Kauli ya kafulila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya kafulila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, Dec 1, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hii ni kwa mujibu wa gazeti la mwananchi dec, 1 '09. Binafsi sijaona uzito wowote katika kumzungumzia huyu kijana zaidi ya kumkuza bila sababu ya msingi. Ila kwa kauli yake hii, 'wanachama hao wanatarajia kurudisha kadi za chadema na kujiunga rasmi na NCCR Mageuzi.' huyu dogo kafadhiliwa na zitto kwenda kufanya mkutano. Hapo hapo anakisema vibaya chadema. Ina maana zitto nae yuko on transit? Anaichukuliaje kauli ya kafulila? Chadema wanamwona vipi zitto? Hii inatupa picha kuwa siasa ni uhuni tu, au ni ya wahuni tu bila kujali haiba ya mtu. Kwa kauli kama hizo tuwachukulie vipi wanasiasa?
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sasa kama chama kimefulia kikisemwe! Na mwanachama ana uhuru wa kwenda chama chochote na kukiacha alichonacho kama anaona hakina mwelekeo wa ukweli na uzalendo halisi
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  maneno ya Nyerere hayawezi kupita bure "UPINZANI WA KWELI LAZIMA UTOKE NDANI YA CCM"
   
 4. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tunamuomba Mh. Zitto, kwakua anaonyesha mapenzi makubwa kiiasi cha kufadhili mahasimu wa Chama na watu wanoasema hovyo chama na viongozi wenzake wa chama aondoke maramoja amfuate huyo kipenzi chake kafulila na atuachie chama chetu.

  Ni dhahiri si mbaya mtu na rafiki yake au hata mke/mume kuwa vyama tofauti, lakini kitendo cha kusupportiana hadharani ilihali ukiwa kama kiongozi na wewe anuatukanwa, hii inaletwa mkanganyiko. Na inasababisha watu kuhoji uwezo na busara za kiuongozi wa huyu mtu.

  Mfano sote twajua mke wa Dr Slaa ni diwani wa CCM lakini hakuna uthibitisho wa wazi kwamba mzee amekua akimpa facility za kumsuport akiangushe chama. Kitendo cha Zitto kumfadhili huyu dogo akakimomonyoe chama kigoma kimeonyesha upeo wake mdogo wa kioungozi na ameshindwa kusimama na kujitofautisha kama kiongozi na kujikita zaidi kwenye urafiki. Huyu mtu hafai na tukiwaendekeza watu kama hawa tutaua chama. Thanks God huyu mtu hakupewa dhamani akiongoze chama, maana ushkaji/Uanamtandao ungejazana kuliko hata serikali ya JK. Tufike mahali kama viongozi tujifunze kusimamia maadili yetu ya uongozi na kuonyesha busara za kuoingozi na kuweka urafiki pembeni.

  Tukiendelea kuwakumbatia watu kama hawa sioni tukifika popote. Chadema chukueni hatua mapema dhidi ya huyu mtu.

  Yetu macho
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Amekuwa dogo sasa! Awali aliitwa sisimizi.... naona soon atakuwa kaka....!
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Zito kigeu geu, amepoteza sifa za kuaminiwa ndani ya Chama, mtu anaejitokeza mara kwa mara kama muharibifu na mzandiki chamani, najua anajidai kua amerisign kuchangia hoja humu JF lakini kuna tetesi kuwa tunashinda nae akijitetea kwa kutumia kivuli cha mtu mwingine, uhodari na mbwembwe zake zote zimeingia ******, anaanza kua na tahadhali kuzungumzia mambo ya chama bila baraka za vikao halali, yeye CHADEMA sio mwanachyama wa kawaida kama mimi, yeye ni kiongozi, amekua akijidai kutoa maini yake hadharani bila mipaka, huyu kajisahau, amejaa kiburi.
   
 7. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtasema yote CCM wale tunasonga mbele
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  bado nasubiri chama kipya...vilivyopo vyote si kwa maslahi ya taifa ndio maana siwezi kupigia kura.....uongouongo tu........maslahi binafsi tu....kulewa sifa tu....hamna jipya.....nasubiri wapambanaji dhidi ya mafisadi walioko ccm waanzishe chama chao...ntawapigia kura.
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nakaribia kuamini kuwa upinzani wa kweli bado sana bongo. Kwa Wapinzani wa dhati tuko nyuma yenu. Sina imani tena na zitto
   
 10. C

  Charuka Member

  #10
  Dec 1, 2009
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Bongo code number: Zitto mtu wangu, naomba magari japo mawili niende jimboni.
  Germany code number: Ahaa dogo, nikikupa magari ntaeleweka kweli?
  BCN: Kumbuka mtu wangu nimechinjiwa baharini kwa sababu yako.
  GCN: Hiyo kweli, ulinifaa kwa jua japo wenye chama waliweka kauzibe
  BCN: Ahsante kwa uelewa mkuu.
   
