Wengine wanasema ni ngumu sana kuivurusha CCM madarakani kwa sanduku la kura bila kujali itasimamisha mawe au watu ili yapigiwe kura....
Lakini ukweli mchungu kwa wenzetu hawa wanaosimama ktk imani hii ni kuwa, KILA KITU KINA NYAKATI NA MAJIRA yake bila kujali ni kitamu ama kichungu; kinapendeza au kuchukiza kiasi gani....
MAJIRA na NYAKATI zikifika huondoka na hufa na watu hushangaa na kujiuliza limewezekanaje hili....!!???
Nani alikuwa anajua kuwa Robert Mugabe angekufa juzi?
Nani alijua kuwa huyu anayeabudiwa na baadhi yetu kama "BABA WA TAIFA" hayati Mwl Julius K. Nyerere angekufa na kuoza ardhini?
Hivi kwa waliokuwepo enzi zile za KANU ya Kenya chini ya mtu aliyetukuzwa kwelikweli na baadhi ya Wakenya hata kupachikwa kitangulizi cha "MTUKUFU" kabla ya jina lake, Rais Daniel Arap Moi.....
Nani alijua hata kuweza kutabiri tu kuwa, kufumba na kufumbua angetoweka yeye, chama chake na watu wake wa kikundi cha sifa kama mvuke wa moto?
Nakubaliana na wewe kabisa, kuwa, ni wakati wa Watanganyika wote kufikiri juu ya hatima ya uongozi wa Taifa letu nje ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) na wafuasi wake.....
Kwangu mimi haijalishi itakuwa CHADEMA na Tundu Lissu, Mbowe, Sumaye ama Nyalandu ama yeyote ndani humor; Ama ACT - Wazalendo na Zito Kabwe ama Bernard Membe ama mwingine yeyote ndani mwao humo.....lakini isiwe CCM na chapa yake, baasi inatosha sana.....
For sure, John Pombe Magufuli na CCM yake iwe mwisho 2020. Miaka 66 toka enzi ikiitwa TANU mwaka 1954 hadi ilipojibadilisha na kuitwa CCM mwaka 1977 inatosha....
Wamefanya waliyoweza kufanya, wameshindwa waliyoshindwa......
Kwa ufupi sana ni kuwa, mbwa huyu ni mzee sana. Hawezi kutuletea mawindo tena ili tuendelee kula kitoweo.....
Ana umri wa zaidi ya umri wa kustaafu binadamu kazini wa miaka 60, inatosha na wote tuseme inatoshaaaaa...!!