The seer
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 407
- 690
Kwa mda mrefu Tanzania kauli ya kwamba Kazi ya ualimu ni wito imekuwa ikitumika na kwa mazingira ya sasa inachangia kuua elimu yetu.Wito ni kufanya kitu kwa kujitolea bila malipo yeyote kwa unayemfanyia labda shukrani.ina maana kusema ualimu ni wito ni kwamba malipo anayepewa MWALIMU ni kama shukrani tu.kitendo hicho cha kuchukulia ualimu ni wito kinachangia kufanya Kazi ya ualimu izaraulike na jamii.na kutochukuliwa kimakini.na ndio mwanzo wa elimu ya Tanzania kuwa chini.dunia imebadilika elimu ndio ina control dunia.mataifa yanayotawala dunia.ndio yaliyowekeza kwenye Elimu kisawasawa.Hivyo ni wakati sasa wa Tanzania kubadilika na kuwekeza kwenye Elimu bora.hatuwezi piga hatua ya kimaendeleo bila kuwa na Elimu ya uhakika.kauli ya kwamba ualimu ni wito imepitwa na wakati.walimu ni professional kama Kazi zingine hivyo lazima walimu wapewe kipaumbele kama fani nyingine kwa maslahi ya elimu na taifa letu.walimu wanahitaji mazingira Mazuri ya Kazi na maslahi Mazuri. N.B KAMA TAIFA NA JAMII WATAENDELEA KUDHALAU KAZI NA FANI YA UALIMU BASI NCHI HAITAENDELEA.Kwa sababu wataamu wote nchini ni zao LA MWALIMU.karibuni kwa michango zaidi wadau.