Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Utangulizi
Tuanze na background issue ni Askofu wa Kanisa la FGBF, Askofu Mkuu, Zakaria Kakobe, amezumza kwa ukali kabisa kumwambia rais Magufuli ni mdhambi na kumtaka atubu, na asipo tubu kuna kitu Mungu atafanya, ila hakusema ni nini


Hii sio thread ya kuzungumzia dhambi za rais Magufuli, bali ni thread ya swali lililotokana na ile kauli ya Kakobe kumtaka rais "Magufuli Atubu", ambayo sasa imekuwa ni kama jambo limezua jambo kwa kauli hiyo kuwaibua watu wanaohoji asili halisi ya rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, baada ya member fulani humu kuibuka na hoja kuwa rais Magufuli na Askofu Kakobe ni watu wamoja, wanajuana vizuri, wote ni watu wa kutoka kijiji kimoja, ni watu wa kabila moja la Waha wa Kakonko. Jee ukweli ni upi?. Jee rais wetu Magufuli ni Msukuma wa Chato, Mhaya wa Wazilankande au ni Muha wa Kakonko?.

Declaration Kuhusu Ukabila
Japo ni bandiko kuhusu ukweli wa asili ya mtu, kuzungumzia asili ya mtu sio ukabila bali hii inaitwa tracing the originality, uki trace the orgin ya asili za makabila mengi ya Tanzania, utashangaa kukuta kumbe makabila ya asili ya Tanzania ni machache, wakiwemo Wasukuma na Wagogo, na makabila ya mikoa ya kati, lakini mengi ya makabila ya Tanzania ni wahamiaji, hivyo watu wote waliokuwepo kwenye ardhi ya Tanganyika kuanzia ile saa 6:00 wa tarehe 9 Desemba, mwaka 1961, ni Watanzania, regardless walizaliwa wapi na asili zao ni wapi, wote tuu Watanzania na tuu wamoja.

Katika bandiko hili pia tutamuangazia kidogo Askofu Kakobe na hoja yake kumtaka rais Magufuli atubu, kama alichofanya ni kitu sahihi au laa!.

Declaration of Interest of Truthfullness
Naomba kuanza na declaration of interest kuwa mimi Paskali Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu na ya kwanza ya tasnia yetu ya habari ni "seek the truth, and tell nothing but the truth!" ikimaanisha ukweli ndio nguzo kuu ya tasnia ya habari, kazi ya mwandishi wa habari wa ukweli ni kuutafuta tuu ukweli na kuandika ukweli huo au kuusema ukweli bali katika kuusema ukweli, mwandishi sio anatakiwa kuusema tuu ukweli no matter what, bali kuusema ukweli utakaoisaidia jamii na kuleta manufaa, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Declaration of Interest ya Usukuma
Kwa vile mimi kwa kabila ni Msukuma, na kwa vile tayari kuna hoja za ukabila na Usukumanaization kwenye awamu hii ya Magufuli, naomba kudeclare my interest kuwa, siandiki bandiko hili kwa ajili ya Usukuma wangu, wala bandiko hili sio la ukabila, na Wasukuma sio wakabila, bali ni bandiko la kuhoji ukweli wa kabila halisi la kiongozi wetu, kwa nia njema kabisa ya kuwa na info, to be informed, kwa imani kuwa hakuna ubaya wowote kwa raia wowote wa Tanzania, kufahamu ukweli wa kabila halisi la kweli na asili halisi ya kweli ya kiongozi wetu.
Essence ya Asili ya Mtu, Kabila na Uongozi wa Nchi.
Najua kuna watu humu wataniponda kwa hoja za ukabila kwa kigezo cha Tanzania ya leo, karne hii ya sayansi, teknolojia na utandawazi, lakini bado watu tunaulizana asili ya mtu au makabila?!'

