Kaya 2,000 'zahitimu' za kupokea fedha za TASAF

Kaya 2,000 'zahitimu' za kupokea fedha za TASAF

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Halmashauri ya Chemba imepokea Shilingi bilioni 2.7 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa mwaka 2024 na 2025 ili kusaidia ruzuku kwa kaya masikini wilayani humo.

Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Chemba, Simon Butondo, alieleza kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 2.1 zilitengwa kwa ajili ya ruzuku kwa walengwa, huku Shilingi 164.7 milioni zikielekezwa katika usimamizi na uendeshaji wa mpango huo katika ngazi ya halmashauri.

Kwa mujibu wa Butondo, kaya 6,990 zenye jumla ya walengwa 23,000 zimenufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini katika wilaya hiyo. Alisema kuwa kupitia msaada huo, baadhi ya walengwa wamefanikiwa kuinuka kiuchumi na sasa wamehitimu kupokea ruzuku hizo.

"Hadi sasa, zaidi ya kaya 2,000 zimeweza kujikwamua na kuhitimu kupokea ruzuku za TASAF, na kaya zilizobaki zinazopokea msaada huo ni 4,116," alisema Butondo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba, Hassan Mnyika, aliishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuleta fedha hizo ambazo zimechangia kuboresha maisha ya walengwa na kuwaondoa kwenye hali ya umasikini.
1743680558705.png

Source: Habari Leo
 
Back
Top Bottom