Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi,

Utangulizi
Tuanze na background issue ni Askofu wa Kanisa la FGBF, Askofu Mkuu, Zakaria Kakobe, amezumza kwa ukali kabisa kumwambia rais Magufuli ni mdhambi na kumtaka atubu, na asipo tubu kuna kitu Mungu atafanya, ila hakusema ni nini

Hii sio thread ya kuzungumzia dhambi za rais Magufuli, bali ni thread ya swali lililotokana na ile kauli ya Kakobe kumtaka rais "Magufuli Atubu", ambayo sasa imekuwa ni kama jambo limezua jambo kwa kauli hiyo kuwaibua watu wanaohoji asili halisi ya rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, baada ya member fulani humu kuibuka na hoja kuwa rais Magufuli na Askofu Kakobe ni watu wamoja, wanajuana vizuri, wote ni watu wa kutoka kijiji kimoja, ni watu wa kabila moja la Waha wa Kakonko. Jee ukweli ni upi?. Jee rais wetu Magufuli ni Msukuma wa Chato, Mhaya wa Wazilankande au ni Muha wa Kakonko?.

Declaration Kuhusu Ukabila
Japo ni bandiko kuhusu ukweli wa asili ya mtu, kuzungumzia asili ya mtu sio ukabila bali hii inaitwa tracing the originality, uki trace the orgin ya asili za makabila mengi ya Tanzania, utashangaa kukuta kumbe makabila ya asili ya Tanzania ni machache, wakiwemo Wasukuma na Wagogo, na makabila ya mikoa ya kati, lakini mengi ya makabila ya Tanzania ni wahamiaji, hivyo watu wote waliokuwepo kwenye ardhi ya Tanganyika kuanzia ile saa 6:00 wa tarehe 9 Desemba, mwaka 1961, ni Watanzania, regardless walizaliwa wapi na asili zao ni wapi, wote tuu Watanzania na tuu wamoja.

Katika bandiko hili pia tutamuangazia kidogo Askofu Kakobe na hoja yake kumtaka rais Magufuli atubu, kama alichofanya ni kitu sahihi au laa!.

Declaration of Interest of Truthfullness
Naomba kuanza na declaration of interest kuwa mimi Paskali Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu na ya kwanza ya tasnia yetu ya habari ni "seek the truth, and tell nothing but the truth!" ikimaanisha ukweli ndio nguzo kuu ya tasnia ya habari, kazi ya mwandishi wa habari wa ukweli ni kuutafuta tuu ukweli na kuandika ukweli huo au kuusema ukweli bali katika kuusema ukweli, mwandishi sio anatakiwa kuusema tuu ukweli no matter what, bali kuusema ukweli utakaoisaidia jamii na kuleta manufaa, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Declaration of Interest ya Usukuma
Kwa vile mimi kwa kabila ni Msukuma, na kwa vile tayari kuna hoja za ukabila na Usukumanaization kwenye awamu hii ya Magufuli, naomba kudeclare my interest kuwa, siandiki bandiko hili kwa ajili ya Usukuma wangu, wala bandiko hili sio la ukabila, na Wasukuma sio wakabila, bali ni bandiko la kuhoji ukweli wa kabila halisi la kiongozi wetu, kwa nia njema kabisa ya kuwa na info, to be informed, kwa imani kuwa hakuna ubaya wowote kwa raia wowote wa Tanzania, kufahamu ukweli wa kabila halisi la kweli na asili halisi ya kweli ya kiongozi wetu.
Turudi kwenye mada kuu
Jee Rais Magufuli ni Msukuma, Muhaya au Muha wa Kakonko?.
Siku za nyuma kuna member mwingine humu aliwahi kuibuka na kudai kuwa rais Magufuli sii Msikuma bali ni Muhaya, akaibuka hadi na jina lake halisi la Kihaya kuwa anaitwa Katto, tulipomuomba atufafanulie ukweli huu, aliingia mitini, sasa leo huyu Gungele naye anaibuka na hoja yake kuwa rais Magufuli ni Muha wa Kakonko anakotoka Kakobe!, nimemuomba athibitishe, wakati tukisubiri uthibitisho huu, ndipo ninauliza, kuna ubaya wowote, Watanzania tukafahamishwa kwa ukweli halisi usiotia shaka na kwa uwazi, asili halisi ya rais Magufuli, jee rais wetu Dr. John Pombe Magufuli asili yake kabisa ni Kabila gani?.

