Muuza simu used
JF-Expert Member
- Aug 23, 2017
- 4,393
- 7,108
Wapendwa mtu kuwa na kauli nzuri ndio mwanzo wa hekima!tumia busara jinsi ya kumjibu mtu!mfano badala ya kumwambia mtu wewe ni Muongo! Unaweza kumwambia Fulani hapo mimi sikubaliani na wewe!,badala ya kumwambia mtu wewe ni mjinga unaweza kumwambia nadhani labda huna uelewa wa kutosha katika hilo jambo,badala ya kumwambia mtu wewe ni mlevi unaweza ukamwambia sio vizuri kunywa pombe kila siku inakupotezea ufanisi!etc,maneno mazuri humtoa nyoka pangoni!sasa wewe endelea kufuga chura utaishia kusindikizwa kwa mateke