Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,727
Ni siku takribani nne tangu Mkuu wa nchi awasute, awakejeli na kuwadharau watu wa mkoa wa Kagera.
Ule haukuwa utani kwa sababu Mkuu yule si mtani wa watu wa Kagera. Zaidi sana, maneno yale yanafanana sana maneno aliyoyasema huko Wilayani Misenyi. Ukitilia maanani kuwa imemchukua miezi mitatu kwenda Kagera kuwapa pole ya tetemeko, ni wazi kuwa Mkuu alimaanisha alichokisema siku hiyo, yaani "Kagera nao wamezidi - Ukimwi, Mnyauko, Tetemeko, katerero, Kiterangoma, n.k". Haya si maneno ya kuwaambia watu walio katika shida, ukiacha mbali kitendo cha serikali kukusanya misaada kwa kutumia shida zao, kisha kuzitumia kwa kazi nyingine.
Najiuliza yafuatayo:
- Wabunge wa Mkoa wa Kagera wanamwakilisha nani?
- Je, wana msimamo gani juu ya kauli hizi za Mkuu wa nchi dhidi ya wananchi waliowachagua wao?
- Wao wakiwa wananchi wa Kagera, nao ni sehemu ya majanga hayo ya "kujitakia"?
Bila kusubiri majibu yao kwa maswali hayo, nawashauri yafuatayo:
- Wamtake Mkuu wa nchi hadharani, aombe radhi na maisha yasonge mbele, akikataa,
- Wajiuzuru kuonyesha kutoridhishwa na kauli za udhalilishaji kwa wananchi waliowachagua,
- Mbali na wabunge, viongozi wote wa kijamii mkoani Kagera walaani kauli hizi
- Wateule wote wa Rais watokao Kagera mahali popote, wajiuzuru kupinga udhalilishaji huu
- Madheheb yote ya dini, yaitishe sala maalum kumwomba Mungu awafanyie wepesi wana Kagera ili waepushe na majanga haya ambayo Mkuu amesema yamezidi kwa Kagera
--/Baija