Kauli ya Kikwete ndiyo ilichochea vurugu Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Kikwete ndiyo ilichochea vurugu Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Jun 7, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kitendo cha raisi JK kuagiza kuwa suala la ama muungano uwepo au usiwepo lisijadiliwe kwenye mchakato wa katiba mpya ndilo lililoamsha hamasa za majadiliano na malumbano juu ya muungano.

  Kikwete alijua kwa ufasaha kuwa kisaikolojia, ukimkabidhi binadamu vitu hata mia ukamwambia kuwa anaruhusiwa kuvichambua vyote, ila kimoja asikiguse, akili ya binadamu huyo inapuuza vile 99 na kudeal na hicho kimoja alichokatazwa huku akiwaza kuwa kuna nini ndani, na kwa nini amekatazwa kugusa hicho kimoja? Ukimuweka mtu kwenye jumba lenye vyumba 20, ukamwambia anaweza kuingia vyote isipokuwa kimoja, then mtu huyo siku hiyo hiyo ataanza juhudi za kujua kuna nini kwenye chumba alichakatazwa kuingia.

  Muda mfupi tu baada ya Kiwete kupiga mkwara kuwa suala la muungano lisijadiliwe, ndipo yalipoibuka malumbano mengi ya watu wakuhoji uhalali wa muungano. Itakumbukwa kuwa ni wakati huo ndipo Sitta alipopeleka mswada wa sheria ya marekebisho ya katiba Zanzibar, na mmoja wa Wazanzibar, ambaye kwa sasa ni moja wapo ya viongozi wa UAMSHO aliuchana mswada ule mbele ya Sitta kwa kudai kuwa kama suala la muungano halijadiliwi, then haukuwa na maana.

  Hadi wakati huu suala la muungano ndilo linalojadiliwa kuliko masuala yote yanayohusu katiba. Fuatilia mijadala ya kwenye TV na vyombo vingine vya habari, utagundua kwa sasa mjadala ni muungano tu!

  Siwezi kusema kuwa Kikwete hakujua hilo maana naamini anao washauri makini, na alifahamu fika kuwa namna peke yake ya kuibua majadiliano makali juu ya uhalali wa muungano, ni kwa 'kukataza usijadiliwe.'

  Kwa mtu yeyote makini, na kwa serikali yeyote makini, vurugu za UAMSHO hazikuja ghafla. Kila mtu aliziona zinakuja na serikali iliziona mapema zaidi pale nakala ya mswada wa sheria ilipochanwa mbele ya kiongozi wa serikali.

  Hata hivyo kundi hili haramu liliendelea kulindwa na kusaidiwa na serikali hadi lilipofanikiwa kukoleza sumu ya chuki miongoni mwa wazanzibar, ndipo serikali inazuga kulidhibiti.

  Kikwete has to be smarter next time, when he wants to play a game...
   
 2. m

  mjt Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unapokuwa muongo kuwa pia mwepesi wa kukumbuka lakini hili rais wetu hakuliona kama ni tatizo sasahivi ndo anaanza kusema watu watoe maoni yao pasipo kukumbuka kwamba alizuia jambo hili. yaliyotokea Zanzibar aliyataka rais mwenyewe
   
 3. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kiongozi huyu ni katili,mwizi, mwongo na........... Anajua anachokifanya! amepanga kutuvuruga ili aendelee kututawala! nchi imemshinda sasa badala kuondoka kwa amani ametuingiza katika udini ili tuanze kuchapana makonde yeye andelee kuiba! ni mrafi, mroho! hana imani tena nimshirikina!
   
 4. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  nyie wazenji mna shida sana kwani Rais ndo aliwatuma mchome makanisa? Huo ni ujuha wenu tu wa kukosa elimu dunia.
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Namuonea huruma sana JK jamani maana atavunja rekodi 3 asipoangalia
  1.Muungano kuvunjika mikononi mwake
  2.CCM kupasuka yeye akiwa Mwenyekiti
  3.Kumkabithi rais toka upinzani..nchi!!!
   
 6. O

  Original JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acheni upumbavu wenu. Kikwete asiwe ni mtu wa kutupiwa kila lawama. Matatizo ya Zanzibar ni ya muda mrefu sana tena kabla hata ya Kikwete kuwa waziri. Mkapa alivyotuma polisi na kuwapiga risasi wazanzibari kikwete alikuwa Ikulu?.Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Wazanzibari wana matatizo yao ya muda mrefu Kikwete asiwe kisingizio. Katika Tanzania ya leo kila tatizo ni kikwete kikwete kikwete. Ifike muda watanzania tutumie akili zetu katika kufikiri na kuchanganua mambo.
   
 7. O

  Original JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe acha kuropoka matusi bila ya kuwa na ushahidi. Huo ni utovu wa nidhamu.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kweli Unauthibitisho au ni habari za jioni hizo? Tuache kulete habari za Uwalakini, sababu siku moja kibao kitageuka na sheria ni Msumeno
   
 9. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hapa sio suala la uthibitisho mkuu... Naamini wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya siasa hapa Tz... Unahitaki uthibitisho gani.. kwamba nakala ya rasimu ya sheria haikuchanwa mbele ya Sitta?, au kwamba Kikwete hakuzuia watu kujadili juu ya uhalali wa muungano?, au kwamba suala la uhalali wa muungano halijazua malumbano? Au uthibitisha gani unataka?
   
 10. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  tatizo watu tunapenda kusikia mambo kinyumenyume mtu hapendi kuambiwa ukweli mtoa mada nakuunga mkono hicho ni chanzo kimojawapo cha machafuko utamzuia vipi mtu kujadili muungano wakati moshi unafuka ndani badala ya kuacha watu waujadili kujua undani wa tatizo ,ile rasmu waliweka hadi faini kwa mtu atakaekiuka sheria hiyo.Unategemea watu watakuchekea?????viongozi inabidi wawe makini sio kila jambo linaendeshwa kisiasa.
   
 11. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kiongozi. Tunaambiwa kuwa baada ya Mungu kuwaumba Adamu na Hawa, aliwaambia wale matunda yote katika bustani isipokuwa tunda moja la uzima. Matokeo yake wakaanza kula tunda hilo!
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nimeshachoka kuzungumzia zanzibar na hata Rais wetu nahisi na yeye kachoka
   
 13. f

  fergusonema Senior Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nina uhakika vita tanzania itachochewa na huu mtandao wa humu jamii forum ,humu ndani kuna chuki,visasi na ghiliba za kipuuzi sana,thatswhy ntaendelea kusema kua hapa sio great thinkers ni great sinkers
   
Loading...