Kauli ya Wilsoni Kabwe baada ya kutumbuliwa jipu darajani na Rais Magufuli

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa tuhuma zilizomfanya Rais John Magufuli kumsimamisha kazi jana utabainisha ukweli huku akihoji; “ikiwa itabainika kwamba nilionewa nitalipwa fidia?”

Alisema hayo mara baada ya Dk Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni ambalo sasa litaitwa Daraja la Nyerere baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza tuhuma dhidi ya mkurugenzi.

Alipoulizwa jana, Kabwe alisema hakuwa na taarifa za kusimamishwa kwake na mazungumzo yake na mwandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwandishi: Habari mkurugenzi?

Kabwe: Salama.

Mwandishi: Tumepata taarifa za kusimamishwa kwako kazi na Rais kutokana na tuhuma zilizotolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda tunaomba maoni yako.

Kabwe: Sijasikia ndiyo kwanza unaniambia wewe, kasema lini Rais?

Mwandishi:Leo wakati akizindua Daraja la Kigamboni.

Kabwe: Alitamka palepale au?

Mwandishi: Ndiyo.

Kabwe: Sasa kama ameshasema yeye ndiyo mkubwa mimi sina la kusema tena.

Mwandishi: Nataka kujua unazungumziaje uamuzi huo?

Kabwe: Nimekwambia sina la kukwambia kwa sasa lakini nimesema tu sina shida na hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu. Lakini kama ukijulikana na ikibainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote nitalipwa?

Chanzo: Mpekuzi
 
Atalipwa fidia hehehe!!
pole yake
Japo naona kawa kipenzi cha Ukawa
Hawa sijui wapoje!!
Mtu akitumbuliwa kaonewa akiachwa CCM ni ileile
Tz kuna vizazi vyahovyo kweli
UKAWA watu wa ajabu sana sijui nani kawaroga watu hawa.
 
Kabwe kasimamishwa. Anasema mwisho wa sakata atalipwa fidia. Lakini anasahau kwamba kwa mujibu wa madaraka ya Rais anaweza kumfuta kazi mtumishi mteule wake kwa manufaa ya umma. Mtumishi akishatimuliwa na Rais kwa manufaa ya umma hawezi kufungua shauri Mahakamani. Na hadithi ya fidia inaishia hapo. Katika awamu iliyopita hizi Notice za kumsimamisha/kumfuta kazi mtumishi kwa manufaa ya umma zilikuwa hazitokitoki na hata kama zilitoka basi zilikuwa chache sana. Je, kwa awamu hii Kabwe anafikiri itakuwa ngumu kwa Rais kutoa Notice ya kumfuta kazi mtumishi kwa manufaa ya umma? Anyway, nimtakie kila la heri.
 
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa tuhuma zilizomfanya Rais John Magufuli kumsimamisha kazi jana utabainisha ukweli huku akihoji; “ikiwa itabainika kwamba nilionewa nitalipwa fidia?”

Alisema hayo mara baada ya Dk Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni ambalo sasa litaitwa Daraja la Nyerere baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza tuhuma dhidi ya mkurugenzi.

Alipoulizwa jana, Kabwe alisema hakuwa na taarifa za kusimamishwa kwake na mazungumzo yake na mwandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwandishi: Habari mkurugenzi?

Kabwe: Salama.

Mwandishi: Tumepata taarifa za kusimamishwa kwako kazi na Rais kutokana na tuhuma zilizotolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda tunaomba maoni yako.

Kabwe: Sijasikia ndiyo kwanza unaniambia wewe, kasema lini Rais?

Mwandishi:Leo wakati akizindua Daraja la Kigamboni.

Kabwe: Alitamka palepale au?

Mwandishi: Ndiyo.

Kabwe: Sasa kama ameshasema yeye ndiyo mkubwa mimi sina la kusema tena.

Mwandishi: Nataka kujua unazungumziaje uamuzi huo?

Kabwe: Nimekwambia sina la kukwambia kwa sasa lakini nimesema tu sina shida na hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu. Lakini kama ukijulikana na ikibainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote nitalipwa?

Chanzo: Mpekuzi

Hakuna fidia utalipwa kwa maana Raisi wa JMTZ ndiye aliyekuondoa yaani amekataa kufanya kazi na wewe, hivyo hapo hakuna kulipwa kitu!
 
Kabwe kasimamishwa. Anasema mwisho wa sakata atalipwa fidia. Lakini anasahau kwamba kwa mujibu wa madaraka ya Rais anaweza kumfuta kazi mtumishi mteule wake kwa manufaa ya umma. Mtumishi akishatimuliwa na Rais kwa manufaa ya umma hawezi kufungua shauri Mahakamani. Na hadithi ya fidia inaishia hapo. Katika awamu iliyopita hizi Notice za kumsimamisha/kumfuta kazi mtumishi kwa manufaa ya umma zilikuwa hazitokitoki na hata kama zilitoka basi zilikuwa chache sana. Je, kwa awamu hii Kabwe anafikiri itakuwa ngumu kwa Rais kutoa Notice ya kumfuta kazi mtumishi kwa manufaa ya umma? Anyway, nimtakie kila la heri.
Mkuu hujaacha ulevi dizaini ya sokomoko
 
Kabwe ni mtu makini sana kuliko mnavyofikiria na sio rahisi kunaswa mtakuja kuniambia humuhumu! Namjua sana nimefanya nae kazi sana!
Ni mtu "makini" huyu huyu aliyetuletea kizaazaa Mwanza kwa kumkata jina Ezekia Wenje kwamba sio raia wa Tanzania ili Lawrence Masha apite bila kupingwa kwenye Ubunge wa Nyamagana mwaka ule. Wenje alipokata rufaa ngazi ya Tume ya Uchaguzi Taifa wakapiga chini maamuzi ya Wilson Kabwe na pia wakamshangaa kwanini aliamua kumbatiza Wenje uKenya wakati kila kitu kilikuwa clear. As a result Wenje akarudishwa kwenye king'ang'anyiro na kushinda Ubunge. Na usikute hata ile michezo ya kufungua Kesi hewa ili kuchelewesha uchaguzi wa Meya DSM alikuwa nyuma yake. Huyu mtu umakini wake sijui reference yake mnaitoa wapi? Yaani tumekuwa wasahaulifu kirahisi hivi? Au tumepandia njiani!
 
Back
Top Bottom