Tanzania inatakiwa kuanza kuwa na sera za mipango miji kama mji wa casino wa Las Vegas, Marekani.
Na hakika wakati Bahari Beach, Kunduchi beach, Silversands n.k ''mjini Dar'' maeneo hayo wakati yakiwa mbali na meneo ya kuishi watu serikali ilitakiwa kufanya eneo hilo kuwa maalum kwa ajili ya starehe, casino, ''red district'' kama Amsterdam na huduma za mahoteli tu, lakini serikali ikaacha watu watumie maeneo hayo kuwa ya makazi ya watu na hatimaye wanaanza kulaumu ''makelele''.
Mfano mwingine eneo la Wazo Hill Dsm labda ilikuwa iwe eneo la viwanda tu lakini serikali ikatoa eneo hilo kuwa la makazi ya watu sasa, wakaazi wanapiga kelele ''uchafuzi wa hali ya hewa''.
Wakulima walikuwa na maeneo maalum, vile vile wafugaji walikuwa na maeneo maalum lakini sasa hakuna sera za namna hiyo matokeo 'mapigano'' kati ya wafugaji na wakulima.