Kemebose Kagera wakisherekea matokeo yao

Kemebose Kagera wakisherekea matokeo yao

Fyodor Dostoevsky

Senior Member
Joined
Mar 23, 2022
Posts
121
Reaction score
85
Shule ya kwanza matokeo ya kidato cha sita, Kemebose kutokea Kagera Tanzania wakisherekea matokeo yao kwa kuzunguka mji mzima!.

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Wanasherehekea ujinga tu. Kwa elimu gani! Hii hii ya kukariri maswali na madesa! Wakirudi nyumbani kutwa wanashinda ndani kuangalia muvi.

Kama Taifa, ni wakati sasa wa kuwa na mitaala yenye kuwaongezea zaidi wanafunzi maarifa na ujuzi, kwa ajili ya maendeleo ya kizazi cha sasa na kile cha baadaye! Badala ya hii mitaala ya sasa ambayo imeegemea zaidi kwenye kumkaririsha mwanafunzi mambo mbalimbali, huku mengine yakiwa hayana tija yoyote ile katika maisha yake.
 
Acha wivu...kwa hiyo wasisherekehe kisa elimu ni mbovu...
 
Acha wivu...kwa hiyo wasisherekehe kisa elimu ni mbovu...
Kwa elimu hii hii ya kukariri madesa na kusovu maswali mengi ya NECTA ndiyo nione wivu! Mtoto anafaulu mtihani, halafu anarudi mtaani akiwa hana maarifa yoyote yale kichwani!

You are not serious. Si bora hata mwanafunzi aliyehitimu mafunzo ya VETA akishangilia, kidogo nitamheshimu.
 
Hao wazamani ambao hawakuwa wa kukariri,walivumbua nini hebu tukumbushe
 
Hao wazamani ambao hawakuwa wa kukariri,walivumbua nini hebu tukumbushe
Kuna sehemu yoyote niliyosema wa zamani walivumbua kitu!
Nimeongelea habari ya mitaala!

Ni wakati sasa wa kuwa na elimu ya kumjenga mwanafunzi kujitegemea, na pia kupambana na dunia ya sasa! Badala ya hii elimu ya kurithi kutoka kwa wakoloni, ya kuwaandaa wahitimu kuajiriwa kwenye ajira ambazo kwa sasa hazipo.

Huwezi kushangilia ujinga kwa kujiona una akili, kwa sababu tu ya uwezo mkubwa wa kukariri madesa na mitihani ya marudio. Ni wakati wa kuwa na wahitimu wenye maarifa na ujuzi mwingi kichwani, na siyo mabingwa wa kukariri mitihani.
 
Kwangu mimi mhitimu wa veta ndio mhitimu sahihi kwa hii nchi.

#MaendeleoHayanaChama
Uko sahihi kabisa. Maana mtoto akitoka huko, kuna kitu anaweza kufanya ili kujiingizia kipato. Siyo hawa watoto wa Kemebos, St. Francis, St. Mary's, St. Kayumba, nk

Wakitoka huko na 0, au One zao; huishia tu kula na kulala nyumbani, na pia kugombania remote sebuleni na wadada wa kazi! Huku wakisubiria kwenda hatua nyingine ya masomo, au kuhangaika na bahasha mjini wakitafuta ajira za maofisini.
 
Hii elimu yetu jau sana serikali yenyewe wanajisifia kwa kujenga shule kwa hela za uviko huwa najiuliza sawa wameshajenga shule what next? Jibu ni process ile ile inajirudia kukariri tu na kurudi nyumbani kuangalia katuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisifurahie kununua baiskeli eti kwasababu wenzangu wana magar?.
Jamani, mumeona jinsi mitihani ya hivi karibuni inavyo tungwa. Kwa asilimia kubwa inahitaji matumizi ya ulicho jifunza. Pengine ikawa mwanzo wa mabadiliko.
Tusiishie kubeza mtaala, kwa uchumi wetu huu na bajeti ya elimu ambayo haitoshelezi hata kwa practical ndogo ndogo, unadhani itakua rahisi kujenga workshop za kujifunza kwa vitendo.
Ni swala la muda tu, Kazi ziendelee, uchumi ukikua, mitaala itabadilika.
 
Shule ni Darasa na wanafunzi,walimu miundombinu tuambie Kemebos madarasa na walimu wao wako wapi na hiyo shule iko mtaa gani? Hii shule inausajili tu wanafunzi wanachukuliwa shule ya Kaizerege siku ya mtihani tu! Tena kwakuchagua cream students! Tuambie tujue au unaongelea Kaizerege,hii nchi tuna viongozi wa ajabu Wizara ya Elimu imelala usingizi wa pono au Rushwa?
 
hivi sikuhizi wameanza kuweka ranking au maana mwaka jana hawakuweka
 
Back
Top Bottom