Kenya: Wezi wavunja dirisha la kanisa na kuiba sadaka

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
27,778
30,749
GENGE la wezi lilivunja kanisa la kikatoliki la Mtakatifu Yusuf mjini Chuka usiku wa Jumapili na kuiba sadaka kiasi kisichojulikana.

Jacinta Gakii, mmoja wa watawa katika kanisa hilo aliambia SwahiliHub kwamba wezi hao walitekeleza uovu huo mwendo wa saa sita usiku walipovunja nyumba yao kwa kutumia jiwe la ujenzi.

Mtawa huyo alisema alisikia mlio mkubwa walipokuwa wakivunja mlango na ndipo alianza kupiga nduru akiita wengine lakini alipotoka mwenzake alitekwa nyara na kulazimishwa kuwaelekeza kwenye nyumba ya kasisi.

“Mwenzangu aliposikia nikipiga duru alitoka nnje kunisaidia lakini wezi hao wakamteka nyara wakamlazimisha awaelekeze anakolala kasisi ambapo walivunja dirisha wakaingia ndani na kuiba sadaka,” alisema mtawa Gakii.

Aliongeza kuwa watuhumiwa walionekana kulifahamu jengo hilo kwa sababu waliingia na lango la nyuma wanakolala watawa.

"Mahali hapa huwa kumelindwa sana lakini walivunja mlango wa nyuma ambapo ni vigumu sana kwa mgeni kujua," alisema.

Akiongea na SwahiliHub kwa njia ya simu, kasisi wa kanisa hilo Cyprian Mbaka alisema kuwa sadaka hiyo ilikuwa takribani Sh16000. “Sadaka ilikuwa kati ya Sh15,000 na Sh16000,” alisema kasisi Mbaka.
Afisa mkuu wa polisi Kaunti ya Tharaka-Nithi Beatrice Karaguri alisema hakuna mtu alijeruhiwa wakati wa tukio hilo. Aidha, alibainisha kuwa tukio hilo linaonekana kupangwa na mtu anayefahamu mahali hapo vizuri kwa sababu nyumba ya kasisi ilikuwa imewekwa alama.
Walijua sadaka inapowekwa

"Kunaonekana wezi hawa walijua vizuri mahali ambapo sadaka huwekwa kwa sababu walipopelekwa kwenye chumba anamolala kasisi walienda moja kwa moja hadi kwenye dirisha iliyokuwa na alama, wakaivunja na kuchukua pesa," alisema Bi Kiraguri.

Alisema polisi wameanzisha uchunguzi juu la tukio hilo. Wakazi wamelaani wizi huo na kutoa wito kwa polisi kutia bidii ili kumaliza uhalifu unaoendelea kuongezeka mji humo.

"Kama wezi wanavunja na kuiba kanisani, basi biashara zetu ziko hatarini," alisema Bw James Muteg

Wezi wavunja dirisha la kanisa na kuiba sadaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom