Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Nchi ya Kenya baada ya kuandika Katiba yake mpya imeweka hiyo ambayo WatanZania wafuasi wa Lowasa & Co. wanaiita Tume huru, ambayo wanataka na sisi pia tuwe nayo kwamba kwa maneno yao hiyo ndiyo itahakikisha Uchaguzi wa TZ kuwa wa huru na haki kwa mujibu wa wana ukawa, lkn wasichokijua ni kwamba mpaka aleo hii wapinzani wa Kenya chini ya Raila Odinga ambaye alikuwa Makamu wa Raisi wakati wa uchaguzi na alishiriki kwenye uundwaji wa hiyo Tume anasema kwamba aliibiwa kura, yaani Uhuru Kenyata aliiba kura na hivi sasa kuna ishu kubwa na Tume hiyo kwamba haitendi haki!
Hii inaonyesha kwamba hapa Afrika sisi ni watu wa kutafuta visingizio siku zote inanikumbusha maneno ya Raisi Kikwete aliyesema Mwafrika huwa hakubali kushindwa hata siku moja hivyo hata hapa TZ kama tukiwa na Tume kama ya Kenya bado hakutaondoa malalamiko ya wale watakaoshindwa, hivyo kila kitu kibakie kama kilivyo leo!