Kelele nyingi ni za wapiga dili

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,428
13,936
Hata jogoo ukimkata shingo yake ghafla na kutenganisha kichwa na kiwiliwili kichwa kinaweza kuendelea kuwika.

Hofu na kelele nyingi zinazosikika nchini inawezekana kabisa zikawa ni za wale watanzania wenzetu waliokuwa na shughuli ambazo hazikuwa halali.

Sisi watanzania wa kawaida huku Tanga tunalala nje ya baraza za nyumba zetu usiku ili kupata upepo kutokana na joto kali ndani ya nyumba zetu.

Tumekuwa tukifanya hivyo kwa miaka mingi sana tangu awamu ya kwanza hadi sasa. Hatuna hofu ya kutekwa wala kubakwa, sasa kwanini watanzania wenzetu wachache leo wanalalamika kutekwa na kuliambukiza taifa hofu kuu ya kutekwa?

Tusipuuze kelele zao, lakini lazima tufanye utafiti wa kina ili kufahamu

1. Kubwa wa tatizo
2. Sababu za kutekwa
3. Sababu za hofu yao
4. Historia ya maisha yao ya kiuchumi
5. Nani anawateka na sababu za kuwateka
6. Ni akina nani wana uwezekano mkubwa wa kutekwa kwasababu zipi.
 
Sasa inchi hii nzima watu hawakuwa na cha kufanya? Kweli CCM mnatuchukia watanzania kwa tuliwakosea nini?
Au kuwapa inchi mtuongoze ndio tumefanya kitu kibaya?
 
Ni kweli mkuu hongera sana mwenyekit wa ccm kuwakomesha wapiga dili
*kufuta ajira
*helsb 15%
*No increment
*No fao la kujitoa
*watu wengi kunyimwa mikopo ya elimu ya juu
*kulea jambazi la vyeti huku mamia wakifukuzwa
*Bei ya vitu viko juu hasa vyakula
* Ubabe kwa watumishi wa umma, kulazimishwa kukesha kwenye mwenge, kupigishwa deki n.k
Ukiwa mfia chama na ni msukule wa buku 7 za mzee pole pole huwezi kuona. Kwa kuwa ww mwenyekiti wako ni dikiteta na unakula kwake huwez huwez kuona haya,
WW UNALINDA TUMBO TU
 
Ingekuwa wewe ndiye rais ungefanya nini kama ukiikuta nchi watu wote hawalipi kodi, madawa ya kulevya tele, safari za nje kila siku, mikutano kila siku, watumishi hewa kibao, wanafunzi hewa kibao, nchi inategemea wahisani, mikataba yote feki, wizi wa fedha kwa njia ya epa, edcrow, nk
 
Kelele ni nying sana, basi waatz wote walikuwa wapiga dili.

Watu wanalalamikqq usalamma kuwa mdogo mnadai ni kupiga deal??
Watu wanasema democrasia iko mahtuti ww unasema kupiga deal? Ooooh come one, can't be serious man
 
Mkuu sio lazima ku post

Ww uliokosa cha kuchangia ndo sio lazima kupost....na lazma tukusahidie kujiuliza swali kwanini mtu kama Roma atekwe badala ya kumteka mtu kama Lowassa au sumaye wanaoijua serikali A to Z....na wamekimbilia CDM?.
 
Kelele ni nying sana, basi waatz wote walikuwa wapiga dili.

Watu wanalalamikqq usalamma kuwa mdogo mnadai ni kupiga deal??
Watu wanasema democrasia iko mahtuti ww unasema kupiga deal? Ooooh come one, can't be serious man
Nani kakwambia watanzania wote wanalia we kima!! Nyie wapiga dili ndo mnalia. Sisi hard workers ndo zamu yetu kufaidika. Siyo ile kwenda oficin kidogo tu unatoka na mamilion ya pesa. Wizi ulikuwa umeshakuwa jadi ya mtanzania hata zitto hakuwahi kuuona alipokuwa mwenyekiti Wa PAC mana take na yeye alikuwa anagawiwa chake. Aiae thak you jpm kuwaonesha watanzania wameibiwa mda mrefu na watu kama nyie
 
