Kauli nzuri ya muuguzi huanza kumpa nafuu mgonjwa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Ndiyo, kauli nzuri ya muuguzi huanza kutoa nafuu kwa mgonjwa. Nafuu ya kisaikolojia, humafanya mgonjwa ajihisi yupo sehemu sahihi na salama kuweza kutatuliwa shida yake ya kiafya.

Kumkaribisha mgonjwa na kuumuelekeza kwa upendo hatua za kufuata wakati wa matibabu yake ni afya kwa mgonjwa, lakini kumkaripia na kumfokea kwa kuwa hakufuata utaratibu au vinginevyo ni kumuongezea ugonjaa wa moyo na hofu ya kuona shaka moyoni hata kuwa huru kueleza tatizo lake na hivyo wakati mwingine kushindaa kupata tiba stahiki.

Kuna muda unaenda hospitali ukiwa na ugonjwa ambao umekuletea msongo wa mawazo. Hivyo unahitaji mtu wa kukufanya upate tahafifu ambaye ni moja ya watu hao ni wauguzi lakini badala yake unafokewa mwanzo mwisho wakati wa kupewa huduma.

Ukiuliza swali unaweza ukajibiwa ovyo au wakati mwingine wakafola tu kuwa kaa kimya subiri zamu yako ikifika utaitwa mbona unakuwa msumbufu hivyo? Kwani watu si wanakuona hapo. Kwa kweli huduma kwako inakuwa ngumu sana kupata.

Na mara nyingi hii hujitokeza kwenye hospitali za Serikali japo sio zote. Unaweza uliza kwa nini nitumie dawa hii na si nyingine inaonekana mjuaji unawafundisha kazi watakujibu majibu ya ovyo sana na kuanza kufanya makusudi ya kukucheleweshea tiba. Kumbe wangeweza kukujibu kwa lugha nzuri na mkaelewana bila tatizo.

Wauguzi manpotoa huduma zenu zingatueni kutumia kauli au lugha laini kwa wagonjwa mnaowahudumia.
 
Na wewe ukienda kutibiwa fuata utaratibu wa eneo husika .. hii itakusaidia wewe pamoja na mtoa huduma.
 
Back
Top Bottom