Kenya wanashindwa kulipa kodi ya jiji, Hiki ndicho kilichowakuta

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,659
2,826
Serikali ya Baraza la Jiji la Nairobi imetwaa majengo ya shirika la utangazaji la Kenya (KBC) kutokana na kutolipiwa kodi.

Baraza hilo limeweka bango kubwa katika lango la majengo hayo kutangaza kwamba kwa sasa majengo hayo yamo chini ya usimamizi wa baraza hilo.

"Wapangaji wote wanafaa kulipa kodi kwa Baraza la Jiji hadi malimbikizi ya kodi yalipwe,” tangazo la baraza hilo linasema.

Baraza la jiji linasema linadai kodi ya jumla ya $20 milioni (Shilingi bilioni mbili za Kenya).

Hii si mara ya kwanza kwa baraza hilo kutwaa usimamizi wa majengo jijini Nairobi kutokana na kutolipiwa kodi lakini huwa nadra sana kwa mashirika ya serikali kuandamwa.

Shirika hilo la utangazaji limekuwa likikabiliwa na matatizo ya kifedha miaka ya karibuni.


Chanzo: swahili-news.com
 
Kwani hawapati Ruzuku serikalini kama wenzao TBC? Ila tuseme ukweli KBC ni wazuri na wako fair sana kulinganisha na TBC.
 
Magufuli nenda na huko uwatumbue hilo jipu...................
Aah wapi,magafuli hatawezana na wakenya.Kenya hakuna nyumbu,kila mtu ana sauti.Hiyo TBC yenu mtaweza kuilinganisha na KBC kweli?Sidhani,TBC hata wakisoma habari inakaa ni kama ZeComedy!
 
kama ya serikali inazinguliwa wakati hapa startv isiyo ya serikali iliendelea kupeta
 
Back
Top Bottom