Kazi ya kujitolea

Wasomi mnabishana jinsi ya kugawana hela baadae, ukifikia phase ya kuhitaji fundi ceiling na decorations we nicheki dm hapo tunaelewana on the spot na tukielewana tunaanza kazi muda huohuo hatuna maneno mengi
Asante kwa ofa mkuu, jengo lilishakamilika
 
Uko sahihi
 
Wazo lako nizuri ila angalau uweke posho . Unapoanzisha kampuni nilazima utenge budget ikiwemo pesa za posho kwa hao
Kwa sababu ni mwanzo, tunaweza kuanza kwa kamisheni kwa kila kazi inayopatikana
 
Kuliko kutafuta watu wajitolee kwnye kampuni yako changa, ni heli utafute kampuni kubwa ujitolee kama kampuni ndogo, jeshi la mtu mmoja ili ujenge company profile, la sivyo watakuja kujitolea kwako na hakuna kazi za kufanya, watabaki wanashinda ofisin na kugonga menu tu bure.
 
Nashukuru kwa ushauri.

Kitu cha kwanza ni kuzalisha bidhaa kwanza, ndipo kazi ya masoko ndio ianze kuitangaza hiyo bidhaa, na dunia pia wajue tunafanya nini.

Kufanya kazi kwenye kampuni kubwa, ni sawa na kusema hizi kampuni zinazotengeneza juisi waungane na pepsi au kampuni ya Coca kuzalisha bidhaa za pepsi/coca na kuacha lengo lao la biashara. Hii ni kuua biashara yako.

Ni bora nianze chini ili kulinda 'brand' kuliko kurukia kwenye kampuni ambazo zipo tayari.

Kwa mawazo niliyonayo, itakuwa kampuni yenye malengo makubwa ya kuteka soko hapa na pale; kwa sababu itakuwa na 'App' yake.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…