Hatuulizani kuhusu ni kabila gani ili tuu kujua jina la kabila au kuzijua mila na desturi as if tunataka kutambika, no!. Tunauliza ili tuu kuujua ukweli, mfano kama mimi asili yangu ni Mchagga, Wazazi wangu wakahamia Usukumani, nikazaliwa Usukumani, nikakulia Usukumani, nikasomea Usukumani, na lugha yangu ni Kisukuma, hakuna ubaya wowote kama nitajitambulisha kuwa mimi ni Msukuma mbele ya watu, lakini officially kwenye maandishi ninapaswa kusema ukweli kuwa asili yangu ni Mchagga tulihamia Usukumani, ili akijitokeza mtu anayejua ukweli kuwa Wazazi wangu walihamia tuu Usukumani, akasema mimi sii Msukuma bali ni Mchagga, nisionekane nilipojinasibu ni Msukuma, nilisema uongo!. Hivyo kujua ukweli kuhusu asili ya kiongozi, has nothing to do with ukabila, but has something to do with ukweli na uadilifu, na maadili, truthfulness, integrity and ethics.

Genes za DNA ya Mtu Ndio Determinant ya Traits, Characteristics na Behavior ya Mtu
Tukija kwenye saikolojia ya binadamu kuna kinaitwa traits, hizi traits zinatokana na asili ya mtu, yaani genes mtu anazozaliwa nazo toka kwenye DNA ya wazazi wake halisi, ukichanganya na characteristics na behaviors kutokana na malezi, makuzi na mazingira aliyokulia, ni biggest determinant ya mawazo, maneno na matendo ya mtu huyo for the rest of his/her life, hivyo kila asili, kila kabila na jamii zina traits zake, behaviours zake na characteristics zake, mnaweza kukuta kuna watu wanamchagua kiongozi fulani kutokana na kuzijua traits na characteristics na behaviors za kabila hilo, lakini baada ya kumchagua mkashanga kumuona ana behave differently, tofauti kabisa na watu wa kabila lile, hivyo watu kujikuta mnajiuliza hivi huyu mtu kweli ni kabila hilo?.

Umuhimu wa Asili ya Mtu.
Asili ya mtu na kabila ni muhimu sana kwenye kufanya tathmini ya kitu kinachoitwa psychoanalysis ya behavior ya mtu, hii psychoanalysis hufanya na watu wanaitwa trend readers ambao kazi yao ni kusoma mielekeo, kwa kila jambo linalosemwa, au linalofanywa, watu wa psychoanalysis hawaishii kuangazia mtu kasema nini, au mtu kafanya nini, bali huangalia the motive behind kitu kilichosemwa, au kitu kilichofanywa, ambapo hata kwa rais Magufuli, kama rais wetu, sisi wapenzi wa psychoanalysis tuna analyse baadhi ya mawazo yake, maneno yake na matendo yake, kwa kuangazia the motive behind, kwanini ana behave anavyo behave in a certain situation.

Mfano mimi ni Msukuma Mkristo Mkatoliki, na nimeoa mke Mchagga, Mlutheri wa Machame. Kwetu Usukumani sherehe ya ubarikio sio big deal, kwa Wachagga Walutheri, Kipaimara is a very big deal. Kutohudhuria kipaimara ukweli kule Uchagani lilikuwa kosa kubwa la kuitiwa kikao cha wazazi!.

Kwetu Usukumani kupenda mwanamke zaidi ya mmoja na kupiga mashuti ya off side trick sio big deal saana kivile na miongoni mwa mashuti hayo megine hutokea kwa bahati mbaya, yanafunga magoli ya offside trick na unayahesabu ni magoli halali kumbe kwa mwanamke wa Kichagga, kosa la off side trick ni kosa kubwa la kuvunja ndoa!. Wanaume wa Kisukuma wanaweza kulaumiwa kupenda wanawake wengi kumbe sio kosa lao bali ni kosa la genes za chapa ng'ombe, wana very high sex drive hivyo mwanamke mmoja anakuwa hatoshi hata ajitahidi vipi!.
Mambo ya psychoanalysis nimeyazungumza hapa Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!
Insane Anahitaji Huruma, Kusaidiwa. Sio Kulaumiwa, Kulaaniwa na Kususwa! He Needs Help, Tumsaidieje?.

