Kazi ya kujitolea

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
39,924
Reaction score
61,707
Nina wazo la kuanzisha kampuni ndogo ya ujenzi, ambayo timu yake itakuwa hivi:-​
  • Architecture - 1​
  • Quantity surveyor - 1​
  • Marketing - 1​
Kwa kuwa kampuni itakuwa bado ni changa, haitaweza kulipa mishahara kwa hao wataalamu, lakini itakuwa na uwezo wa kuwapatia chai na chakula cha mchana tu, ndani ya miezi sita.

Baada ya soko kuitikia, ndio tutaanza kupata mapato (mishahara).

Kwa wale wenye hiyo fani na wana nia kweli, njoo hapa jukwaani tujadili.​
 
Vipi mkuu huitaji bodaboda kumzungusha marketing manager around? Mie nipe chai na msosi tuu mafuta juu yangu. Sharti marketer awe mwanamke
 
Kweli wapo, ila ni vigumu kuaminika kwa mteja
Kuaminika nini? Hao mainjinia wanaanza kukupigia mahesabu ya feasibility study, sijui viprogram vya computer animation and transition sijui kupima udogo sijui ratio ya udongo mchanga na maji brahbrah nyingi na hela ndefu ataanza kukupigia sijui "unajua nyumba yako kubwa ina vyuma brahbrsh kila chumba laki 3 mara jumla ya vyumba mxiuuuuuh! @&#$?£&#! Lakini ukimleta fundi maiko hata kama huna ramani ukamwambia kwa maneno ana jua chumba urefu na upana na wima, mnaelewana kesho wanatia timu na vibarua wa uswazi chakula ugali maharage mwiko ni kipande cha mti maji ya kunywa ya visima siku mbili kitu kinaonekana! Hawanaga mambo mengi fundi maiko! Mainjinia tafuteni kazi nyingine maana fundi maiko ndo tulionao kitaa kama mchina na Trump
 
Wazo zuri. Hii hao ni co founder wenzako.. inabidi kuwapa share
 
Kwenye nyumba binafsi inawezekana
 
ata kwambia nawapa mshahara 😄
Pia ni vizuri wakajichukulia kama waajiwa, kwa sababu watatumia majengo ya kampuni, watatekeleza malengo ya muda mrefu na mfupi ya CEO; kampuni ingekuwa iko vizuri, terms zingekuwa ni kuajiri tu hao wataalamu​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…