Kauli za rais wa Tanzania na mtetezi wa wanyonge Dkt. Magufuli leo mkoa wa Manyara

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Katika hii vita ya uchumi, watatugombanisha, na sisi tukikubali kugombana wataendelea kutuibia. Ni vyema tushikamane sana.

Ukiona kazi huwezi, acha uondoke, kuna watanzania wengi sana wanaotamani kufanya hiyo kazi.

Mtu analalamika maisha magumu, lakini mshahara wake haujapunguzwa ni ule ule. Basi hapo unajua kulikuwa na namna ya ziada.

Wengine wakisimama na kusema pesa zimepotea, sitawashangaa kwa sababu walizoea kuiba pesa zisizo zao, na kweli zimepotea.

Najua hamna hata ambulance, hiyo nitawaletea mimi. Nitakwenda kuwa katakata huko, nitapata ambulance itakuja.

Hii barabara watapita watu wote wa vyama vyote. Hata majizi wa Tanzanite, watapita barabara hii.

Najua kuna wawekezaji wameanza kuondoka, na wengine wameshaondoka kwa sababu walichokuwa wanakifanya hakikuwa sahihi.

Tanzania tunataka wawekezaji, lakini kama anadhani anakuja kutuibia, kwa sasa hawezi. Tumeweka mikakati kudhibiti mali zetu

Soko la madini ya Tanzanite liwe hapa hapa Simanjiro lisiwe Arusha. Wanunuaji waje hapa, wakae hapa, wale hapa hapa.

Kwa sababu Mungu hakukosea kuweka Tanzanite Tanzania, basi ni lazima tuitumie kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wetu.

Hapa patafungwa kamera za ulinzi, kutakuwa na mlango mmoja tu, na hata mtu akimeza Tanzanite itaonekana. Tumechoka kuibiwa.

naagiza JWTZ kupitia Suma JKT kujenga ukuta eneo la Block A-D ambalo ndilo lenye madini mengi ya Tanzanite, na kufunga kamera
 
Back
Top Bottom