KENYA; MBUNGE ANYWA SUMU BAADA YA KUZOMEWA NA WANANCHI

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
27,778
30,749
MBUNGE Mwakilishi wa Wanawake wa kaunti ya Baringo amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi huku kukiwa na madai kuwa huenda alikunywa sumu.


Bi Grace Kiptui alipelekwa katika Nairobi Hospital Jumatatu wiki hii, siku mbili baada ya mkutano wa Naibu Rais William Ruto eneo la Kabarnet, Baringo.

Siku hiyo, Bi Kiptui aliandamana na Bw Ruto kwenye mkutano wa kuwahimiza wakazi kujisajili kuwa wapigakura.
Lakini Bw Ruto alipomwita mbunge huyo wa kaunti kuhutubu, umati ulipiga kelele na kumzomea vikali.

“Kila alipopeleka kipaza sauti mdomoni, umati ulimzomea.
Hatimaye alirejesha maikrofoni hiyo bila kuzungumza hata neno moja,” alisema mmoja wa wandani wake ambaye aliomba asitajwe.

Inadaiwa siku iliyofuata, mbunge huyo aliamua kunywa sumu kutokana na fedheha aliyopata mbele ya Naibu Rais.

Lakini mshirika wake wa karibu, ambaye pia aliomba tusimtaje, aliambia Taifa Leo kuwa Bi Kiptui alilazwa kutokana na uchovu, kwa kuwa kabla ya mkutano huo, alikuwa ametoka hospitalini.
“Alikuwa amelazwa kwa wiki nzima.
Alipotoka hospitali, aliagizwa na daktari apumzike.
Lakini aliposikia kuwa Naibu wa Rais anatembelea kaunti yake, akajitokeza na kuandamana naye.
Ikizingatiwa huu ni msimu wa kiangazi, uchovu wa wikendi hiyo ulimlemea,” akasema.

Hata hivyo, kuna taarifa pia kwamba huenda mbunge huyo alitaka kujitoa uhai kutokana na mzozo wa kifamilia.

Baadhi ya watu wake wa karibu wanaamini huenda shinikizo hizo zimemlemea na kumdhoofisha kimawazo.

Bi Kiptui pia amewahi kuhusika kwenye ajali mbili za barabani. Mwezi Septemba mwaka jana, gari lake lilibingiria eneo la Chepkogon, kwenye barabara ya Eldama Ravine -Saos -Tenges Kabarnet.
 
Back
Top Bottom