Kauli ya Kakobe Yaibua Mambo, Mtu Ambadilisha Kabila Rais Magufuli Kuwa Muha wa Kakonko.
Ile kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa na FGBF, Zakaria Kakobe, kumtaka rais Magufuli atubu, inazidi kuibua mambo humu kwenye mitandao ya kijamii, sasa kuna jamaa ameibuka na kudai kuwa rais Magufuli na Askofu Kakobe ni watu wa kabila moja na wametoka kijiji kimoja cha Kakonko kama anavyoeleza hapa mwana jf huyu katika uzi huu.Wanaombeza na kumshambulia Kakobe wachunguzwe .
Kakobe na Magufuli wote Waha wa Kakonko,wapambane tu maana hakuna namna
Mkuu Gungele, jee unaweza kuthibitisha kuwa Magufuli ni Muha wa Kakonko?.

Kama rais wetu, amejinasibu kuwa ni Msukuma, na amejitambulisha kama ni Msukuma, hata ikitokea ni kweli kuwa wewe unamfahamu kwa undani zaidi kuwa kabila lake ni Muha wa Kakonko, huwezi kuja tuu public na kusema tuu kuwa Rais Magufuli ni Muha wa Kakonko wakati sote tunamjua rais wetu Magufuli ni Msukuma wa Chato!, ama thibitisha kauli yako hii, au futa kauli hii!.

Jee Kuna Uwezekano Usukuma na Uchapakazi wa Rais Magufuli Ulichangia Kumletea Ushindi?.
Jee wajua kuwa kuna makabila ya wachapa kazi na makabila ya wavivu wavivu?. Kabila la Wasukuma ni kabila la wachapakazi, mgombea wa kabila la wachapakazi akigombea na mtu wa makabila mengine, wapenda wachapa kazi, watamchagua mchapa kazi. Hivyo kwa vile rais Magufuli ni mchapakazi na ametoka kabila la wachapakazi, kuna uwezekano mkubwa, kuna Wasukuma wengi walimpigia kura rais Magufuli kwa sababu ya uchapakazi wake na sio kwa sababu ya Usukuma wake, ila kuwa tuu ni Msukuma ikwa an added advantage kwasababu kwanza Wasukuma ndilo kabila kubwa kuliko makabila yote Tanzania, hivyo ndilo lenye wapiga kura wengi zaidi, hivyo inawezekana kabisa, japo sio lazima, wapiga kura wa Kisukuma Tanzania nzima walimpigia kura Magufuli kwa Usukuma wake, lakini Watanzania walimpigia kura Magufuli kwa uchapakazi wake, sasa huo uchapakazi ukiujumlisha na Usukuma, kutokana na Wasukuma kuwa ni watu wenye upendo mkubwa sana, ni wapenda watu, wanapenda sana watoto hadi kwa Wasukuma hakuna mambo ya DNA, watoto wowote wanaozaliwa kwa mke wa Msukuma ni watoto wa mwenye mke!.

Wasukuma ni wapole, ni wakarimu, ni wanyenyekevu, ni wastahimilivu, ni watu wenye huruma sana, wana utu, ni wacheshi, ni watu wasiokasirika kwa urahisi,ni watu wasio na jazba, sio waropokaji, na ni watu wenye heshima sana, ukimkuta mwanamke wa kijijini, anatoka kisimani, ndoo ya maji kichwani, mtoto mgongoni na mzigo mkubwa wa kuni mkononi, bado atapiga magoti hadi chini kukusalimia!. Simaanishi Wasukuma ni malaika, licha ya matatizo yao ya kupenda wanawake wengi, kupenda wanawake weupe, na kuhonga sana, lakini ni watu wanaofaa sana kwa urais, yaani Wasukuma ni presidential material, hivyo kuna uwezekano wa wengi walimpigia kura nyingi rais Magufuli kutokana uchapakazi wake, ule Usukuma wake ukawa ni just an added advantage, sasa akitokea mtu leo from no where, anaibuka jf na kusema rais Magufuli sio Msukuma bali ni Muha wa Kakonko!, huku si kunaweza kupelekea wale wote waliomchagua rais Magufuli kwa added advantage ya Usukuma wake, wakajidhania kuwa walidanganywa?.

