Kenya: Nyumba ya Makamu wa Rais William Ruto yashambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
3bafaf3d48d4a3c7db7f45f1efa7fd9d.jpg
85b0c0009ac83e73b1aae211d11218af.jpg
Watu wasiojulikana wameshambulia nyumbani ya mashambani ya Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto Magharibi mwa Uasin Gishu Kaunti, ripoti zinasema.

Ripoti katika eneo hilo zinasema kuwa washambuliaji hao waliwashinda nguvu polisi mmoja katika lango la nyumba hiyo na kuingia ndani.

Ufyatulianaji wa risasi uliendelea katika nyumba hiyo ambayo imezungukwa na maafisa wa polisi.

Bwana Ruto hakuwepo wakati huo.

Kisa hicho kinajiri siku 10 kabla ya Kenya kufanya uchaguzi wa Rais, Ubunge na ule wa Kijimbo.

Makamu wa Rais alikuwa alikuwa ameondoka saa chache kabla ya uvamizi huo ili kuhudhuria mkutano wa kampeni katika mji wa Kitale, ambapo alijiunga na Rais Uhuru Kenyatta.

Kenyatta anatetea kiti chake cha urais mwezi ujao.

Huku uchaguzi wa 2013 ukifanyika kwa njia ya amani kulikuwa na ghasia mbaya za baada ya uchaguzi 2007 ambazo zilisababisha vifo vya watu 1000 huku wengine 600,000 wakiwanchwa bila makao

Hata hivyo wataalamu wanasema hawatarajii kuona kiwango cha ghasia kama hicho kufuatia uchaguzi wa Agosti 8.

Chanzo: BBC
 
Washambuliaji wasiojulikana wameshambulia nyumbani kwa Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto eneo la Sugoi.

Kwa mujibu wa televisheni ya KTN ya nchi hiyo, mpaka sasa vikosi vya usalama vinaendelea kupambana na washambuliaji hao na inasemekana wapiganaji hao wamejificha ndani ya nyumba hiyo.

Hivi yale ' masalia ' ya Umafia wa aliyekuwa ' Mafia ' Mkuu nchini Kenya Marehemu Nicholas Biwott ( anayesifika kwa mauaji ya Wanasiasa wengi nchini Kenya ) yamemalizwa?
 
Hivi yale ' masalia ' ya Umafia wa aliyekuwa ' Mafia ' Mkuu nchini Kenya Marehemu Nicholas Biwott ( anayesifika kwa mauaji ya Wanasiasa wengi nchini Kenya ) yamemalizwa?
Mkuu.. Kwa namna siasa za Kenya kwa sasa na nikipima kifo cha Waziri Nkaissery

Nashidwa kuelewa uelekeo wake.!

Tuwaombee amani itawale jirani zetu
 
Huo ni mpango wa kuleta tension kwenye uchaguzi ili watumie jeshi. Hii ni movie part 1
 
Siasa na madaraka ni kitu kibaya sana hawa jamaa walianza na kipindupindu sasa mashambulizi this time Kenya mambo magumu
 
Mkuu.. Kwa namna siasa za Kenya kwa sasa na nikipima kifo cha Waziri Nkaissery

Nashidwa kuelewa uelekeo wake.!

Tuwaombee amani itawale jirani zetu

Na watauwana sana tu Mkuu. Taarifa za chini kabisa kutoka kwa ' wafuatiliaji ' wa Siasa waliopo huko nchini Kenya wanasema kwamba kuna uwezekano Raila Odinga na mwenzake Kalonzo Musyoka safari hii wakaibuka washindi kutokana na kwamba sasa wamejipanga kwa hila / hujuma / ngendembwe zote na kuna mahala nasikia wameshamshika pabaya Kenyata na Ruto hivyo kupelekea wao kuwa na hali mbaya.

Kuanzia sasa na hadi siku moja kabla ya upigwaji Kura hizo tutegemee makubwa kwani kama akina Uhuru na William walisababisha yale ' mauaji ' makubwa yaliyopelekea kuwa na post election violence nina uhakika hata safari hii tena baada ya kuona wanaelekea kushindwa basi ndiyo wakasababisha ' mauaji ' makubwa mno.
 
He is enforcer of the president. The guy who do all the dirty jobs. Sometimes shit hit the fan, and you reap what you saw. Ukitumia nguvu pia watu watakufuata kwa nguvu. Action and reaction are equal and opposite.
 
If you hear the gunmen have been neutralized, killed and no bodies seen just know Osama mission like executed.
Anyway let's watch.
 
Back
Top Bottom