Kauli ya CUF kwa yanayoendelea Arusha sasa hivi

Kambaya umesahau ilivyokuwa mauaji ya 2001 pale Unguja? Yalikuwa na sababu za kisiasa au za jinai tu? Chama gani kinatumia mauaji hayo kisiasa kama si CUF kwa kutoa matyamko ya kujikomba kwa wenzi wao maCCM? Haya yalifanywa kwenye mkutano wa kisiasa na ya kampeni za uchaguzi kwa lengo la kuviza juhudi za kisiasa na kuzuia uchaguzi huru ambao ushindi ulikuwa dhahili kuwa ni wa CHADEMA. HAKUNA ANAYEFURAHIA MAUAJI HAYA ISIPOKUWA MASHETANI WA KIJANI MA MARAFIKI ZAO. WALIUA WATU MTWARA - KUSINI NA SASA WAMERUDIA ARUSHA- KASKAZINI. JAMBO MOJA NI DHAHILI, HATAMALIZA WATANZANIA WOTE KABLA YA WENYEWE KUMWONA ALIYEWAUMBA WAKIWA JEHANAMU NA SADDAM. Ukikosa cha kufanya, kareview sera za kiliberali na usilete mada za kukera
 
"Mwisho CUF-Inatoa wito kwa wapiga kura wa Arusha kuwakataa wale wote wanaotumia mauaji haya kama mtaji wa kuwapatia kura."
Nafikiri wananchi watasikia na kuwapa basi hizo kura, maana mnatumika hadi mnakosa akili.
 
wewe tokwa mapovu tuu,

mbona hata chadema chama chako hakikulaani tukio, wewe umeona CUF tu.,.....kweli nyani haoni.....
 
Hivi inawezekana mume akawa na virus vya ukimwi na hawara/nyumba ndogo akakosa kuupata? Cuf hawana pa kukwepea swala la Arusha
 
Si rahisi kuukosa ukimwi maana wote wanashirikiana! Ukizingatia wote ni wanandoa!
 
Tarehe 118? au watu wanatumia tarehe za bara gani ?
Yaani Profesa Lipumba anaadhirika kwelikweli kufanya kazi na vilaza kama huyu aliyeandaa bandiko hili, kwanza hata ujumbe wake hauleweki kama ni nini
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 118/06/2013
RAMBI RAMBI KWA WAFIWA BAADA YA MLIPUKO WA BOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA MJINI ARUSHA

CUF-Chama cha Wananchi kinatoa pole kwa Wafiwa na Majeruhi wa Tukio la Bomu lililorushwa kwenye Mkutano wa Chadema,uliofanyika kwenye Viwanja vya SOWETO Mjini Arusha. Hili si sula la Siasa wala si suala la Udini wala si ukabila, haya ni mauaji. Tena ni mauaji yenye lengo la kusambaratisha Taifa letu. Kama ambavyo tumekwisha eleza mara kadhaa kupitia Mikutano tuliofanya kipindi cha Kampeni na kusisitiza juu haja ya Arusha kuwa na utulivu wa Kisasa, tunasisitiza tena kwamba ni muhimu kwa sasa Vyama vya siasa kuacha kutupiana lawama juu ya nani au Chama gani cha Siasa kimehusika na Mlipuko huo.

CUF- Inashauri ni vyema Viongozi wa Vyama tukawa Dira kwa Wanachama wetu kwa kutoa muongozo utaojenga Taifa letu na sio kuwa wachochezi wa kuligawa Taifa letu kwa misingi ya itikadi za Vyama vyetu. Suala hilI libaki katika
mikono ya Serikali ili ifanye uchunguzi na hatimae itoe majibu kwa Wananchi. Tangu kutokeE maafa haya, baadhi ya Vyama vinataka kugeuza mauaji haya kuwa Mtaji wa kupatia kura kwa Wananchi jambo ambalo linazidisha machungu kwa Wafiwa. Watu waliopoteza maisha kwa mlipuko huo, ni pamoja na wato wawili waliokuwa wakitoka Madrsa , watoto hawa kwa vyovyote vile hawana Chama, na hata wazazi wao huwenda wasiwe CCM,CUF au CHADEMA , vyama ambavyo vipo kwenye Ushindani wa kwania Viti vya Udiwani unaotarajiwa kufanyika June 30 2013.

