Kazi ya kumsaidia Rais siyo ya Mawaziri tu

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Wabunge wapo kwa ajili ya kutatua changamoto za Wananchi, hivyo ni jukumu lao kumsaidia Mh Rais kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi. Mwaka 2020 Chama kiliwadhamini Wanachama wake kupata ubunge lakini baadhi yao ni mizigo kwa Chama mpaka kwa Wananchi.

Mwaka 2025 CCM ondoeni Wabunge ambao sio msaada kwa Wananchi wala kwa Chama, Mbunge toka achaguliwe hajawahi kuzungumzia Maendeleo ya utekelezaji wa miradi jimboni kwake, hajawahi zungumzia changamoto za jimboni mwake, Serikali imejenga madarasa, Zahanati, Vituo vya Afya, miradi ya maji, barabara.

Mbunge muda wote yuko tweeter kuandika vitu ambavyo havieleweki, Mbunge ni kiongozi ana sehemu ya kushauri Bungeni, anaweza kumfikia Waziri mwenye dhamana, anaweza kumfikia hata Waziri Mkuu kama ana jambo lake la kushauri, ni upuuzi Mbunge kushinda tweeter wakati kuuliza maswali ambayo Wananchi nayo wanajiuliza, Mbunge anashindwa hata kuelezea mfuko wake wa Jimbo.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu Mbariki Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
 
Back
Top Bottom