 11. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,987
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  Mimi CCM lakini sipendi kufanya faulo kwenye demokrasia kwa kuhonga vibaraka (akina Zitto) kuua upinzani. Huu ni uzandiki. Mzee Butiku jana katusema saana wana-CCM (utadhani Mwl Nyerere (RIP) vile!!).
   
 12. chishango

  chishango JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 827
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
  Kaka zito kila kilele kina ngazi za kukifikia, ni chombo chenye uwezo wa kupaa pekee ndicho chaweza kufika kileleni bila hizo hatua, kaka tafadhali sana umaarufu umeupata saaana hata ukatuaminisha wadanganyika kuwa ni mwenzetu, nilianza kupata mashaka ishu ya mitambo ya dowans ilipoanza nikashtuka lakini kwa haya yanayotokea sasa naanza kuwaza kuwa yawezekana huu ni mwanzo wa mwisho wako, wakumbuke kina Lamwai, Ngawaiya, Kabourou, tambwe na wengineo wengi. Mungu alikuinua akang'aza nyota yako na sasa umejaa kiburi waona chadema haipo bila ZITO naisikitikia nchi yangu kwa hata wapinzani nao ni wale wale MH. ZITO naomba kutoa hoja
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Jamani tumechoka na stori za huyu jamaa.Hebu tujadilini mambo mengine ya muhimu.Hivi nyie hamjakinai tu?
   
 14. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chama kisichokuwa na MIIKO YA UONGOZI (kiwe CHADEMA, CCM, CUF au kinginecho) hakiwezi kuiongoza Tanzania wala kuifikisha popote! Kitaanza vizuri lakini mwisho wake utakuwa mbaya! Turudishe AZIMIO LA ARUSHA, haya mambo yote ya ufisadi na migongano ya maslahi itakuwa historia! Kazi ipo kwenye kumfunga paka kengele kama panya watafikiri kwamba paka anaweza kujifunga kengele mwenyewe! Amini usiamini hata CHADEMA wakichukua nchi watakuwa kama CCM tu na hakuna jipya watakalolifanya! Tusubiri chama kipya, kwa sasa ni kudanganyana tu wanaJF!
   
 15. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh mwaka huu tutasikia mengi! Zito anatoa MAINI YAKE HADHARANI?
   
 16. l

  lukule2009 Senior Member

  #16
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ushauri wa bure kwa Kafulila :

  Wewe sasa ni mwanachama wa NCCR Mageuzi, kwa hiari yako umejitoa Chadema. Basi sasa anza kujenga chama chako kipya, mambo ya Chadema waachie wenyewe. Kama Mbowe anakula ruzuku au hali , au kama watu wengine watatoka hawatoki hayo yote kwa sasa kwako wewe ni "history". ukiitisha mkutano zungumzia sera za NCCR .. na kwa kuwa umeenda huko ili utimize ndoto ya kuwa mbunge kama ulivyosema mwenyewe ni wazi hujaenda NNCR kwa kuwa unazikubali na kuunga mkono sera za chama.. hapana.. umefuata ubunge .. ikitokea ukakosa ubunge sijui utakuwa unasema nini. Chama ni imani na sera sio maswala na malengo binafsi ( opportunist) yako binafsi... sasa basi kila la kheri .. Chadema ndio umeshatoka .. wewe waachie wenyewe kuendelea kutaja Chadema utawaudhi NCCR :):) .. u need to show them that your heart is with NCCR white and blue sawa baba ..tehtehte:):).. If you really love the party and not that you just want to use it to be Honourable MP. Kila la kheri, halafu usisahau ndani ya NCCR kuna watu nao walikuwa wanajiandaa kugombea .. usishangae ukapingwa vile vile .. na wewe hujazoea kukaa bila cheo .. utahama?? just kidding ahahah
   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  yetu macho. hii ndo siasa ya bongo
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Dec 1, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Kigeugeu umejua lini? maana hizi stori hazijaanza leo,zilianza kabla ya uchaguzi. Na baada ya uchaguzi mmempe uongozi wa juu.Unataka kusema Chadema yote ni vigeugeu kama Zito.Au umejua lini kuwa ni kigeugeu?

  wanachadema bwana, wamekosa mbinu za vita wanapambana wenywe kwa wenyewe mpaka aibu! ndo mnataka kusika nchi! acheni hwa CCM mafisadi waongoze mpaka mkome!
   
 19. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Haya bwana sie yetu macho yakhe kwa kauli hizi msisake mchawi wa chama chenu kwani hapa mnaroga chama mchana kweupe!
  NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  azimio la arusha ni itikadi au sera au mkakati fulani? Sioni sababu ya kurudi nyuma. Sera na itikadi popo tuliyonayo vinatosha kujipanga. CHADEMA THIS IS IT! mwakani mkichemsha ndio mwisho wenu
   
Loading...