Kabaridi
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 2,023
- 534
- Thread starter
- #41
Kama mna uhakika kuwa tukifunga mipaka hamtaumia kwanini mnalialia tunapowapandishia ushuru? Halafu nani kasema karasha ni mtanzania? au wee ndo unaongea kwa hisia! Lakini hata kama ni mtanzania bado watanzania ni fraction ndogo mno kulinganisha na wakenya wanaohangaika kuingia Tz, hivyo kwetu sie hiyo movement ya watu kati ya TZ na kenya haitulipi kama na nyie mlivyoona haiwalipi miaka ile ya 1977. Kwasasa flow ya waTZ kwenda nchi za SADC ni kubwa mno kulinganisha na nchi za EAC hasa kenya na hata hao wachache wanaoenda kenya wengi wao ni waganga wa kienyeji na wale wanafunzi waliofeli na kushindwa kuendelea kimasomo TZ hivyo wanatafuta pa kutokea ndo maana wengi huwakuti ktk public universities kama Nairobi, kenyatta, moi n.k bali unawakuta kwenye vyuo kama USIU ambako pesa ni kama tai. Kwa upande wa wafanya biashara ni wachache mno, jaribu kutafiti ktk malawi miji ya chitipa, karonga, mzuzu, lilongwe na blantyre halafu nenda ktk miji ya zambia; kuanzia nakonde mpaka Lusaka utaona jinsi kulivyo na watanzania wengi. ukifanya utafita utagundua ni kwanini TZ haiwezi kuiacha SADC na jinsi ilivyo rahisi kwa TZ kuidamp EAC. Halafu hoja yako ya kiswahili ni dhaifu sana, kwa maelezo yako unamaanisha Uganda tuko mbali nao kwasababu wanatumia zaidi kiingereza na hawajui kiswahili. Ukweli ni kuwa kenya iko mbali zaidi na TZ kiitikadi kuliko ilivyo kwa uganda na TZ japo kenya mnajitahidi kuongea kiswahili cha kuungaunga, na kuonesha kuwa lugha sio ishu ndo maana Zambia na Msumbiji ndo nchi zilizokaribu mno na TZ kiitikadi kuliko nchi yoyote ya EAC lakini Zambia kiingereza tupu na Msumbiji kireno tupu.
Mie kwa ushauri wangu kama tunataka kuwe EAC yenye nguvu na hatimaye shirikisho ni lazima kwanza tuanza kujenga mahusiano mazuri kati ya kenya na Tanzania halafu ndio baadae tuanze kufikiria kushirikiana kiuchumi. Lakini kwa jinsi historia kati ya TZ na kenya ilivyokwenda haiwezekani kabisa Tanzania ikaitrust kenya labda kama itatokea Tanzania ikashikwa na wafanyabiashara wanaotegemea sana soko la EAC.
Hapa unasema kuwa watu kama waganga na waliofeli mitihani ndio hupenya mipaka ya kenya. Ni hii dhana kuhusu watu wenu infanya mufeli katika majukumu yenu. Umenidhihirishia tatizo moja yenu. Hawa waliofeli mitihani wanaeza kutumika katika sekta za ujenzi na biashara. Lakini wakija mahali kama USIU inamaanisha wamepata kitu walishindwa kupata hapo. Pili, mumesalia SADCC kwa maana rahisi kwamba nchi za Afrika kusini zinangangana kujikwamua kutoka kwa mifumo duni za uongozi pamoja na kuwa chini kibiashara, vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hivyo mnataka maisha rahisi, hampendi competition hapo ndipo ukweli ipo.