Tusijidanganye: Dhana ya Ukabila Kwenye The Political Landscape in Tanzania Ipo na ina Exist!.
Kwa kutumia kanuni ile ile ya kuwa mkweli daima, hata kama ukweli huo utakuwa ni mchungu kiasi gasi, lazima usemwe, kwenye the political landscape in Tanzania, ukanda na ukabila una play the biggest role, ili mtu au chama kishinde urais wa Tanzania, ni lazima kivune kura za kutosha kutoka Kanda ya Ziwa. Kura za Kanda ya Ziwa ndizo kura determinant ni nani anakuwa rais wa Tanzania, na hili nililizungumza tangu mwaka 2010 wakati Chadema walipoiteka Kanda ya Ziwa, nilipandisha uzi huu, nikiamini CCM imekwisha, Chadema inaingia Ikulu 2015, ila kilichotokea 2015 ndicho kile kile nilichokizungumza kwenye nyuzi hizi
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni!
Kuelekea 2015: Ni Mbio Za Magari Kati ya Mkweche na Mashine Mpya!

Jee Wajua 2015, CCM Ingemsimamisha Mtu Mwingine Yoyote Zaidi ya Magufuli, Ingeshindwa!, Kilichomfanya Magufuli Ashinde, Sio Tuu Uchapakazi Wake Bali pia ni...
Sii wengi wanatambua kuwa hata siasa ni sayansi, inaitwa sayansi ya siasa, political science, kufuatia Edward Lowasa kuzianza harakati za kuitafuta Ikulu kipindi kirefu kabla, wataalamu wa sayansi ya siasa wa CCM wanaojua kutazama mbali, waliliona hili kuwa Lowassa asiposimamishwa na CCM akahamia chama kingine chochote na kugombea, CCM itapigwa chini, hivyo wakaangalia ni mtu gani ataweza kumkabili Lowassa ndani ya CCM na kuipa ushindi, ndipo wakaamua mtu pekee ni John Pombe Magufuli, wakati hao waliomua kuwa 2015 mgombea wa CCM ni Magufuli, inawezekana wakati huo, hata Magufuli mwenyewe hakuwa anajua, lakini mimi ni miongoni mwa watu wachache sana waliopata Bahati ya kujua kwa nini 2015 lazima awe ni Magufuli na Mwezi Agust 2014, nilipandisha bandiko hili nikaeleza kuwa 2015 mgombea wa CCM ni Magufuli kwa sababu fulani fulani
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Japo Tanzania Haina Dini na Hatuna Ukabila, Jee Kuna Ubaya Wowote Watu Kuhoji Dini au Kabila Halisi la Mtu?.
Naamini japo nchi yetu haina dini, lakini watu wake wana dini zao, na japo hatuna ukabila, watu wote wana makabila yao, ndizo asili zao, hivyo naamini hakuna ubaya wowote watu kuhoji na kujua dini za viongozi wetu, au makabila halisi ya viongozi wetu, mfano rais wetu John Magufuli ni Mkristo Mkatoliki, na aliwahi kusema wazi kuwa ni kupitia kusali Rozari Takatifu, ndiko kumemuwezesha kuupata urais, akitokea mtu anayemfahamu kwa undani na kusema kuwa huyu sio Mkatoliki, lazima wale wa kujiuliza watajiuliza ukweli wa hoja hii!, na kama ikitokea ni kumzushia tuu, huu utakuwa ni uchochezi!.

Vivyo hivyo kwenye ukabila, ikitokea kama tunajua kuwa Rais Magufuli ni Msukuma wa Chato, halafu akaibuka mtu, anayeijua haswa historia ya Magufuli na asili yake halisi, akaibuka na kusema kuwa rais Magufuli sio Msukuma wa Chato bali ni Muha wa Kakonko, kama mtu huyu atakuwa ndio mkweli na huu ndio ukweli wa mambo, jee anaweza kuitwa ni mchochezi?. Inawezekana kuusema ukweli unaojua kuwa ni ukweli halisi, ukawa ni uchochezi?.
Hili la watu humu kuusema kila ukweli wanaoujua, nimelizungumza hapa
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
Tuiangazie Kidogo hoja ya Kakobe Kumtaka Magufuli Atubu.
Jee Kakobe Yuko Right Kumwambia Rais Magufuli Atubu?.
Kuhusu alichokisema Askofu Kakobe kama kiongozi wa kidini na kiongozi wa kiroho, yuko right kuwaamuru waumini wake tuu kuwa watu, kama rais Magufuli ni muumini wa kanisa lake, then he is right kumtaka atubu, lakini kama rais Magufuli sio muumini wake, then Askofu Kakobe, hana mamlaka ya kumtaka rais Magufuli kutubu, mamlaka yake yanaishia kwa waumini wake tuu, hivyo Askofu Kakobe is not right kumtaka rais Magufuli atubu, mtu ambaye yuko right kumtaka rais Magufuli atubu ni Muadhama Policarp Kardinali Pengo lakini hata Pengo hawezi kumuamuru Magufuli atubu, huko kutakuwa ni kumuhukumu, anachoweza ni kumhubiria tuu habari njema ya neno la Mungu na kumsisitiza asitende dhambi au uovu na suala la kutubu ni suala binafsi.

