Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko?

Wanabodi,

Hii ni thread ya swali kuwa ile kauli ya Kakobe kuwa "Magufuli Atubu", yaibua mambo!. Kumeibuka watu wanaohoji asili halisi ya rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, baada ya member Fulani humu kuibuka na hoja kuwa Magufuli ni Muha wa Kakonko anakotoka Kakobe, sasa ukweli ni upi?. Jee rais wetu Magufuli ni Msukuma Chato, Mhaya au Muha wa Kakonko?

Declaration of Interest
Naomba kuanza na declaration of interest kuwa mimi ni Msukuma, na kwa vile tayari kuna hoja za ukabila na Usukumanaization, naomba kudeclare kuwa mimi sio mkabila, na hili sio bandiko la ukabila, bali ni bandiko la kuhoji ukweli wa kabila halisi la kiongozi wetu, kwa nia njema kabisa ya kuwa na info, kwa Imani kuwa hakuna ubaya wowote kwa raia wowote wa Tanzania, kufahamu kabila halisi na asili ya kiongozi wetu.

Kauli ya Kakobe Yaibua Mambo, Mtu Ambadilisha Kabila Rais Magufuli Kuwa Muha wa Kakonko.
Ile kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa na FGBF, Zakaria Kakobe, inazidi kuibua mambo humu kwenye mitandao ya kijamii, sasa kuna jamaa ameibuka na kudai kuwa rais Magufuli na Askofu Kakobe ni watu wa kabila moja na wametoka kijiji kimoja cha Kakonko kama anavyoeleza hapa mwana jf huyu katika uzi huu.Wanaombeza na kumshambulia Kakobe wachunguzwe .Mkuu Gungele, jee unaweza kuthibitisha kuwa Magufuli ni Muha wa Kakonko na sio Msukuma wa Chato kama tulivyo aminishwa?, vinginevyo huu utakuwa ni uchochezi tuu!.

Kama rais wetu, amejinasibu kuwa ni Msukuma, na amejitambulisha kama ni Msukuma, hata ikitokea ni kweli kuwa wewe unamfahamu kwa undani zaidi kuwa kabila lake halisi si Msukuma, bali ni Muha wa Kakonko, lazima uweze kuthibitisha, vinginevyo huwezi kuja public na kusema tuu kuwa Rais Magufuli ni Muha wa Kakonko wakati sote tumeambiwa na kuaminishwa ni Msukuma wa Chato!, futa kauli hii!.

Jee Kumbadili Kabila Kiongozi wa Nchi ni Uchochezi?.
Jee wajua kuna uwezekano mkubwa, kuna Wasukuma wengi walimpigia kura Magufuli kwa sababu waliamini ni Msukuma, kutokana na Wasukuma kuwa ni watu wenye upendo mkubwa sana, ni wapenda watu, wanapenda sana watoto hadi kwa Wasukuna hakuna mambo ya DNA, watoto wowote wanaozaliwa kwa mke wa Msukuma ni watoto wa mwenye mke!.

Wasukuma wapole, wanyenyekevu, wastahilivu, wenye huruma, utu, wacheshi, wasiokasirika kwa urahisi, wasio na jazba, wasio ropoka ropoka onyo, licha ya matatizo yao ya kupenda wanawake wengi, kupenda wanawake weupe, na kuhonga sana, lakini ni watu wanaofaa sana kwa urais, hivyo wakampigia kura nyingi rais Magufuli kwa sababu tuu ya usukuma wake, halafu leo mtu from no where, anaibuka jf na kusema rais Magufuli ni Muha wa Kakonko!, huku si kunaweza kupelekea wale wote waliomchagua Magufuli kwa Usukuma wake, wakajidhania kuwa walidanganywa?. Huu sio uchochezi?.

Japo Tanzania Haina Dini na Hatuna Ukabila, Jee Kuna Ubaya Wowote Watu Kuhoji Dini au Kabila Halisi la Mtu?.
Naamini japo nchi yetu haina dini, hakuna ubaya wowote watu kuhoji na kujua dini za viongozi wetu, mfano rais wetu John Magufuli ni Mkristo Mkatoliki, na aliwahi kusema wazi kuwa ni kupitia kusali Rosali Takatifu, ndiko kumemuwezesha kuupata urais, akitokea mtu anayemfahamu kwa undani na kusema kuwa huyu jamaa sio Mkatoliki kwa sababu hakuwahi kubatizwa, au kupata sacrament za kumunia na kipaimara, na huwa anafanya matambiko, jee mtu huyu atakuwa sio mchochezi?.

