Kauli ya Zitto dhidi ya Mbowe kuhusishwa na madawa ya kulevya

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Kauli ya zitto dhidi ya Mhe.Mbowe kuhusishwa na madawa ya kulevya.

Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amemkingia kifua Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kusema kuwa anaamini Mbunge huyo wa Hai hajawahi kujihusisha na dawa za kuleva kwa namna yoyote

Zitto ambaye ameambatana na Mbowe katika mkutano wake na wanahabari leo mjini Dodoma, amesema kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumtaja Mbowe katika sakata la dawa za kulevya ni sawa na kutangaza vita na chuki dhidi ya chama hicho.

Amesema kuichafua CHADEMA ni sawa na kuuchafua upinzani hivyo na yeye hawezi kukaa kimya kuona upinzani ukishambuliwa, na ndiyo sababu ya kuongeza nguvu kwa kuungana naye.

tmp_1622-FB_IMG_1486731453664217428012.jpg

Nini maoni yako??
 
Namuunga mkono.,alichofanya makonda baada yakuona kila anaehusika na dawa zakulevya kajikinga na ccm ikambidi aijumlishe chadema kilazima ili aweke uwiano kwakukwepa aibu.kuna taarifa ambazo hazijadhibitishwa zinasema makonda alipewa maelekezo yakulijumlisha Jina la mbowe kwenye list yake na bwana yule anaofahamika kwa chuki.
 
Hahaha,
Bwana yule
 
Hili liko dhahiri. Ni pamoja na jina la Gwajima, lakini Gwajima siyo kutoka kwa huyo, bali ni kule anakofutaga viatu.
 
Suala la madawa ya kulevya ni serious, sidhani kama ni busara kufanya mapambano kwa mihemuko. Unapomtuhumu mtu kwenye suala zito kama hili, wahitaji eveidence beyond doubt, maana lina implication nyingi Zaidi tufikirivyo. Let us be serious and act matured.
 
Nahis mbowe amekamatwa kwasabab ya club ya billz mana naskia pale biashara ya unga inafanyika sana.labda ameitwa ili aelezwe kuwa inabd adhibit hiyo biashara pale billcanas
Sio kweli,
Manake Billz haipo tena,
 
tungemuamini zaidi zzk, kama angetoa orodha ya watu anaowafahamu kujihusisha kwa namna yoyote na madawa
kwa hiyo, yeyote .wenye kuse.a lolote kuhusu hao watuhumiwa, kama hana majina anachokisema chochote hakiaminiki,

we hujatulia!
 
Back
Top Bottom