Kenya ya 3 kwa Umeme wa uhakika wakati Tanzania umeme ni anasa

Kenya kieneo ni karibia nusu tu ya Tanzania tena sehemu kubwa ya ardhi yake ikiwa na kame isiyozalisha chochote na pia ikiwa na rasilimali chache sana kulinganisha Tanzania ila ina uchumi mkubwa sana kuishinda Tanzania kwa zaidi ya theluthi. Hii ilipaswa kuwa aibu kubwa.
 
Wewe mtu binafsi lazisha kauzie hio serikali ,wewe mtu binafsi kawekeze in partneship na hio serikali , wewe mtu binafsi tajirika wewe na uirudishie kodi serikali yako isaidie wale watu masikini ,wewe mtu binafsi jiendeleze wewe basi na serikali yako itakuwa na watu walioendelea ila wewe mtu na watu binafsi kumbatieni umasikini sana mnazalisha taifa masikini ndivyo ilivyo nq itaendelea kuwa watu masikini huzalisha taifa masikini watu werevu na wenye uwezo huzalisha taifa la werevu na lenye uwezo it began with indivinduals .
 
Yani ili taifa kuna wakati ni bola lingepinduliwa tu awa walevi wa madalaka waisome namba na wao
 
Ukisema uongo ulio wazi, hata kama utauwasilisha kwa tarakimu za maandishi ya dhahabu, utabaki tu kuwa ni uongo siku zote. Hauwezi kugeuka na kuwa ukweli kwa vile tu takwimu pinzani hazikuwasilishwa.
Swali ni kuwa wewe umeupimaje huo uongo wa mwenzako kwa hoja ya ukweli ili na wewe upimwe na wengine iwapo sio mwongo vilevile (labda)?

Mwenzio kahesabu au katengeneza namba na kuziweka hapa (kwa mujibu wako) na kusema hizi ndizo takwimu. Wewe unasema, hapana haya ni manamba ya kujiandikia tu..

Okay, it's well and good.

Sasa wewe takwimu zako, na namba zako "za kitaalamu" au zozote zile kwa kadiri ya utafutaji wako ziko wapi ili wasomaji wafanye comparison kujua yupi ni mtafiti na mtakwimu makini?

That's all. Nothing more, nothing less..
 
Ni kweli ila inakuaje nchi yenye uchumi mkubwa na viwanda vingi tunawazidi kwenye suala la utoaji wa ajira?
 
Ni kweli ila inakuaje nchi yenye uchumi mkubwa na viwanda vingi tunawazidi kwenye suala la utoaji wa ajira?
Ajira tunazowazidi nazo ni za mashambani uvuvi, ufugaji, migodini na uchomaji mkaa. Watanzania wengi ni vibarua mashambani. Kukiwa na maendeleo makubwa ya Kilimo Tanzania na mashamba yaanze kulimwa kisasa kwa mashine raia wengi sana wa mashambani watapoteza ajira na kubaki wanazurura tu.
 
Unahitajika mirembe aisee
 
"Ndiyo maana Kikwete alipoulizwa kwa nini nchi hii ni maskini, alisema hata yeye hajui", alishangaa kuona yeye alikuwa masikini lakini leo ametajirika bila ya kufanya biashara yoyote ile.
 
Kwa mazingira kama hayo, badala ya kuhangaika vitu vya msingi kama huduma ya umeme, tunahangaika na vitu vyenye impact ndogo sana kama ROYAL TOUR, tukiamini itaongeza watalii, wakati mazingira yetu yanafukuza watalii.
Na Cha ajabu sijui niseme kustaajibisha kila Mzungu anaefika akiulizwa unaelekea wapi jibu ni moja tu 'Zanzibar', kwa hio wazungu wengi wanakimbilia kwenye umeme usiosumbua yaan 'Zanzibar'
 
Kwanza ni muhimu ujue, ni nani kati yetu ana 'burden of proof." Mimi sina jukumu la kuleta utafiti ulinganishwe na hayo manamba aliyotengeneza huyo mtu. Mimi nawasilisha tu uhalisia uliopo usioendana na hayo manamba yaliyopachikwa humo.
Nikiona nyumba ambazo hazina umeme, lakini zinahesabika tu kuwa nazo ni kati ya hayo manamba yanayohesabika kwenye huo utafiti, nitayakataa hayo manamba, na wala sina wajibu wa kufanya utafiti kwanza halafu niuwasilishe kupinga hayo manamba yasiyokuwa na ukweli.