CUF-Chama cha Wananchi , kinaona jambo baya na halitaweza kujenga Arusha yenye Mshikamano iwapo kuna baadhi Vyama vitatumia Mauaji haya kama njia ya kupata kura toka kwa Wananchi.Tunavishauri Vyama vinavyotumia Mauaji haya kama mtaji wa Kisiasa viache kwa maslahi ya watu wa Arusha na Nchi yetu kwa ujumla.
CUF-Chama cha Wananchi pia kinatoa wito kwa viongozi wa Dini kuacha kuingilia suala la Uchaguzi kwa kutoa maelekezo kwa waumini wao kuchagua mgombea wanaemtaka wao kwa utashi wa Imani zao. Ni vema kwa Viongozi wa Dini wakafahamu kwamba maelekezo ya kumchagua kiongozi wa kisiasa kwa utashi wa Imani yake utatupeleka mahala pabaya sana. Wananchi hawachagui Kiongozi wa kuendesha Ibada Msikitini au Kanisani, jambo hili litatuletea matatizo hapo baadae. CUF-Chama cha Wananchi kinawaomba viongozi wa Dini, kuacha jambo hilo kwa Maslahi ya Tanzania. Ni vyema viongozi wa Dini wakijikita zaidi kutoa mafunzo ya kiimani yatayoezesha Viongozi wataochaguliwa kutoa Haki na kuwa waadilifu kwa Wataowaongoza na si kuwaelekeza waumini kumchagua mtu kutokana na Imani yake.

Mwisho CUF-Inatoa wito kwa wapiga kura wa Arusha kuwakataa wale wote wanaotumia mauaji haya kama mtaji wa kuwapatia kura.
Imetolewa na

Abdual Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Haki za binadamu,Habari na Uenezi

0719566567
Maoni ya Waliberali. Haki sawa kwa wote. kura 07 Kata ya Genge huko Muheza Tanga
 
Sawa. Lakini inawezekana vipi mtoto akajitoa kwenye kesi inayomhusu baba yake? CUF na CCM ndiyo wanaongoza serikali CCM nidyo inayotuhumiwa kupanga na kutekeleza mauaji. Sasa anatuambia nini? Ni bora angekaa na viongozi wa CCM akawapa haya mawaidha. Huu ndiyo mtazamo wangu.
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]

sio mtoto hawa ni wana ndoa.
 
sijaona tofauti ya hili tamko na lile la nape.
 
CUF mnashida sana ninyi. Mnadhani mlivyowasaidia CCM 2010 nmkafanikiwa ndivyo mtakavyofanikiwa kwenye hili la Arusha? Naona kaanza Nape alafu nanyi mmelipokea. Hapa watu wanazungumza msiba nyie mnazungumza kura. Kweli mmepotoka na hii rubish yenu mlioitoa kwenye vyombo vya habari
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 18/06/2013
RAMBI RAMBI KWA WAFIWA BAADA YA MLIPUKO WA BOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA MJINI ARUSHA

CUF-Chama cha Wananchi kinatoa pole kwa Wafiwa na Majeruhi wa Tukio la Bomu lililorushwa kwenye Mkutano wa Chadema,uliofanyika kwenye Viwanja vya SOWETO Mjini Arusha. Hili si sula la Siasa wala si suala la Udini wala si ukabila, haya ni mauaji. Tena ni mauaji yenye lengo la kusambaratisha Taifa letu. Kama ambavyo tumekwisha eleza mara kadhaa kupitia Mikutano tuliofanya kipindi cha Kampeni na kusisitiza juu haja ya Arusha kuwa na utulivu wa Kisasa, tunasisitiza tena kwamba ni muhimu kwa sasa Vyama vya siasa kuacha kutupiana lawama juu ya nani au Chama gani cha Siasa kimehusika na Mlipuko huo.

