sana"
Hili Tawi la CRDB Tegeta limekuwa na kero zisizokwisha. Kila wakati hapa kuna shida ya network. Viongozi wa CRDB jaribuni kuwa serious na biashara yanu na mpunguze mambo ya kitoto, kwa maana haiwezekani kila siku hapa kukawa na shida isiyoweza kutatuliwa. Kama vipi, fungeni ili tawi kwa muda na mfanye marekebisho ya network kuliko hivi mnavyotusumbua sisi wateja.