Kauli ya Nape: Tutashinda Arumeru zaidi ya Igunga

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
[h=2]Nape;"tutashinda arumeru zaidi ya igunga"[/h]
Nimemsikia katibu wa uenezi wa CCM akijitamba kwenye chombo kimoja cha habari kwamba chama chake wana uhakika wa kushida zaidi ya walivyoshinda Igunga. Amesema hii ni kutokana na utafiti walioufanya na kugundua kwamba bado sisiem inakubalika sana Arumeru.Ila kilichonishangaza hajasema huo utafiti ulifanyika kwa njia gani ukizingatia hakuna kura za maoni zilizowahusisha wananchi ambozo zimeshafanyika au anataka kutuambia kwamba ana scanner inayoscan ubongo wa wananchi.


Hizi ndizo dhana potofu za ccm zilizowafanya washindwe vibaya sana. Kufikiri watu wote ni wajinga na wanaweza kudanganyika kwa mahindi na maharage, kofia, Tshirt na khanga kumeonekana kufikia mwisho wake. Kama bado hamjaamka mpaka sasa na kuelewa hilo, jueni kuwa siku za ccm zimefika ukingoni!

Hongera sana wana Arumeru! Mlinong'ona na dunia imewasikia! Hamkuhitaji matusi wala kelele, naam tumewasikia!
 
1.jpg
 
Back
Top Bottom