Hoja za Kakobe Kwa Nini Magufuli Atubu, Zote ni Valid, ila Kumuamuru Atubu ni Invalid.
Katika mahubiri hayo ya Askofu Kakobe alitoa hoja tatu kuu kumhusu rais Magufuli ambazo zote ni very valid, ni hoja za kweli na ndicho kinachotokea sasa Tanzania, invalidity ni hoja moja tuu ya kumuamuru atubu!. Hili sio bandiko la hoja za Kakobe, ni kuhusu amri yake kumtaka atubu sio amri halali, ila pia Kakobe alimalizia kwa kutoa onyo kuwa rais Magufuli asipotubu, Mungu atafanya kitu, lakini hakusema ni kitu gani!. Kwa vile namfahamu Kakobe has powers, kama ni kweli rais Magufuli amefanya hizo dhambi, then atubu tuu maana asipotubu...

Process ya Kutubu kwa Wakatoliki Kunaitwa Kuungama ni Inafanyika Wazi na Transparent, or Behind Closed Doors for Confidentiality
Kwa sisi Wakristo Wakatoliki, ukifanya dhambi, unatakiwa kwenda mbele ya padre, kwanza kwa kukuri dhambi, kwa kumwambia padre ukweli wa ulichotenda, kisha unatubu kwa kuungama dhambi zako mbele ya padre katika eneo la wazi, hivyo wakristo wengine wote mnakwenda kuungama mnaonana wazi wazi huyu ni fulani na huyu ni fulani mkisubiri kuungama kwa kupiga magoti mbele ya padre na kutubu zambi zetu hivi tuko very transparent. Ila pia process hii huweza kufanyika behind the closed doors kwa kufanya appointment ya kuungama, hivyo mtu mtu unapangiwa siku yako maalum ya kuja kuungama peke yako bila mtu mwingine yoyote kujua just for confidentiality kidunia ila sio mbele ya Mungu.

Lakini Dhima ya Kutubu ni Dhamira ya Mtu, The Content Maungamo ni Very Confidential. Maondoleo ya Dhambi ni Sakramenti ya Kitubio.
Japo process ya kutubu dhambi kwa Wakatoliki ni transparent kwa kwenda physically na transparently kutubu, na kuwajibika kuwa open na transparent kwa padre umefanya dhambi gani, yet maungano ni very freely, private na confidential kwa sababu uamuzi wa kuungama ni uamuzi binafsi wa dhamira ya mtu mwenyewe kuamua kuungama na sio kushurutishwa kuungama!. Hivyo kanuni ya kunyooshea kidole mdhambi yoyote na kumwambia akaungame!. Na kule kwenye kuungama hakuna kutaja jina wewe ni nani, na hata kama umefanya dhambi ya kuua, unasema tuu nimeua mtu, bila kumtaja mtu huyo, au umumuuaje kwa panga, kwa risasi kwa sumu etc, dhambi ni kuua na sio umeuaje!.

Pili padre anayepokea kutubu kwako au maungamo yako, hatakiwi kukuona, waka kukuangalia, bali huweka tuu sikio kwenye kitundu cha kusikiliza sauti tuu na kitundu hicho kimefunikwa na kitambaa cheusi ili ni sauti tuu ipite, padre asiweze kumuona ni nani anayetubu, ili asikufahamu, (japo kutokana na uumini wa muda mrefu, mapadri wanazizua sauti za baadhi ya waumini wao prominent). Wakati wa kuungamani, padre anayekuungamisha hapaswi kukuuliza maswali yoyote. Wewe kazi yako ni kutubu tuu makosa yako, na yule padre unayetubu kwake ni Mwakilishi wa Mungu, anapokea, anakabidhi kwa Mungu, na kupokea maelekezo ya Mungu kukupa wewe dhambi zako ziondolewe.

