Kenneth Kaunda atimiza miaka 93

Kenneth Kaunda atimiza miaka 93

Nimeona hizi picha nimejikuta natabasamu peke yangu, hakika hawa watu walikuwa na uchungu na Afrika kwa ujumla Allah awapunguzie adhabu za kaburi, hawakuwa waigizaji na waliwapenda kwa dhati wananchi wao
 
Mungu Aendelee Kumlinda Dr KK.

Ndio faida ya kutenda mema na haki kwenye uongozi..

KK hakuwa mbadhilifu, hakuwa mvunjaji wa Katiba ovyo ovyo kama Viongozi wengi wa hivi sasa na KUBWA kupita yote alikuwa MWANA DEMOKRASIA wa ukweli.

Ndio maana kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwisho alioshirik,i alishindwa kwenye sanduku la kura na Frederick Chiluba na kwa amani kabisa akakubali kuwa ameshindwa akakabidhi madaraka.

Hakufanya chembe ya dhuluma kwa kumpigia "Jecha" wa Zambia simu abadili matokeo na yeye ndio atangazwe mshindi japo alikuwa na uwezo huo.

Ndio maana mpaka kesho wananchi wa Zambia wanampenda na kumkubali.

Live Long Dr KK.
KK kwenye uchaguzi ule aliruhusu matokeo kurushwa moja kwa moja kutoka vituo vya kupigia kura na kutangazwa na ZBC (tbc ) hivyo kila mtu aliona mwelekeo wa matokeo (transparency ). Hakuna aliesubiri tamko la tume ya uchaguzi kujua nani mshindi. Kwa hili alionyesha njia ambayo wenzake wengi hadi leo wanakwepa. Rejea yaliyotokea kenya, Zanzibar etc kwa system ya KK tusingefika huko. BIG UP KK. Mola ampe maisha marefu kwa hili.
 
MUNGU mkubwa na MUNGU hamtupi mja wake, Nakumbuka jinsi Rais wa pili Frederick Chiluba alivyomweka ndani Mzee Kaunda mpaka Kaunda akagoma kula na Mwl Nyerere akaenda Zambia na kula naye Mzee Kaunda na kumuuliza swali mmoja moja tu F.Chiluba kwanini unamtesa Mzee Kaunda?? Baada Nyerere kuondoka Chiluba alimwachia huru Mzee Kenneth Kaunda.

Na ndiyo maana ktk msiba wa Mwl Nyerere Mzee kenneth Kaunda alilia sana na alishindwa kumalizia kusoma utenzi aliouandika kwa majonzi.

Frederick Chiluba Rais wa pili wa Zambia alifariki June 2011

Dr Levy Mwanawasa Rais wa tatu wa Zambia alifariki August 2008

Michael Sata Rais wa tano wa Zambia alifariki October 2014
Aiseee maajabu sana Lungu naona anapeta
 
Hivi ile issue ya mwanae aitwae Kambarage Kaunda aliyeua iliishaje? Alinyongwa au kufungwa maisha?
 
Sema ndio mapenzi ya mwenyezi Mungu alimchukua Mwalimu tukiwa bado tunamuhitaji kama trafiki wa nchi,maana tangu aondoke yeye madereva hawatak kupangiwa pa kupita nadhani wote mnajua sehemu ambayo trafik hayupo madereva ufanyaje.R.I.p mwalimu happy birthday Kaunda.
 
e8bcc98ff48a3a07c1248488ff050ff1.jpg
Kombati, cdm kombat typical. The true combatant's wear! Pepoooz, only that Mugabe is overpowered by the Jechaz of Zimbabwe, he was a true combatant then!
 
Kila la kheri Dr Kaunda..

..mwenzio ametuacha wakiwa huku...kuna lijitu lina roho mbaya sana linafukuza kazi wasio na vyeti lkn ndugu zake linawaacha, limeacha sembe inauzwa ghali kuliko petroli hata halijali!! Lipigie hata simu tu uliambia nchi hii sio yake na watu wa kwao, ni ya watanzania wote!
 
Mungu aendelee kumuongezea miaka ya kuishi dunia.HUYU ndiye alikuwa rafiki wa kweli wa Tanzania.
 
Tunapomuongelea comredi huyu,tusisahau kukiongelea chama cha UNIP ambacho kama CCM inaelekea huko
 
Back
Top Bottom