Kauli ya ndoa ni uvumilivu imepitwa na wakati

IKIRIRI

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
2,734
3,017
Zamani heshima ya mwanamke/mwanaume ilikuwa kuolewa au kuolewa hata kama una elimu kiasi gani.

Lakini dunia ya leo mambo yamebadilika sana. Hili linawagusa sana wadada nawaambia mjue.

Kwanza, wanaume wengi sio waoaji ni wachezeaji. Na wanaume wanaofanikiwa kuoa wanatumia muda mwingi kuwatesa wanawake. Ndio maana kesi za kuua, kupiga na kunyanyasa wanawake ziko nyingi sana.

Wewe kama mwanamke usisikie vibaya eti kisa hauna ndoa. Na wewe ambaye umeolewa kauli za ndoa kuvumilia zimepitwa na wakati kabisa.

Manyanyaso hayavumiliki hata kidogo.
Tuwalee watoto na tuwaambie ukweli huyu mwanaume mmekutana ukubwani kwanini akutese?

Kwa watoto wa kike na kiume ndoa sio mateso, unaweza kuishi bila ndoa.
 
Uvumilivu muhimu wala si uongo.

Ila haaanishi kwenye mateso makali au vipigo na matusi ya kuvunjiana heshima. Binadam tunatofautiana sana kuishi pamoja kama mke na mme si lelemama.
 
Heshima yangu mimi ninayo. Ndoa ni system iliowekwa na wanaume kuwatumikisha na kuwakandamiza wanawake. Basi ndo waka attach ndoa na thamani ya mwanamke ili wanawake wasioolewa wajione/ waonekane hawana thamani. I won't fall for that nonsense.
 
Wanawake wenyewe siku hizi ni wajeuri sana coz wengi wao wana vielimu elimu sawa na wanaume, wakiona mateso mbona wanaachia ngazi mapema na ndio maana kuna idadi kubwa ya single maza mtaani.
 
Heshima yangu mimi ninayo. Ndoa ni system iliowekwa na wanaume kuwatumikisha na kuwakandamiza wanawake. Basi ndo waka attach ndoa na thamani ya mwanamke ili wanawake wasioolewa wajione/ waonekane hawana thamani. I won't fall for that nonsense.
Itabidi tuoane mkuu, you will fall unconsciously
 
Nyie wanawake mnaodanganya kuhusu ndoa mnatakiwa mjue hata wazazi wenu wanavumiliana; sio vijielimu vyenu vya kukaririshwa mnawadharau waume zenu. Kuna mtu amesema ndoa no mfumo uliotengenezwa na wanaume kuwakandamiza wanawake. Kwani kama hamna ndoa hukandamizwi?
 
Heshima yangu mimi ninayo. Ndoa ni system iliowekwa na wanaume kuwatumikisha na kuwakandamiza wanawake. Basi ndo waka attach ndoa na thamani ya mwanamke ili wanawake wasioolewa wajione/ waonekane hawana thamani. I won't fall for that nonsense.

Kinywaji gani unatumia?
 
Tusijaribu kudanganyana hapa, nakubaliana na mtoa mada na ndio maana kwenye mahusiano nikizingua najitoa mapema tu kuepusha lawama zisizo za msingi
 
Heshima yangu mimi ninayo. Ndoa ni system iliowekwa na wanaume kuwatumikisha na kuwakandamiza wanawake. Basi ndo waka attach ndoa na thamani ya mwanamke ili wanawake wasioolewa wajione/ waonekane hawana thamani. I won't fall for that nonsense.
Ha ha haa
Tangu zamani walikuwepo wenye ndoa na wasio.
Hilo ni fungu lako.
Hatuwezi kuwa na viongozi wasiooa kila siku wanabadili wanaume au wanawake.
Marekani na maendeleo yao mpaka leo bado wanaona umuhimu wa viongozi wao kuoa.
Maana kwa kiongozi nje ya ndoa maisha yake yako mikononi mwa mahawara zake na anaweza asijue tatizo kalipata kwa nani
 
Back
Top Bottom