Kwa hiyo, elewa kuwa siyo jukumu langu kuleta utafiti, jukumu langu ni kukataa uongo unaowasilishwa kutokana ninayoyaona kiuhalisia yakiwepo.
Naona mjadala huu sasa tunazungukia tu kweye hayo hayo ambayo tumekwishaelezana tokea mwanzo.
 
Hizi takwimu sio za kuamini toka mwaka jana South Africa wana mgao Tanzania ikasome. Labda ni takwimu za kua na miundombinu bora ya umeme ila sio kua na umeme wa uhakika.
Kenya wanatushinda kwa sababu zipi?
 
Mkuu 'Yoda', kwanza nikueleze kuwa maswali yako hayana uhusiano wowote na mada inayojadiliwa hapa, ambayo inahusu "Kenya ya 3 Kkwa "UMEME WA HAKIKA...."; kwa hiyo pamoja na kwamba ningeweza kujibu maswali hayo, ambayo mengine ni 'redundant' sioni umuhimu wa kufanya hivyo.

Pili ni lazima nikukumbushe kwamba hakuna popote nilipoandika katika mada hii kuonyesha kwamba hali ya umeme Tanzania ina unafuu wowote, kwa hiyo siyo swala la ulinganisho wa nchi hizi mbili, ambazo zote kiuhakika ni mbovu tu, hakuna yenye unafuu.

Tatu, ni muhimu pia uelewe, hayo uliyoyaita ni "bRah bRah", bila shaka utakuwa huelewi maana ya msemo huo. Yasome tena, unionyeshe ni yapi hasa ni 'bRah' kwa maoni yako.
 
Haya hapa ndiyo maana ya kuwa na "umeme wa uhakika" kama mada inavyosema?
Hiyo Megawatt 3,000 unayoimba kama kasuku juu yake uliiona ikizalishwa wapi nchini humo. Kama huku siyo kujitoa akili. EPRA wenyewe, wahusika na maswala yao ya umeme wanasema nchi hiyo haizalishi zaidi ya MW 2,300; lakini unakuja hapa na kuvimbisha mishipa kwa jambo ambalo hulijui kabisa?

Hivi unaelewa maana ya ujuha kama huu uliouweka hapa: "...takwimu ambazo ni public na yeyote anayetaka anaweza kuziona" Sasa kama unalitambua hilo, kinachokuliza hapa ni kitu gani?
Umeangalia hizo takwimu ukaziona zinaendana na uongo uliowekwa katika hicho kinachoitwa utafiti unaodai nchi hiyo kuwa ya tatu Afrka katika (hata haieleweki jambo gani hasa)!
 
Juzi niliona kwenye vlogs za I am marwa Yule mkenya wamekaa miezi sita bila umeme kijiji kwao....kenya power ni jipu tu kama ilivyo tanesco
 
Juzi niliona kwenye vlogs za I am marwa Yule mkenya wamekaa miezi sita bila umeme kijiji kwao....kenya power ni jipu tu kama ilivyo tanesco
Actually ni zaidi ya Tanesco kwa njia nyingi mtu akitaka kuchambua hizi taasisi mbili; na Tanesco chini ya Maharage na Makamba jukumu lao lilikuwa ni kuipeleka Tanesco katika muundo ule ule wa Kenya Power, ila mpango huo naona umebuma.
 
LOooooh!
Huyu ni wewe, au kuna mwingine kachukua ID yako?

Haya sasa, tueleze, wakati ukiyataja haya takwimu ziko wapi. Utafiti uliufanyia wapi hadi ukafikia mahitimisho haya?

Wakati mwingine uwe na akili ya kutambua kwamba kukataa uongo ulio wazi hakuhitaji kuweka manamba. Huyo aliyeweka hayo matarakimu ndiye mwenye jukumu la kueleza hayo manamba yake usahihi wake ni upi yanapohojiwa.
Hapa zile ulizoziita wewe "bRah bRah" umeona hazihusiki au siyo?

Hivi nikuulize, una uraia pacha wa huko mahala, maana naona umeguswa sana na habari hii.
 

Hujaenda kwenye mambo ya msingi.

Jiulize, kwa nini maendeleo makubwa na mabadiliko makubwa, Dunia nzima, yalihusishwa na utawala fulani.

Elewa tu:

Failure of any organisation is failureof the management. Hakuna, hakuna hata nchi moja iliyowahi kuendelea au itakayoendelea, ambayo ina Serikali ya hovyo au uongozi wa hovyo.

Uuongozi/serikali ukiwa mzuri, inakuwa ni uongozi/serikali wezeshi wa maendeleo.

Uongozi/serikali ikiwa ya hovyo inakuwa ni kizuizi cha maendeleo ya watu na wananchi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…