Swine
 
Hili ndilo linalopeleka nchi shimoni yani mkulu na watu kama nyie hamtaki kusikia uchambuzi wa wataalam mnaamini kila mwenye mafanikio anapiga deal.
Uchumi unadidimia biashara zinafungwa watu wanapoteza ajira makusanyo yatashuka lakini mmekaloa wapiga deal wapiga deal.
Mkija kushtuka itakuwa tia maji tia maji
 
kama si wapiga dili tuonyesheni vijiwe vyenu vya kipato vilipo ili tujue la kuwasaidia. Magufuli ni dereva wa lori, kelele zenu hazimzuii kutufikisha kwenye maendeleo. mtabaki na midomo itemayo lawama sisi leo tulikuwa tunaongelea Dar mpaka Moro train. povu likiwakaukaa tayari tumemaliza majenzi ya Moro mpaka Makutu. na tutakapokuwa na dar makutu tunauanza mwendo wa makutu Tabora. Baba yetu Magu Nyoosha mguu Nyoosha Hakuna cha 50 50 za matrafiki wala sumatra.
 
Ingekuwa wewe ndiye rais ungefanya nini kama ukiikuta nchi watu wote hawalipi kodi, madawa ya kulevya tele, safari za nje kila siku, mikutano kila siku, watumishi hewa kibao, wanafunzi hewa kibao, nchi inategemea wahisani, mikataba yote feki, wizi wa fedha kwa njia ya epa, edcrow, nk
Km watu wote walikuwa hawalipi kodi nchi ilikuwa inaendeshwaje, kwa pesa za mfukoni za Rais? Unga wa sembe leo kg. 1 ni sh 2400, ni kwa sababu ya wapiga dili?
 
Mweee Kavulata kweli unasema hayo?
nakumbuka zamani nilikuwa nikimsifu jamaa yangu mmoja kuwa kapata ajira nzuri sana RTC eti kwakuwa alikuwa na uwezo wa kutoka kazini na mifuko 2 ya sukari kila siku, mimi sikuwa na habari kuwa wizi wake ule ulikuwa unaniathiri hata mimi. Nilidhani alikuwa akiibia serikali sio mimi, matokeo yake dawa hospitalini na huduma nyingine zilikosekana. Na sisi tuliyabatiza mashirika ya umma (SU) kwa jina la S oma U le. Ndo maana ninasema hebu tufanye utafiti wetu sisi wenyewe ili kufahamu ni akina nani wanaopiga kelele sana katika awamu hii na ni akina nani wanaohofia kutekwa na sababu zao na maisha yao huko nyuma.
 
Hili ndilo linalopeleka nchi shimoni yani mkulu na watu kama nyie hamtaki kusikia uchambuzi wa wataalam mnaamini kila mwenye mafanikio anapiga deal.
Uchumi unadidimia biashara zinafungwa watu wanapoteza ajira makusanyo yatashuka lakini mmekaloa wapiga deal wapiga deal.
Mkija kushtuka itakuwa tia maji tia maji
kwa maoni yangu mimi ni heri kuwa na uchumi mdogo halisia kuliko kuwa na uchumi mkubwa wa bandia. Yaani ni sawa na kuwa na hela nyingi ulizolipwa baada ya kumfumania mkeo akiwa na mwanaume mwingine.
 
kwa maoni yangu mimi ni heri kuwa na uchumi mdogo halisia kuliko kuwa na uchumi mkubwa wa bandia. Yaani ni sawa na kuwa na hela nyingi ulizolipwa baada ya kumfumania mkeo akiwa na mwanaume mwingine.
Hilo ndilo linawadanganya watu wanafunga maduka yani badala kutoza ushuru wa kawaida kwa watu wengi wameongeza ushuru watu wanashindwa biashara wanazidi kukaba kwa watu wachache.
Just imagine container la alumium bars ft 40 kwa ajili ya milango na madirisha ni 45 mils
 
Back
Top Bottom