Au ikitokea kama tulivyoaminishwa kuwa Rais Magufuli ni Msukuma wa Chato, halafu akaibuka mtu, anayeijua haswa historia ya Magufuli na asili yake halisi, akaibuka na kusema kuwa rais Magufuli sio Msukuma bali ni Muha wa Kakonko, kama mtu huyu atakuwa ndio umkweli na huu ndio ukweli wa mambo, jee anaweza kuitwa ni mchochezi?. Inawezekana kuusema ukweli unaojua kuwa ni ukweli halisi, ukawa ni uchochezi?.

Jee Rais Magufuli ni Msukuma, Muhaya au Muha wa Kakonko?.
Siku za nyuma kuna member mwingine humu aliwahi kuibuka na kudai kuwa rais Magufuli sii Msikuma bali ni Muhaya, akaibuka hadi na jina lake halisi la Kihaya kuwa anaitwa Katto, tulipomuomba atufafanulie ukweli huu, aliingia mitini, sasa leo huyu Gungele naye anaibuka na yake kuwa rais Magufuli ni Muha wa Kakonko anakotoka Kakobe!, nimemuomba athibitishe, wakati tukisubiri uthibitisho huu, ndipo ninauliza, kuna ubaya wowote, Watanzania tukafahamisha kwa ukweli asili usio na chenga zozote jee rais wetu Dr. John Pombe Magufuli asili yake kabisa ni Kabila gani?.

Ili kupata majibu yakweli ya ya ukweli huu, tunaomba members wowote wa jf, wenye data za ukweli na uhakika kuhusu rais wetu watuletee kwa kuyajibu haya maswali simple
  1. Jee alizaliwa lini na wapi?.
  2. Wazazi wake halisi ni nani?.
  3. Asili ya wazazi hao ni wapi?.
  4. Ni kweli aliwahi kuitwa Katto?.
  5. Ilikuwa akaibukia Chato?.
  6. etc, etc
NB. Hii tabia ya baadhi ya viongozi kubadili makabila na kutumia makabila mengine, haikuanza leo, ilianza tangu Enzi za Baba wa Taifa, watu walisema humu, hata Mkapa naye akasemwa ni wa kule..., Edward Lowassa inafahamika kwa wengi kuwa ni Mmeru, ila wazazi wake ndio walihamia Monduli, akazaliwa Monduli, akakulia Monduli, akalelewa Kimasai na kukua na morani wa kule, kwa kupitia hatua zote ikiwemo initiations, hivyo sasa yeye kweli ni Mmasai.

Jumatano Njema ya Kufungia Mwaka.
Paskali.
Rejea
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."
Tuhuma za udini, ukanda na ukabila katika teuzi, kama wote wana sifa, kuna tatizo gani?.
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi!
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na Zile Boeing ni TT, Then Hatufai!.
https://www.jamiiforums.com/threads...edeye-ni-bomu.570208/page-8n-hatufai.1246099/
Sintofahamu zote hizi ni kutokana na kazi yake, angekua legelege yote haya yasingeulizwa, Kweli bongo tuanongoza kwa majungu dunia nzima, ni chuo kikuu cha dunia cha majungu
 
Magufuli ni msubi jamii Fulani yenye mwenendo wa kihaya .babu zake waliishi katoma bkb zamani wengine wapo mpaka Leo kama mzee machalila aliyeishi uswahilini ila wameishi usukumani maeneo ya chato lakini kasomea biharamulo kagera
WASUBI NA WAHAYA WAPI NA WAPI MZEE IKO HIVIIII.......

WASUBI NA WAHA NDIO JAMIII MOJA NA LUGHA YAO NI MOJA YAANI MSUBI NA MUHA NI SAWA NA MNYAMWEZI NA MSUKUMA.
WANATOFAUTIANA MANENO MACHACHE SANA......
 