Japo Kuungama ni Kwa Padri, Dhambi Zinaondolewa na Mungu Mwenyewe.
Bwana wetu Yesu Kristu, kabla ya kupalizwa mbinguni alitoa mamlaka kwa mapadri wa Katoliki kuwa "watakachokifungua duniani, na mbinguni kinafunguliwa, na watachokifunga duniani na mbinguni kinafungwa", hivyo kutubu au kuungama kwa padre ni just a vehicle tuu, anayetubiwa dhambi ni Mungu, na anayeondolea dhambi sio padri, ni Mungu mwenyewe, binadamu hana mamlaka ya kunyooshea kidole binadamu mwingine yoyote kuwa ni mdhambi.

Kuhusu hoja mbalimbali zinazoibuliwa na Askofu Kakobe, niliwahi kushauri humu, asipuuzwe
Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians!, hivyo namshauri rais wetu, hata kama hana dhambi yoyote, one day akasali tuu kwa Kakobe na kusema ametubu, he'll have everything to gain and nothing to loose, lakini asipotubu...naomba nisimalizie...
Turudi kwenye mada kuu
Jee Rais Magufuli ni Msukuma, Muhaya au Muha wa Kakonko?.
Siku za nyuma kuna member mwingine humu aliwahi kuibuka na kudai kuwa rais Magufuli sii Msikuma bali ni Muhaya, akaibuka hadi na jina lake halisi la Kihaya kuwa anaitwa Katto, tulipomuomba atufafanulie ukweli huu, aliingia mitini, sasa leo huyu Gungele naye anaibuka na hoja yake kuwa rais Magufuli ni Muha wa Kakonko anakotoka Kakobe!, nimemuomba athibitishe, wakati tukisubiri uthibitisho huu, ndipo ninauliza, kuna ubaya wowote, Watanzania tukafahamishwa kwa ukweli halisi usiotia shaka na kwa uwazi, asili halisi ya rais Magufuli, jee rais wetu Dr. John Pombe Magufuli asili yake kabisa ni Kabila gani?.

NB. Hii tabia ya baadhi ya viongozi kubadili makabila na kutumia makabila mengine, haikuanza leo, ilianza tangu enzi za Baba wa Taifa, watu walisema humu, hata Mkapa naye akasemwa ni wa kule..., Edward Lowassa inafahamika wazi kwa wengi kuwa ni Mmasai wa Monduli, but in reality, Lowassa Mmeru, ila wazazi wake ndio walihamia Monduli, akazaliwa Monduli, akakulia Monduli, akalelewa Kimasai na kukua na morani wa kule, kwa kupitia hatua zote ikiwemo initiations, hivyo sasa yeye kweli ni Mmasai.

Hitimisho.
Rais Magufuli ni rais wetu, tumemchagua kwa kura zetu, yeye sio malaika bali ni binadamu tuu kama sisi, na hivyo kuweza kufanya makosa na hata dhambi, ila hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kumhukumu binadamu mwingiwe kuwa ni mdhambi, na sio kumhukumu kuwa ni mdhambi, na katika kuijua asili yake, kuna baadhi ya mambo ni mambo yake ya binafsi, na hatupaswi kuyaulizia ili tusiingilie uhuru wake binafsi, yaani his right to privacy, lakini kuijua asili yake, dini yake, kabila lake sisi as taxpayers, we have the right to know details, his public as well as his private conduct haswa katika determination ya truthfulness, morality, na integrity ambayo ni ethical issue ni sifa kuu muhimu kabisa kuliko sifa zote za kiongozi wa nchi.
Jumatano Njema ya Kufungia Mwaka.
Paskali.
Rejea
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."
Tuhuma za udini, ukanda na ukabila katika teuzi, kama wote wana sifa, kuna tatizo gani?.
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi!
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na Zile Boeing ni TT, Then Hatufai!.
https://www.jamiiforums.com/threads...edeye-ni-bomu.570208/page-8n-hatufai.1246099/
Update 1
Haya ni baadhi ya majibu ambayo ambayo ni very objective na yana coherence, na kwakutumia uzoefu wangu wangu wa miaka 27 ya uandishi wa habari, naamini haya yasemwayo ni kweli kwa msingi tuu wa hearsay na third party contributions, confirmation itapatikana kutoka kwa ndugu wa karibu, wana ukoo, next of kin or from the horses mouth.
Kuna kijiji kimoja kinaitwa KATOMA Katikati ya Nyamboge na nkome mkoani Geita tarafa ya Bugando, hapo kijijini kuna kaburi LA BABU yake na Mkulu wetu nimewahi kufika hapo na wakazi wa hicho kijiji wanadai Mzee magufuli (siyo jina halisi) Walimuita wenyeji kutokana na ukorofi wake na kuwashitaki watu na kuwafunga, Alikuwa Mzee mwenye ng'ombe wengi sana na Alihamia hapo kijijini akitokea Kati ya nchi ya Rwanda au Burund kwa kisukuma huitwa (bwadushi)(Tutsi) Hivyo huyu Mzee alikuwa mhamiaji na Alifia hapo katoma na kuzikwa hapo ndipo Baba yake na Mkulu wetu na ndg wengine walipohamia Biharamlo mkulu akiwa Mdogo sana hajaanza hata shule na shule alienda kuanzia kule,,

