Kenneth Kaunda atimiza miaka 93

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda, mmoja wa viongozi wa mwisho walio hai barani Afrika walioshiriki katika kupigania uhuru wa nchi zao ametimiza miaka 93.

Bwana Kaunda aliongoza Zambia kupata uhuru mwaka 1964 na kuwa rais wake wa kwanza.
Baadhi ya raia wa Zambia wamekuwa wakisambaza picha ya baba mwanzilishi wa taifa hilo.

Picha iliyo chini hapa ni kutoka kwa kumbukumbu wakati bwana Kaunda alikuwa akishiriki kwenye mazungumzo na waingereza mwaka 1961.

_95827930_bcf1cd48-dc8d-4acf-b21c-b6612f8e549e.jpg
 
Itabidi wakutane Kaunda, mzee Mwinyi na Mugabe waongee wawili matatu

Wote age yao ni above 90
 
Mungu Aendelee Kumlinda Dr KK.

Ndio faida ya kutenda mema na haki kwenye uongozi..

KK hakuwa mbadhilifu, hakuwa mvunjaji wa Katiba ovyo ovyo kama Viongozi wengi wa hivi sasa na KUBWA kupita yote alikuwa MWANA DEMOKRASIA wa ukweli.

Ndio maana kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwisho alioshirik,i alishindwa kwenye sanduku la kura na Frederick Chiluba na kwa amani kabisa akakubali kuwa ameshindwa akakabidhi madaraka.

Hakufanya chembe ya dhuluma kwa kumpigia "Jecha" wa Zambia simu abadili matokeo na yeye ndio atangazwe mshindi japo alikuwa na uwezo huo.

Ndio maana mpaka kesho wananchi wa Zambia wanampenda na kumkubali.

Live Long Dr KK.
 
Huyu ni mmoja wa majabari ya Viongozi wa Africa wengine walikuwa ni Mwalimu Julius K Nyerere, Kwame Nkrumah, Nelson Madiba Mandela. Mungu ampe afya njema na maisha marefu. Hahitaji kupiga piga kelele huyu ili aombewe kama nanihii, matendo yake wakati alipokuwa madarakani ukiyasoma unaona kabisa alikuwa kiongozi mzuri huyu.

Hili linanii si lina maovu mengi ndiyo maana linataka liombewe
 
  • Thanks
Reactions: BAK
MUNGU mkubwa na MUNGU hamtupi mja wake, Nakumbuka jinsi Rais wa pili Frederick Chiluba alivyomweka ndani Mzee Kaunda mpaka Kaunda akagoma kula na Mwl Nyerere akaenda Zambia na kula naye Mzee Kaunda na kumuuliza swali mmoja moja tu F.Chiluba kwanini unamtesa Mzee Kaunda?? Baada Nyerere kuondoka Chiluba alimwachia huru Mzee Kenneth Kaunda.

Na ndiyo maana ktk msiba wa Mwl Nyerere Mzee kenneth Kaunda alilia sana na alishindwa kumalizia kusoma utenzi aliouandika kwa majonzi.

Frederick Chiluba Rais wa pili wa Zambia alifariki June 2011

Dr Levy Mwanawasa Rais wa tatu wa Zambia alifariki August 2008

Michael Sata Rais wa tano wa Zambia alifariki October 2014
 
Hawa jamaa walikuwa kweli wanakisimamia walichokuwa wanakiamini, ni majembe ya ukweli kabisa

Sam Nujoma, Kenneth Kaunda, Samora Machel, Nyerere, Mugabe na Dos Santos
image.jpg

Kaunda, Samora na Nyerere
image.jpg

Nujoma, Samora Kaunda, Mugabe
image.jpg
 
Harakati za Tazara

Nyerere na Kaunda wapo na Wachina wakijadili ujenzi wa TAZARA
image.jpg

Siku ya ufunguzi wa TARAZA Kapiri Mposhi -Zambia
image.jpg
 
Chiluba baada ya Kuchukua nchi, Kaunda alikuwa kama Mpinzani, kwenye mwaka 1997 mwishoni Chiluba alimtia ndani Kaunda. Na Nyerere alienda kumtembelea Gerezani na kumshinikiza Chiluba amtoe Kaunda Gerezani

Back
Top Bottom