Kawagombanisha ili aolewe yeye na ameolewa

Kawagombanisha ili aolewe yeye na ameolewa

Mwinjilist mtume nabii

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2015
Posts
2,437
Reaction score
1,100
Jamani hii ni hatari, ebu fuatilieni mjifunze, mke na mume wanaishi pamoja na wanapendana tu, sasa huyu mke ana rafiki yake wa karibu sana, ambaye hajaolewa na anamwonea wivu sana mwenzake. Kwani na yeye alikuwa anapenda sana kuolewa.

Sasa kilichotokea huyu rafiki akamfuata mume wa yule dada na kumwambia uongo eti mkeo amekwenda kwa mganga na amepewa dawa kaambiwa akupake mgongoni leo usiku ukiwa umelala ili usiwe na sauti.

Na yule mume kwa kuwa anajua ni rafiki wa karibu sana wa mkewe akaamini, akalichukulia serious na akasema nitakuwa makini nione. Baada ya hapo yule rafiki akamfuata rafiki yake mke wa jamaa akamwambia rafiki yangu hii ni siri ya ndani mimi nakupa tu kwasababu ni rafiki wa damu, unajua mumeo ana mkia mgongoni?

Amewekewa na mganga ili ww usimfuatilie katika mambo yake, basi na huyu mke akaamini akasema leo usiku nitamkagua. Kwahiyo sasa wote wakawa makini bila kujijua. Jamaa akawa anakoroma,mwanamke akaanza kumpapasa na ghafla mume akaamka na ndio ikawa mwisho wa ndoa, mume kwa fadhila kamchukua rafikiye.
 
mkuu umenikumbusha mbali sana..umenirudisha miaka kadhaa nyuma..hadithi kama hizi nilikuwaga nasimuliwa na bibi kipindi hicho utotoni...kama una watt nahisi watakuwa wanaenjoy sana uwepo wako
 
mkuu umenikumbusha mbali sana..umenirudisha miaka kadhaa nyuma..hadithi kama hizi nilikuwaga nasimuliwa na bibi kipindi hicho utotoni...kama una watt nahisi watakuwa wanaenjoy sana uwepo wako

hapana bado cna watoto, lkn iyo ni live
 
Hii hadithi mtumishi inajengaje ufalme wa Yesu?
 
RTD miaka hiyo ya giza mama na mwana baada ya hadithi kama hii swali linafuata,"hadithi hii inatufundisha nini?"
 
Hii hadithi mtumishi inajengaje ufalme wa Yesu?

neno linasema mungu hafanyi jambo lolote paspo kuwafunulia watumishi wake. kwa iyo kama mahusiano yako na mungu yapo vzr, hauhitaj kuamini maneno ya mpagani,na pia mungu hutupa kuzijua hila za adui, lkn huyu jamaa amekosea
 
Back
Top Bottom