NB. Hii tabia ya baadhi ya viongozi kubadili makabila na kutumia makabila mengine, haikuanza leo, ilianza tangu enzi za Baba wa Taifa, watu walisema humu, hata Mkapa naye akasemwa ni wa kule..., Edward Lowassa inafahamika wazi kwa wengi kuwa ni Mmasai wa Monduli, but in reality, Lowassa Mmeru, ila wazazi wake ndio walihamia Monduli, akazaliwa Monduli, akakulia Monduli, akalelewa Kimasai na kukua na morani wa kule, kwa kupitia hatua zote ikiwemo initiations, hivyo sasa yeye kweli ni Mmasai.

Hitimisho.
Rais Magufuli ni rais wetu, tumemchagua kwa kura zetu, yeye sio malaika bali ni binadamu tuu kama sisi, na hivyo kuweza kufanya makosa na hata dhambi, ila hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kumhukumu binadamu mwingiwe kuwa ni mdhambi, na sio kumhukumu kuwa ni mdhambi, na katika kuijua asili yake, kuna baadhi ya mambo ni mambo yake ya binafsi, na hatupaswi kuyaulizia ili tusiingilie uhuru wake binafsi, yaani his right to privacy, lakini kuijua asili yake, dini yake, kabila lake sisi as taxpayers, we have the right to know details, his public as well as his private conduct haswa katika determination ya truthfulness, morality, na integrity ambayo ni ethical issue ni sifa kuu muhimu kabisa kuliko sifa zote za kiongozi wa nchi.
Jumatano Njema ya Kufungia Mwaka.
Paskali.
Rejea
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."
Tuhuma za udini, ukanda na ukabila katika teuzi, kama wote wana sifa, kuna tatizo gani?.
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi!
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na Zile Boeing ni TT, Then Hatufai!.
https://www.jamiiforums.com/threads...edeye-ni-bomu.570208/page-8n-hatufai.1246099/
Update 1
Haya ni baadhi ya majibu ambayo ambayo ni very objective na yana coherence, na kwakutumia uzoefu wangu wangu wa miaka 27 ya uandishi wa habari, naamini haya yasemwayo ni kweli kwa msingi tuu wa hearsay na third party contributions, confirmation itapatikana kutoka kwa ndugu wa karibu, wana ukoo, next of kin or from the horses mouth.

 
Askofu Kakobe amesema kuwa mamlaka ya Rais, na uwezo wa rais unabaki pale pale, hata kama raia fulani anamkosoa. Askofu Kakobe haoni kwa nini Rais ahangaike kwa kuwa tu kajamaa fulani kamemsema vibaya. Ameenda mbali na kusema kuwa Mungu mwenyewe anasemwa vibaya, na wengine wanamtukana, sembuse kiongozi binadamu.

Askofu Kakobe amesema kuwa msamaha ni tunu kubwa ya uongozi. Amesema kwamba Mungu mwenyewe ni wa msamaha. Amesema kuwa kiongozi anapokuwa mtu wa kusamehe, thawabu zinamwangukia yeye na jamii nzima.
Raisi anatakiwa kutubu hata kama nimejitolea kumtetea
 
Anajiona malaika hawezi kukosea wala kutubu anasahau kuwa hata Mungu tunamkosea kila siku akiwemo yeye raisi lakini Mungu anatusamehe
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana, yaani mtu anazaliwa , anasoma na kukulia hapahapa TZ lakini historia yake haifahamiki, yaani mtu kama Makonda wa juzi tu haijulikani alipozaliwa, wala jina lake halisi, itawezekanaje kwa Uncle aliuezaliwa zamani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…