Paskali, kuna mtu yeyote mwenye uthibitisho wa wazi unaoonesha mahali popote JPM aliwahi kutamka yeye mwenyewe kuwa ni Msukuma?

Maelezo ya baadhi ya watu ni kuwa JPM alizaliwa Bukoba. Na yeye alipoenda Bukoba aliwaeleza watu kwenye mkutano kuwa Bukoba ni nyumbani pake maana hata babu yake (alimtaja na jina) amezikwa karibu na mnara wa Mayunga. Japo alizaliwa Bukoba, haimaanishi kuwa ni Mhaya. Yeye kwa maelezo yake alisema kuwa ni wa ukoo wa Mzilankende, ukoo ambao upo kwa Wahaya na waha, na siyo kwa wasukuma.

Maelezo ya ziada ambayo sina uthibitisho, ni kuwa wazazi wake walihamia Bukoba wakitokea Kigoma. Jambo ambalo siyo la ajabu kwa wakazi wa Bukoba maana wanapakana.

Maelezo mengine ni kuwa Baba yake wa Kambo ni Msukuma. Hivyo JPM alikulia katika mazingira ya usukumani na kulelewa na Baba ambaye ni msukuma. Je, ni kosa kwa mtoto kujitambulisha kwa kabila la Baba mlezi au Baba yake wa kambo?

