Kipindi cha ITV kuhusu ripoti barabaran kilichorushwa kwa ustadi mkubwa kimeweka mambo wazi na SAIDI Mwema amakubali kwamba matrafiki wanakula rushwa kwa kwenda mbele utafikiri kiama imefika. Serikali sasa inaweza kuchukua mbinu hiyo kuwanasa maaskari wengine wala rushwa. Maaskari walionyeshwa wakipokea rushwa wanaweza kufukuzwa kazi, je wale waliotoa rushwa watachukuliwa hatua gani? Na Je Jerry Muro aliyerekodi maovu hayo kwa ugunduzi huo na kazi nzuri atapewa zawadi gani?