KENYA: Mwanamume adai Polisi humkamata ili kujiburudisha na mkewe kimahaba, ajisalimisha

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
6cdd968d0e380216df5c4ed25c35b464.jpg
Mwanamume mwenye umri wa miaka 39 aliye baba wa watoto wawili wenye umri wa miaka miwili na minne, amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Muthithi, Kaunti ya Murang'a akitaka aandikiwe makosa yake yote maishani mwake na kisha ashtakiwe rasmi

Anadai amekuwa akikamatwa kila Ijumaa au siku za Sikukuu na kutupwa ndani ya seli na huwa anaachiwa siku ya kupelekwa mahakamani bila kushtakiwa

Amesema kuwa uchunguzi wake umebaini kuwa afisa wa polisi wa kituo cha Muthithi ambaye huwa na urafiki wa kimahaba na bibi yake na ndiyo sababu huwa anakamatwa ili aondoe 'Jam' katika uhusiano huo haramu

"Leo nimejitokeza katika kituo hiki cha Muthithi nikitaka niandikiwe makosa yangu yote ambayo nashukiwa naweza nikayatenda siku zijazo za wikiendi na za Sikukuu, nataka niwe huru kutokana na dhuluma hii ya kukaa na wasiwasi kila Ijumaa ikiingia au kukiwa na holidei,"alisema

FARAGHA

Maafisa wa kituo waliokuwa katika kituo hicho walionekana kuchanganyikiwa huku wengine wanadai wana ufahamu wa dhuluma ambazo huwa anapitia Mwanamume huyo wakimpa ushauri pembeni kuwa ang'ang'anie kukombolewa kutoka dhuluma hiyo

Afisa mmoja katika kituo hicho aliambia Swahilihub kuwa hawafurahii jinsi mwanamume huyo hupewa adhabu za bure na 'tunajua kuwa mwenzetu hapa huwa anakamata ili apate nafasi ya kujiburudisha na mkewe kimahaba'.

Alisema kuwa huwa wanamhurumia lakini kwa kuwa afisa huyo ana Cheo 'huwa hatuna la kufanya ila tu kumhurumia'

Mwanamume huyo ameshauriwa na weledi wa masuala ya polisi na utaratibu wa mahakama kwamba aandike barua rasmi ya kulalamika kwa Kamanda wa polisi wa Kaunti hiyo na kisha ainakili kwa tume ya kupiga msasa utendakazi wa maafisa wa polisi (IPOA) na pia tume ya huduma za polisi (NPSC)

Afisa mmoja alimsaidia mwanamume huyo kupata ushahidi wa kukamatwa kwake mnamo Desemba 23 na ambapo aliachiliwa huru Desemba 27 bila mashtaka yoyote na ambapo alifika nyumbani alifahamishwa kuwa mkewe alitoweka siku hiyo hiyo ya kukamatwa kwake na akarejea nyumbani siku hiyo hiyo ya kuachiliwa

Tume hizo huwa na uwezo wa kuchunguza ukosefu wa uadilifu kwa maafisa wa polisi na kila anayepatikana akiwa na makosa huwa anaadhibiwa kwa mujibu wa kanuni na utaratibu wa utendakazi wa kikosi cha polisi.

Chanzo : Taifa Leo
 
Duh aisee watu wanadhuluma hatari..
Mwanamke ni mkatili sana yaani anakubali mume wake akateseke rumande kwa ajili ya uzinzi wake.!?

Tuwe na utamaduni wa kuchunguza baadhi ya makabila
tukitaka kuoa
 
Back
Top Bottom