Eti wasukuma wana utu, huruma, hivi mngeongoza kwa kuuana na kuuwa vikongwe na albino?
Pili, hivi kabila la Rais linasaidia nini nchi au mwananchi wa kawaida? Kama ni msukuma, muha au mhaya atapimwa kwa uwajibikaji wake na sio kabila lake.
Mpaka sasa hivi
Unahisi amefanya nini cha maana na
-Embu vita picha after 3 year tutakuwa wapi na hii hali ya kuvuruga uchumi
-hatukatai hii inchi ilikuwa Shamba la bibi but ilitakiwa weledi mkubwa sana utumike katika kuvunja hiyo mianya ya ufujaji wa hela za wananchi iliyokuwepo na si kutumia mihemko na kutatua hizo changamoto.
 
Anayeweza kufahamu uhalisia wa kabila la dr John Pombe Magufuli ni wazazi kwa sababu wengine wanadai ni asili ya Mkoa wa Mara kati ya Mluo na Mjita. Lakini miye nadhani haya hayana maana kwetu sisi watanzania
Naamini vyema tukajadili mambo yenye tija kwa Taifa kuliko kujadiliana kuhusu ukabila wa viongozi. Haya mambo ya ukabila tuwaachie wachaga wa chadema ndiyo wanayaweza
WACHAGGA WAMEKUKOSEA NINI
 
Anayeweza kufahamu uhalisia wa kabila la dr John Pombe Magufuli ni wazazi kwa sababu wengine wanadai ni asili ya Mkoa wa Mara kati ya Mluo na Mjita. Lakini miye nadhani haya hayana maana kwetu sisi watanzania
Naamini vyema tukajadili mambo yenye tija kwa Taifa kuliko kujadiliana kuhusu ukabila wa viongozi. Haya mambo ya ukabila tuwaachie wachaga wa chadema ndiyo wanayaweza
Unakataza nini na mwisho umeandika nini?inaelekea ukiwa CCM na akili zinaenda likizo
 
Kumeibuka watu wanaohoji asili halisi ya rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, baada ya member Fulani humu kuibuka na hoja kuwa Magufuli ni Muha wa Kakonko anakotoka Kakobe, sasa ukweli ni upi?. Jee rais wetu Magufuli ni Msukuma Chato, Mhaya ?
Wengine wanadai ana asili ya nchi jirani ukandabhuo.kabila lake naona utata.kwa nini iwe hivyo?[/QUOTE]
 
Paschal ametumwa kututoa kwenye hoja ya msingi ya Rais kufanya toba!!! Kabila la Rais hatuna shida nalo hata kidogo

All we want ni Rais ATUBU.
 
Magufuli kama Magufuli ni mwanadamu na hajakamilika hata yeye huwa anasema hayo maneno kila mara na huwa anakwenda kanisani na huko makanisani tunajua kila mmoja ni kuenda kumsifu Mungu na kuomba msamaha kwa kila dhambi uliyotenda kwa makusudi na dhambi ambazo hata hujui kama ulitenda ili Mungu wa mbinguni akusamehe sasa hayo ni mambo very persona au binafsi mtu na Mungu wake katika ulimwengu wa Roho huwezi kumuingilia kabisa.

Hata Katiba ya nchi ya mwak 1977 haijamlazimisha mtanzania kumtambua Mungu au kumlazimisha mtanzania kwenda kanisani au msikitini ingawa inatambua uhuru wa kuabudu Mungu.

Kwangu mimi ushauri wa Askofu ni kuingilia mambo ya mtu binafsi kitu ambacho Katiba inazuia.Nadhani Askofu anatakiwa kuangaliwa kwanza boriti katika jicho lake kabla ya kuangalia kibanzi katika jicho la Magufuli.
Watazania bado tunaulizana makabila!!!??? Kweli watanzania ss bado tupo gizani!! KABILA!!?? na huyu mungu aitwae kakobe amepata wp huo utakatifu?! Huyu mungu wa UKAWA NA MUNGU WA LOWASSA.amepata wapi huo utakatifu??!!hv hawa watakatifu akina kakobe.gwajima.na wengeneo huwa wanatubu kw nani wao?! Na huwa anawaombea nani?! Cku ya mwisho anaijua mungu alie hai muumba mbingu na nchi.na ole wao watumiao jina lake kw uchawi na utapeli.
 
Back
Top Bottom