Lazima ataukwaa tu, maana sina hakika kama anaweza kuingia kwenye coalition govt bila ya kuahidiwa nafasi nono (including u-VP).
Nimesikitishwa na kitu kimoja kwamba vile viti 12 vya wabunge wa kuteuliwa siyo sheria, bali yalikuwa ni makubaliano tu. Kwa hiyo kuna hisia kwamba kwa kuwa Kibaka amepata viti 35 tu, anaweza kuvichukua viti vyote 12 akateuwa watu wake ili awape nafasi za uwaziri.
Katiba za nchi za Afrika zina mambo! Niliwacheka Malawi wakati Bingu anaki-dump chama kilichomuingiza Ikulu na kuunda chama kipya. Katiba ya Malawi ilikuwa haiongelei lolote kama Rais akijivua uanachama, lakini mbunge akijivua na ubunge anapoteza. Sasa ndiyo haya ya Kenya!
Hapana, hiyo iko kwenye Katiba. Hebu tafuta tovuti ya bunge la kenya utakuta hii iko stipulated kabisa kuwa watatuliwa kulingana na proportion ya wabunge waliochaguliwa kwa kila chama.
Kichuguu,
Ni kweli haiko kwenye katiba. Ilikuwa ni makubaliano, ambayo vyama vote viliafiki lakini sasa Kibaki anaweza kudharau kama alivyofanya kwenye suala la kuunda katiba mpya.
Hata hivyo nimeangalia kwa makini nikagundua kuwa hiyo ni Guide tu wala siyo legal ducument.Composition
The Parliament consisted of two hundred and ten (210) elected Members of Parliament,
twelve (12) nominated through proportional representation of the Parliamentary parties and
two ex-officio Members, the Speaker and the Attorney General.
But the country has been shocked by the deaths of dozens of people - mainly Kikuyu, the same tribe as Mr Kibaki - in a church that was torched in the Rift Valley town of Eldoret.
Raila na wenzako jamani angalieni, maana kuna mbinu za kuonyesha ODM ndio wauaji na kwamba kuwapunguzia imani kwa wananchi. Upo uwezekano mkubwa kwa wanaotaka madaraka kama ilivyo kwa madikteta wengi duniani kuwatoa kafara hata watoto wao ili wapate madaraka. Sitoshangaa kusikia kwamba Kibaki anaua Wakikuyu ili ionekane kwamba ODM ndio inayoua. Inawezekana makachero wa Kibaki wakafanya fujo na kupora ili ionekane kwamba ODM ndio wahalifu, ili watangazwe kuwa ni magaidi. Baada ya kuapishwa kwa nguvu sasa watatumia mbinu zote kuhalalisha ikiwamo kuonyesha kuwa ODM hawafai kutawala kwa kuwa wana ukabila na ni WAHUNI. Kuweni macho muangalie kwa macho yote.
Kazi ipo. Jamani tukiendelea kufuatilia haya matokeo tuwe tunajiuliza sisi watanzania tutafikia lini hatua ya ushindani kama ya hawa wenzetu? tufanyeje ili nasi tufike hapo? Nafikiri wazo moja ni sisi "elites" tunaoweza angalau kushika keyboard kushiriki kikamilifu katika kujenga upinzani badala ya kukaa kuwalalamikia na/au kuwasifia akina Wangwe na Zitto tu design ya football fans! Ndivyo walivyofanya wenzetu Kenya.
Forget about kurudia kuhesabu kura ili haki ipatikane, this time kurudia kuhesabu will be on favor of Kibaka. Muda wote waliokaa kimya wameutumia kurekebisha kura zote. I'm telling you the truth soon Kibaki atakubali kura zirudiwe kuhesabiwa kisha utajionea madudu....kumuomba Kibaki ajiuzulu mara moja hili kura ziesabiwe upya.
K-T Hivi huyu jamaa michuki minister wa security kenya does he really have that powers to be in office at this juncture maana. i find it ironical for him to be ordering while he was voted out in his constituency. does he have a scandal that he is protecting at any cost maana he is very active to ensure that everything settles.
Nimeanza kuona kuwa sasa kweli Kibaki amerudi and he is there to stay. Watu wameanza kuizoea hali na kidogokidogo wanaikubali, hata hapa kwenye forum wanaonesha hivyo. Hasira zimepungua. Punde mambo mengine kama mahitaji ya kimaisha (chakula, huduma mbalimbali) yatachukua nafasi, na watu watarudi kuwatafutia watoto wao nafasi za shule, ni januari hii. Chuma kinaelekea kupoa, hakitapondeka tena. Raila na wenzie wamesahau msemo huu "strike the iron while it's still hot". Bw Odinga, chuma chapoa hicho, kallaghabaho!
Mambo haya yapo sana kwetu. Ukipata taarifa za msiba unajitupa chini na kujigalagaza huku ukiangua kilio, unachafuka kila mahali. Ajabu siku ya mazishi unaonekana na suti mpya nyeusi, tena nyote na nduguzo kama sare, hata tunashangaa mlipataje muda wa kufikiria sare kama mlikuwa na uchungu kiasi hicho. Baada ya maziko, siku hiyohiyo inafuata pilau, ndizi mbivu na vinywaji. Wale waliokuwa wanajigaragaza chini tunawaona wanacheza karata na kutaniana! Kila kitu kinasahaulika, maisha yanaendelea! Ndivyo tunavyosahau msiba, na ndiko Raila na wenzie wanakoelekea, hivi punde watasahau yote, kama mwendo ndio huu wa kusuasua. Yetu macho!
Nasikia JK anakwenda Kampala kushauriana na M7 ili kujua hatima ya Kenya. Mimi nafikiri wote hawana la maan la kushauri kwani wote wameingia kwa kama Kibaki na Kibaki anajua hilo. So JK ni kutumia pesa ya walipa kodi bure
Kweli nimeona...Adding to the chaos, Kenya's electoral commission head Samuel Kivuitu said: "I do not know" when asked if Kibaki won the vote. The comment by Kivuitu, who pronounced Kibaki victor on Sunday, stunned Kenya and cast further doubt on the result.[/B]..what a shame?? Ni aibu tupu! mtu mizima na akili timamu?? Kuweweseka na kutoa majibu ya aina hii!!Kama si wizi na kusutwa na damu inayomwagika kote nchini kenya ni nini??Kuna habari nimeiona inasema kuwa Samuel Kiviutu (head of Electoral Commission of Kenya) amekaririwa akisema hajui kama Kibaki alishinda uchaguzi.
Anasema alilazimishwa na wakubwa kutangaza mapema matokeo.
http://uk.news.yahoo.com/rtrs/20080102/tts-uk-kenya-2c15123_1.html
Kweli nimeona...Adding to the chaos, Kenya's electoral commission head Samuel Kivuitu said: "I do not know" when asked if Kibaki won the vote. The comment by Kivuitu, who pronounced Kibaki victor on Sunday, stunned Kenya and cast further doubt on the result.[/B]..what a shame?? Ni aibu tupu! mtu mizima na akili timamu?? Kuweweseka na kutoa majibu ya aina hii!!Kama si wizi na kusutwa na damu inayomwagika kote nchini kenya ni nini??