CUF- Inashauri ni vyema Viongozi wa Vyama tukawa Dira kwa Wanachama wetu kwa kutoa muongozo utaojenga Taifa letu na sio kuwa wachochezi wa kuligawa Taifa letu kwa misingi ya itikadi za Vyama vyetu. Suala hilI libaki katika
mikono ya Serikali ili ifanye uchunguzi na hatimae itoe majibu kwa Wananchi. Tangu kutokeE maafa haya, baadhi ya Vyama vinataka kugeuza mauaji haya kuwa Mtaji wa kupatia kura kwa Wananchi jambo ambalo linazidisha machungu kwa Wafiwa. Watu waliopoteza maisha kwa mlipuko huo, ni pamoja na wato wawili waliokuwa wakitoka Madrsa , watoto hawa kwa vyovyote vile hawana Chama, na hata wazazi wao huwenda wasiwe CCM,CUF au CHADEMA , vyama ambavyo vipo kwenye Ushindani wa kwania Viti vya Udiwani unaotarajiwa kufanyika June 30 2013.

CUF-Chama cha Wananchi , kinaona jambo baya na halitaweza kujenga Arusha yenye Mshikamano iwapo kuna baadhi Vyama vitatumia Mauaji haya kama njia ya kupata kura toka kwa Wananchi.Tunavishauri Vyama vinavyotumia Mauaji haya kama mtaji wa Kisiasa viache kwa maslahi ya watu wa Arusha na Nchi yetu kwa ujumla.
CUF-Chama cha Wananchi pia kinatoa wito kwa viongozi wa Dini kuacha kuingilia suala la Uchaguzi kwa kutoa maelekezo kwa waumini wao kuchagua mgombea wanaemtaka wao kwa utashi wa Imani zao. Ni vema kwa Viongozi wa Dini wakafahamu kwamba maelekezo ya kumchagua kiongozi wa kisiasa kwa utashi wa Imani yake utatupeleka mahala pabaya sana. Wananchi hawachagui Kiongozi wa kuendesha Ibada Msikitini au Kanisani, jambo hili litatuletea matatizo hapo baadae. CUF-Chama cha Wananchi kinawaomba viongozi wa Dini, kuacha jambo hilo kwa Maslahi ya Tanzania. Ni vyema viongozi wa Dini wakijikita zaidi kutoa mafunzo ya kiimani yatayoezesha Viongozi wataochaguliwa kutoa Haki na kuwa waadilifu kwa Wataowaongoza na si kuwaelekeza waumini kumchagua mtu kutokana na Imani yake.

Mwisho CUF-Inatoa wito kwa wapiga kura wa Arusha kuwakataa wale wote wanaotumia mauaji haya kama mtaji wa kuwapatia kura.
Imetolewa na

Abdual Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Haki za binadamu,Habari na Uenezi

0719566567

Nimeamini hii ni CCM B haya mambo gani ya kuwaambia watu mwaliofiwa!!!!??? UMESHAONA TANGU LINI MTU ANAYEFIWA ANACHAGUWA WA KUMPA POLE NA KUMSAIDIA!!!!!?? NINYI ARUSHA KWA CHADEMA MUIONE KAMA PEMBA KWENU NINYI.
 
Cuf bora mungenyamaza kwa taarifa hii mume onyesha wazi muko uoande gani.laiti bomu lingerushwa kwenye mkutano wa cuf misikti yote ngeongelea hayohayo na usalama arusha ungevurugika kama ilivyotokea pemba mwaka 200? Askari kuchinjwa na wana cuf.
 
Back
Top Bottom