Kiwi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 1,054
- 990
Heshima kwenu wadau,
Mara kadhaa nimekuwa nikijiuliza swali kuhusu kazi ya Makamu wa Rais wa JMT, Dr. Mohamed Bilal. Job description yake kiongozi huyu wa ngazi ya juu kwenye serikali ni kuweka mawe ya msingi, kufungua makongamano, warsha na semina? Hivi hana kazi nyingine? Kila kukicha kwenye TV, magazeti na mpaka kwenye Michuzi hukosi kumwona akiwa kwenye harakati za ufunguzi ama kufunga mojawapo ya matukio kama hayo. Hivi kweli amekosekana mtu mwingine wa kufanya kazi kama hizo mpaka zifanywe na Makamu wa Rais? Ama ndiyo 'job description' yake inavyosema? Kuna haja gani basi ya kupokea mshahara na marupurupu kibao ya cheo cha Makamu wa Rais kama kazi yake ni sawa na MC kwenye tafrija ambazo kwa Tanzania yetu haziishi?