barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Wakati tukiendelea na kampeni ya kuutarifu ulimwengu kuwa "Olduvai Gorge" ipo Tanzania na si Kenya kama ambavyo Mwanadada wa Kikenya alivyouambia ulimwengu,katika mitandao ya kijamii kumezidi kusambaa kwa picha za ndege ya KQ aina ya B777 inayoonyesha "Fuselage Name" ya "Mt.Kilimanjaro".Hali hii imezua malalamiko mengi kwa watu mitandaoni na kusababisha watu kuona Kenya wanatumia vivutio vyetu kuitangazia dunia kuwa vinapatikana nchini kwao Kenya.Hii inatokana na malalamiko ya muda mrefu ya Tanzania kuituhumu Kenya kupata watalii kwa mgongo wa vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.
Ukweli ni kuwa hakuna "makosa" yoyote ambayo Kenya kupitia ndege za shirika lake la Taifa(National Carrier) la Kenya Airways linafanya,kwenye ulimwengu wa usafiri wa anga,shirika la ndege la Taifa huwa ni kama "Flying Ambassador".Kuiwakilisha nchi na yote yanayoihusu kule inapokwenda na kutua,zaidi ya yote mashirika haya yamekuwa yanatumia "fuselage name" za vivutio vya utalii kuelezea ulimwengu kuwa ukipanda shirika hili la ndege basi unaweza kufika mahali fulani palipo na kivutio fulani.Kwa upande wa Afrika Mashariki,shirika la ndege la KQ limekuwa likitumia "fuselage name" kama "Mt Kilimajaro","Victoria Falls","Maasai Mara" nk kuulezea ulimwengu kuwa popote unapokuwa duniani ukipanda Kenya Aireays utafika katika vivutia hivyo.
"Fuselage Name" haifanywi na KQ(Kenya Airways) tu,bali hata shirika la ndege la KLM limekuwa likitumia "fuselage Name" ya "Mt Kilimajaro" kwa ndege yake moja aina ya B777 PH-BQP inayofanya safari zake toka Ulaya kwenda nchi za Asia.Hii inawasaidia KLM kupata abairia wengi wanaotoka nchi za Asia na kutaka kuja Mlima Kilimanjaro,kuonekana kwa fuselage name hii itafanya abiria wengi kukata tiketi za KLM wakijua kuwa watafikishwa moja kwa moja kuuona Mlima Kilimajaro,itakumbukwa kuwa shirika la KLM hufanya safari zake kila siku kutoka Amsterdam-Kilimajaro(KIA)-Dsm na baadae kurudi Amsterdam.
Hii haifanywi na KLM na KQ tu,hata shirika la ndege la Ujerumani baada ya kuzindua ndege yake mpya aina ya Airbus 380(A380) imeipa ndege hiyo jina la "Johanesburg" sababu limeanzisha safari za kwenda Afrika ya kusini.Ndege nyingi za Swiss Air zina majina ya vivutio vinavyopatikana nchi nyingine za Ulaya,na hivyo kuwahakikishia abiria kuwa wakipanda Swiss Air wana uhakika wa kufika katika vivutio hivyo vya utalii.
Kuna mambo ya kulalamikia lkn si haya,sisi tunapaswa kuirudisha ATCL yenye nembo ya Twiga wetu anagani.Pembeni ya ndege zetu za ATCL kulikuwa na maandishi yameandikwa "WINGS OF THE KILIMANJARO",lakini pia ndege nyingi za ATCL zilikuwa na "fuselage Name" kama "Serengeti","Manyara","Ngorongoro","Zanzibar" nk.Leo tunao Precisiona Air wanafika Nairobi tu...baadhi ya "Fuselege Name" zake ni "Rombo","Kilimajaro","Iringa","Musoma" na "Mwanza".Tuache kulalamika kwa baadhi ya mambo,tusideke kwa kuombaomba "huruma" ya kuonyesha tunadhulumiwa,dunia ya leo ni "ubabe" na "ukatili" wa kutetea cha kwako na kulinda vyako.Nilipofuatilia mzungumzaji baada ya Miss Odinga kwenye lile Kongamano la IYLA aliposema "Olduvai Gorge" ipo Kenya,mzungumzaji aliyefuatia alikujai kuzungumzia "Maendeleo ya Technolojia na Vijana",kabla ya kuanza mada yake akasema "Ninamshukuru leo Rosemary,nilikuwa najua Olduvai Gorge ipo East Africa,lakini leo nimejua mahususi kumbe ipo Kenya,ndio uzuri wa kukutuianisha vijana toka nchi mabalimbali ulimwenguni".Bado naendelea kufuatilia majina ya vijana wa Kitanzania walioshriki mkutano huo wa IYLA na kwanini hawakujibu hapo hapo,lakini toka August 215 leo baada ya mitandao ya kijamii kama JamiiForums kuibua dhihaka hii ndio Tanzania Tourism Board wanaibuka na tamko.Aibuuu!!!
Fly Emirates ilitumia fursa ya Kombe la Dunia 2014 na kujibandika "machata" ya kombe la Dunia na kunadika "Fuselage name" za miji yote kombe la dunia lilipokuwa linachezwa nchini Brazil..Kwao ilikuwa fursa na kwa Brazil ilikuwa ni kutangaza miji yao bila ghalama yoyote.Tuitumie fursa ya Wakenya kututangazia Vivutio vyetu bila ghalama kupitia shirika lao la KQ.