Kazi kazi kazi kazi

Benny

JF-Expert Member
Jun 6, 2014
3,275
5,392
TANGAZO LA KAZI
Mkurugenzi wa Halmashaya Maji wa Bariadi anatangaza nafasi za kazi themanini na moja (81). Maombi ya kujaza nafasi tajwa hapa chini yanakaribishwa kutoka kwa mtanzania yeyote mwenye sifa zilizotajwa katika tangazo hili.
Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

1. MTENDAJE WA MTAA III (NAFASI 73)

Ngazi ya Mshahara: TGS B

SIFA ZA MWOMBAJI
• Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
• Aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

MAJUKUMU

• Kuratibu na kutekeleza Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri.
• Kuishauri kamati ya maendeleo ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa.
• Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogo na sheria zinazotumika katika Mtaa.
• Kusiamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
• Kutekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo katika Mtaa.
• Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

============

2. MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI III (NAFASI 3)

Ngazi ya mshahara: TGS B
SIFA ZA MWOMBAJI
• Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
• Aliyefuzu mafunzo ya Stashahada (Diploma) kwenye fani ya Maendeleo ya Jamii kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii au vyuo vingine vinavyotambuliwa na serikali.

MAJUKUMU

• Kuratibu shughuli za maendeleo ya jamii katika mtaa zikiwemo za wanawake na watoto.
• Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo.
• Kuwezesha jamii kubuni, kupang, kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo.
• Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na kimaendeleo.

===========

3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 5)

Nafasi 3 Msaidizi wa kumbukumbu masijala ya kawaida.
Nafasi 1 Msaidizi wa kumbukumbu masijala ya Ardhi.
Nafasi 1 Msaidizi wa kumbukumbu masijala ya Afya.

Ngazi ya mshahara: TGS B
SIFA ZA MWOMBAJI
• Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
• Aliyefuzu mafunzo ya cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani za masijala ya kawaida, Afya na Ardhi.

MAJUKUMU

Msaidizi wa kumbukumbu masijala ya kawaida
• Kutafuta kumbukumbu/majalada yanayohitajiwa na wasomaji
• Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika majalada.
• Kuweka majalada katika makundi.
• Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/Nyaraka.
• Kuweka kupanga kumbukumbu sehemu ya kuhifadhia.

Msaidizi wa kumbukumbu masijala ya Ardhi

• Kushughulikia madai/malalamiko ya hati za viwanja na kutunza kumbukumbu zake.
• Kutunza kumbukumbu za cadastral surveys na mahesabu yake.
• Kuandaa nakala za cadastral site plans.
• Kutunza miongozo ya ramani na viwanja.

Msaidizi wa kumbukumbu masijala ya Afya

• Kutafuta kumbukumbu/majalada yanayohitajiwa na wasomaji.
• Kushughulikia mapokezi ya wagonjwa wa ndani na nje.
• Kukusanya kukagua na kuhifadhi taarifa mbalimbali za wodi za wafonjwa

SIFA NYINGINE ZA JUMLA

i. Mwombaji awe raia wa Tanzania.
ii. Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 40.
iii. Maimbi yake yaambatishwe picha (passport size) na vielelezo vya sifa zake.
iv. Cheti cha kuzaliwa kinambatishwe pia.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi
Hlmashauri ya Mji
S.L.P 526
BARIADI

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12.10.2015 saa tisa na nusu alasiri.
Source: Mwananchi 21st September, 2015
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom