Kazaa na mwanaume mwingine hataki nimuoe

Kazaa na mwanaume mwingine hataki nimuoe

waraha

Member
Joined
Oct 24, 2014
Posts
22
Reaction score
5
Habari wandugu.

Miaka miwili nyuma nlikua na mpenzi wangu ambaye tulishafikia stage ya uchumba alifahamika kwetu kama mimi nlivofahamika kwao.

Siku moja tulifarakana kidogo kam ilivo kawaid ya mapenz.na tulikaa wiki nzima bila kuwasiliana mpaka alipokuja kunitumia sms ameomba likizo ya mwezi mzima na hivyo atasafiri kwenda kwao.

Alibadili namba ya simu na hata nilivotumia namba za ndugu zake aligoma kuongea na mimi, baada ya muda kupita akaniambia amepata mwanaume mwingine na wamepanga kuzaa nae.

Mwishoni mwa mwaka jana amejifungua mtoto, ila tatizo likaja kwa wazazi wake,wakamkataa yule mwanaume kisa ya dini tofauti sasa ananibembeleza nirudiane nae na nimuoe,kisa wazazi wake walisha nikubali na yeye anataki kuolewa.

Naombeni ushauri nifanyaje.
 
Sikiliza moyo wako na nafsi vinasemaje ufanye hayo
 
Hapo hamna kitu hakuna maamuzi mabaya na ya kujidhulumu kama kuoa au kuwa na mwanamke aliyezaa na mtu mwingine alafu wengi wanakuwa watu wa drama sana.
 
Wataalamu wa mambo huwa wasema kuwa ati masuala ya wanandoa/wachumba/watu ambao ni wapenzi wa muda tayari,
Kuwa mipango ama maamuzi yao hayangiliwi kwa nasaha za mnasihiji wala ushauri wa ashauriye mpaa yamkute masaibu mazito ambayo atashindwa stahamili....
Kimsingi hilo saibu lokusibu weye ni ishara kama si darsa tosha kuwa ulipozania pema si pema tena...
 
Huyo dada alikua na akili ya kuzaa sio kuolewa.
 
Anaogopa kuwa single parent yaani mtu ulikuwa naye, akazaa na mtu mwingine sasa hivi anarudi kwako na unaomba ushauri?At least angekuwa hajazaa ningekushauri ucheki nafsi yako maana nna jamaa zangu kadhaa walipigwa chini na wachumba zao. walipokwama walikoenda wakarudi na jamaa wakaoa.
 
Nadhani wewe mwenye utakua na mamuzi zaidi sababau wewe ndio unamjua huyu mdada raha zake na machungu yake
nadhani jibu umeshalijua ndani ya moyo wako kabla hujaanza kuandika huu uzi ila ulitaka mawazo ya ziada...
 
Sasa unataka ushauri gani?

Hapo kuna route mbili tu, kukubali au kukataa. Na yote hayo wewe unapaswa kujua lipi la kufanya
 
Achana na huyo binti, heri ungekuwa hujawahi kuwa naye kabisa, sasa umekutana naye huku akiwa na mtoto hapo ningekushauri umuoe, lakini kwa situation yako huyo hakufai mara mia.
 
Inavyo onekana wewe bado unampenda huy dada ila ushauri wangu;
Angalia sababu iliyo fanya utengane naye mara ya kwanza na kumfanya aende kuzaa na mtu mwingine Je ina mashiko?
Tahadhari yangu ni asije kuwa ni mtu wa kukimbia kimbia au kununa nuna ovyo ukaishia kuwa na presha bure.
Kama sababu ilikuwa na mashiko; Angalia uhusiano wake na huyo aliye zaa naye kama huyo kijana anampenda au ilikuwa ni pas time tu mtoto akapatikana?

Ukijiridhisha na hayo maswali, fuata moyo wako ila usisahau kwenda kupima Afya zenu kwanza...
 
Mapenzi mi huwaga simshauri mtu mana siwezi jua yeye anampenda vipi, maamuzi yako bro.
 
MO11

Akili za usiku hizo.
 
Last edited by a moderator:
Ndio ujue hitaj lake ni ndoa na si vingnevyo utampa ndoa af atarud kwa baba watoto wake kuliendleza so amua kama unataka kumuuolea mtu au otherwise.
 
Achana nae huyo buana we sio microwave mpasha viporo acha uboya mtimue
 
Sasa hapo unaomba ushauri wa nn wakat kila kitu kipo wazi?assume wazazi wake wangemkubali huyo kijana wa dini nyingine,unahisi angekuja kwako?Huyo kaja kwako coz 1. Anahitaj kuolewa na 2.

Wazaz wamemkataa mwanaume wa kwanza so akishaolewa then ndio mambo yanarud na yule wa kwanza mana ashatimiza anachokitaka.Make decision ambayo unajua utaishi nayo maisha yako yote na usijelaum watu baadae na maneno ya Ningejua
 
Ndugu yangu usiumize kichwa bule huyo mwanamke hana mapenzi na wewe kabisa anataka aolewe na wewe il à pâte sehemu ya kujishikiza baada ya kuona chaguo lake wazazi wake hawajalikubali na kama utamuoa huyo dada basi fahamu ndoa yako itakuwa full matatizo tena itakuwa sio ya kudumu ndoa inataka UPENDO wa kweli toka rohoni sio ubabaishaji
 
Piga chini kijana bado mbichi limama linanuka mtindi Wa mtoto Wa mumume mwenzio unaoa haihitaji diploma kuchanganua
 
Back
Top Bottom