Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,159
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, katika ufunguzi wa maktaba mpya hapo Chuo kikuu cha Dar-es-salaam, Rais Magufuli akitamka waziwazi huku akimsifia Lowassa na kudai kuwa huyo ni kiongozi wa mfano na kumpa ujumbe kuwa akawaeleze viongozi wenzake wajifunze ku-behave ama sivyo wataishia gerezani!
Kwanza kauli hiyo siyo sahihi kabisa, kwa kuwa ni chombo cha mahakama pekee kinachoweza kuthibitisha tuhuma ya mtu
Kwa kutoa kauli hiyo tayari yeye keshawahukumu viongozi wa Chadema kuwa wana hatia!
Tunajua kuwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani na Mbunge wa kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe na mbunge mwenzake wa Jimbo la Tarime mjini, Esther Matiko, wanaendelea kusota gerezani segerea kwa kilichodaiwa na mahakama ya Kisutu kuwa wameidharau mahakama hiyo
Hivi kwa kutamka maneno hayo Rais wa nchi haoni kuwa anaingilia mhimili wa mahakama katika kufanya maamuzi yake na kuonyesha kuwa hata kufutwa kwa dhamana ya kina Mbowe imetokana na influence yake??
Hivi Rais haijui kanuni ya kimahakama ambayo inazuia kutoa kauli kwa kesi inayoendelea mahakamani??
Kama anaijua iweje yeye anatoa kauli ya vitisho kuwa viongozi wenzake na Lowassa wataishia gerezani, huku akijua kuwa kuna kesi inayoendelea Kisutu na kuna viongozi wa Chadema ambao dhamana zao zimefutwa kwa njia ya utata??
Hivi viongozi hao wa Chadema si walishaweka pingamizi la kumkataa Hakimu anayeendesha kesi yao??
Kwa kawaida unapokataliwa na washitakiwa kuendelea na kesi yao inabidi wewe Hakimu ukubaliane na uamuzi huo wa washitakiwa na ukae pembeni ili Hakimu mwingine ateuliwe kuendelea na kesi hiyo
Hivi Hakimu Mashauri anaweza kutupa sababu za kukataa kujitoa kuendelea na kesi hiyo ambayo washitakiwa wenyewe wamesema hawana Imani naye kutokana na mwenendo anaouunyesha wa kupendelea upande mmoja??
Mwenendo wa kesi ya akina Mbowe na kauli iliyotolewa na Rais Magufuli kuwa viongozi wa Chadema wasio-behave wataishia jela ni kauli mbaya kabisa kuwahi kutolewa na Rais was nchi hii
Hivi viongozi wengine watakaofikishwa mbele ya mahakama watakuwa na Imani gani na mahakama baada ya kauli hii ya Rais??
Mungu ibariki Tanzania