Paskali, kwa sababu wengi inaonekana wanataka kujua biography ya JPM, unaweza kumwomba JPM mwenyewe, ili uweze kuandika kitabu kinachohusu maisha yake binafsi. Nina hakika kitapata wateja.
Mwezi wa saba mwaka huu nikiwa biharamulo nyumbani nilikutana na ndugu zangu.katika maongezi yetu tuligusia kuhusu utendaji wa JPM. Sasa ndugu mmoja akanambia kuwa suala la JPM kuwa mtu wa chato ni sawa ila wazazi wake ni WAHA kutoka KIBONDO (zamani lkn sasa ni wilaya ya KAKONKO). Ushuhuda ni kwamba JPM na wazazi wake asili yao ni kata ya BUKILILO jilani na kata ya KASANDA.
Nilichoelezwa na ndugu yangu ni kuwa familia ya wazazi wa JPM walikuwa na mgogoro wa kindoa hata kabla ya JPM hajazaliwa na hapo ikabidi ndoa ivunjike.Mama Yake JPM aliondoka BUKILILO akiwa mjamzito na kwenda CHATO na kuanza maisha mapya huku akiwa mjamzito.(inasemekana kuwa baba MZAZI Wa JPM alibaki BUKILILO baada ya ndoa kuvunjika.)
Kwa walioko BUKILILO na wanamfahamu baba halisi wa JPM walishangaa kusikia eti JPM ni msukuma wakati wazazi ni waha tena jimbo la BUYUNGU kwa Injinia ATASHSTA NDITIYE ( Naibu waziri - uchukuzi zamani jimbo likiwa kwa Injia CHRISTOPHER CHIZA aliyewahi kuwa Waziri wa kilimo na umwagiliaji.)
Ukoo wa Wazilankende upo pia katika kabila la waha kama ilivyo kwa wahaya.
Nayaongea haya kwakuwa nina ndugu zangu WAHA na Mimi ni Muha japo kwa sasa tunaishi Biharamulo tangu 2003. Kuna wazee wanamfahamu baba Yake mzazi wa JPM aishiye Bukililo.
Mzalendo2015
Ukianza kufuatilia asili ya watu waishio KIGOMA na kagera wengi wao ni kutoka Burundi ama Rwanda.sababu ni kwamba mipaka ya nchi jilani na mikoa hii inaingilika.mfano halisi ni kwamba wakati tunaishi kakonko eneo la Malenga ilikuwa rahisi kuvuka mipaka kwenda Gisagara na Chankuzo ambayo ni mikoa ya Burundi kwa urahisi.
Pia warundi wengi wako kigoma na kujipatia uwenyeji na kuwa wakazi halali ( kwa mujibu wao) kwani kabla walikuja kama vibarua Wa kulima (warundi wanasifika kwa uhodari Wa kulima) sasa wakifika huanza kujifunza lafudhi ya kiha.Kwao lugha siyo tatizo kwani kiha na kirundi maneno ni Yale yale.
Wakishajua lafudhi huhamia mikoa mingine kama Kagera,Tabora ama Dsm huku wakijinasibi kuwa ni waha.Kwahiyo katika msingi huo watu wa kigoma na kagera wana ndugu zao burundi.
Kwa sasa niko dsm na kwakuwa kiha ndo lugha yangu, kirundi kwangu siyo taabu.Nilishangaa kuwakuta warundi wengi huku dsm wakijinasibu kuwa ni waha.Kwa walioko dsm Kigamboni maeneo ya kwa Urasa ajaribu kuwachunguza wale wauza maji chini ya mti karibu na banda la video atajua kuwa ni waha lkn kwa mtu anayejua kiha atagundua tofauti ya kiha chao na kiha halisi.
Jpm Kuwa Muha sishangai kwani baba yake alitengana na mama yake kabla hata JPM hajazaliwa.
 
Askofu Kakobe amesema kuwa mamlaka ya Rais, na uwezo wa rais unabaki pale pale, hata kama raia fulani anamkosoa. Askofu Kakobe haoni kwa nini Rais ahangaike kwa kuwa tu kajamaa fulani kamemsema vibaya. Ameenda mbali na kusema kuwa Mungu mwenyewe anasemwa vibaya, na wengine wanamtukana, sembuse kiongozi binadamu.

Askofu Kakobe amesema kuwa msamaha ni tunu kubwa ya uongozi. Amesema kwamba Mungu mwenyewe ni wa msamaha. Amesema kuwa kiongozi anapokuwa mtu wa kusamehe, thawabu zinamwangukia yeye na jamii nzima.
Raisi anatakiwa kutubu hata kama nimejitolea kumtetea
 
Askofu Kakobe amesema kuwa mamlaka ya Rais, na uwezo wa rais unabaki pale pale, hata kama raia fulani anamkosoa. Askofu Kakobe haoni kwa nini Rais ahangaike kwa kuwa tu kajamaa fulani kamemsema vibaya. Ameenda mbali na kusema kuwa Mungu mwenyewe anasemwa vibaya, na wengine wanamtukana, sembuse kiongozi binadamu.

Askofu Kakobe amesema kuwa msamaha ni tunu kubwa ya uongozi. Amesema kwamba Mungu mwenyewe ni wa msamaha. Amesema kuwa kiongozi anapokuwa mtu wa kusamehe, thawabu zinamwangukia yeye na jamii nzima.
Raisi anatakiwa kutubu hata kama nimejitolea kumtetea
Anajiona malaika hawezi kukosea wala kutubu anasahau kuwa hata Mungu tunamkosea kila siku akiwemo yeye raisi lakini Mungu anatusamehe
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana, yaani mtu anazaliwa , anasoma na kukulia hapahapa TZ lakini historia yake haifahamiki, yaani mtu kama Makonda wa juzi tu haijulikani alipozaliwa, wala jina lake halisi, itawezekanaje kwa Uncle aliuezaliwa zamani?
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom