Wanabodi,
Hii ni thread ya swali lililotokana na ile kauli ya Kakobe kumtaka rais "Magufuli Atubu", yaibua mambo!. Kumeibuka watu wanaohoji asili halisi ya rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, baada ya member fulani humu kuibuka na hoja kuwa Magufuli sii Msukuma wa Chato, bali ni Muha wa Kakonko anakotoka Kakobe, sasa ukweli ni upi?. Jee rais wetu Magufuli ni Msukuma wa Chato, Mhaya wa Wazilankande au ni Muha wa Kakonko?. Japo ni bandiko kuhusu ukweli wa asili ya rais Magufuli, pia tutamuangazia kidogo Askofu Kakobe na hoja yake kumtaka rais Magufuli atubu, kama alichofanya ni kitu sahihi au laa!.
Declaration of Interest
Naomba kuanza na declaration of interest kuwa mimi Paskali Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kwanza ya kuu ya tasnia ya habari ni seek the truth, and tell nothing but the truth!. Kwa kabila ni Msukuma, na kwa vile tayari kuna hoja za ukabila na Usukumanaization, naomba kudeclare my interest kuwa mimi sio mkabila, na hili sio bandiko la kuhusu ukabila, bali ni bandiko la kuhoji ukweli wa kabila halisi la kiongozi wetu, kwa nia njema kabisa ya kuwa na info, kwa Imani kuwa hakuna ubaya wowote kwa raia wowote wa Tanzania, kufahamu kabila halisi na asili ya kiongozi wetu ili kwa kwa vile rais wetu amejinasibu kuwa ni wa kabila la Wasukuma, hixi kauli za kusema rais Magufuli sio Msukuma bali ni kabila Fulani, hii ikitokea kuwa ni ni kweli sii Msukuma kama anavyojisibu, then this has nothing do to with ukabila, but has something to do with uadilifu.
Turudi kwenye mada kuu
Jee Rais Magufuli ni Msukuma, Muhaya au Muha wa Kakonko?.
Siku za nyuma kuna member mwingine humu aliwahi kuibuka na kudai kuwa rais Magufuli sii Msikuma bali ni Muhaya, akaibuka hadi na jina lake halisi la Kihaya kuwa anaitwa Katto, tulipomuomba atufafanulie ukweli huu, aliingia mitini, sasa leo huyu Gungele naye anaibuka na yake kuwa rais Magufuli ni Muha wa Kakonko anakotoka Kakobe!, nimemuomba athibitishe, wakati tukisubiri uthibitisho huu, ndipo ninauliza, kuna ubaya wowote, Watanzania tukafahamisha kwa ukweli asili usio na chenga zozote jee rais wetu Dr. John Pombe Magufuli asili yake kabisa ni Kabila gani?.
Ili kupata majibu yakweli ya ya ukweli huu, tunaomba members wowote wa jf, wenye data za ukweli na uhakika kuhusu rais wetu watuletee kwa kuyajibu haya maswali simple
- Jee alizaliwa lini na wapi?.
- Wazazi wake halisi ni nani?.
- Asili ya wazazi hao ni wapi?.
- Ni kweli aliwahi kuitwa Katto?.
- Ilikuwaje akaibukia Chato?.
- etc, etc
NB. Hii tabia ya baadhi ya viongozi kubadili makabila na kutumia makabila mengine, haikuanza leo, ilianza tangu Enzi za Baba wa Taifa, watu walisema humu, hata Mkapa naye akasemwa ni wa kule..., Edward Lowassa inafahamika kwa wengi kuwa ni Mmeru, ila wazazi wake ndio walihamia Monduli, akazaliwa Monduli, akakulia Monduli, akalelewa Kimasai na kukua na morani wa kule, kwa kupitia hatua zote ikiwemo initiations, hivyo sasa yeye kweli ni Mmasai.
Hitimisho.
Rais Magufuli ni rais wetu, tumemchagua kwa kura zetu, yeye sio malaika bali ni binadamu tuu kama sisi, na hivyo kuweza kufanya makosa na hata dhambi, ila hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kumhukumu binadamu mwingiwe kuwa ni mdhambi, ila sisi kama raia wema wa taifa letu, rais wetu anapofanya makosa ya wazi, tuko huru kumkosoa kwa heshima na staha, na kumueleza makosa yake au mapungufu yake ili ajirekebishe lakini sio kumhukumu kuwa ni mdhambi, na katika kuijua asili yake, kuna baadhi ya mambo ni mambo yake ya binafsi, na hatupaswi kuyaulizia ili tusiingilie his right to privacy, lakini kuijua asili yake, dini yake, kabila lake na jinsi anavyoendesha familia yake, jambo ni mambo binafsi, lakini sisi as taxpayers, we have the right to know details, his public as well as his private conduct haswa katika determination ya truthfulness ambayo ni ethical issue ni sifa kuu muhimu kabisa kuliko sifa zote za kiongozi wa nchi.
Jumatano Njema ya Kufungia Mwaka.
Paskali.
Rejea
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."
Tuhuma za udini, ukanda na ukabila katika teuzi, kama wote wana sifa, kuna tatizo gani?.
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi!
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na Zile Boeing ni TT, Then Hatufai!.
https://www.jamiiforums.com/threads...edeye-ni-bomu.570208/page-8n-hatufai.1246099/
Update 1
Haya ni baadhi ya majibu ambayo ambayo ni very objective na yana coherence, na kwakutumia uzoefu wangu wangu wa miaka 27 ya uandishi wa habari, naamini haya yasemwayo ni kweli kwa msingi tuu wa hearsay na third party contributions, confirmation itapatikana kutoka kwa ndugu wa karibu, wana ukoo, next of kin or from the horses mouth.