Kauli Mbili Muhimu za Mwalimu Nyerere

Kauli Mbili Muhimu za Mwalimu Nyerere

Mariswaga

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2015
Posts
201
Reaction score
2
Marehemu Mwl Julius Kambarage Nyerere wakati wa uhai wake alitoa kauli kubwa mbili
1. "Watanzania wanataka mabadiliko... wasipoyaona.. wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM".
Kauli hii ni tata kwakua haikuweka wazi ni kwanamna gani watayatafuta mabadiliko hayo nje ya CCM. Lakini pia Mwalimu hakuonesha kama endapo tutayatafuta mabadiliko nje ya CCM tutafanikiwa kuyapata

2. "Rais wa Tanzania atatokea kwenye chama chochote, ila Rais bora wa Tanzania hawezi kutoka nje ya CCM"
Hii kauli iko wazi kabisa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Rais na Rais Bora, kama tutaamua kumchagua Rais nje ya CCM atakuwa tu Rais wetu lakini si Rais bora.

Kauli hizi mbili zikijumlishwa kwa pamoja tunapata majibu makubwa mawili
1. Kumchagua Rais nje ya CCM ni kumchagua Rais asiye bora na asiye na faida kwa maendeleo na mustakabali wa nchi yetu

2. Mabadiliko yatakayopatikana toka kwa kiongozi wa nje ya CCM hayatokuwa mabadiliko bora, au kwa lugha nyingine tunasema kuwa yatakuwa mabadiliko hasi

KUMBE: Kwa mujibu wa kauli hizi za Mwl. Nyerere ni kuwa tunatakiwa kumchagua Rais anayetangaza mabadiliko ndani ya CCM kwakuwa ndiye atakayekuwa Rais bora wa Tanzania na ndiye atakayeleta mabadiliko chanya kwa Watanzania

ASANTE SANA BABA WA TAIFA KWA WOSIA WENYE MANUFAA KWA MAISHA YETU YA SASA NA YA BAADAE
 
Wanamnadi EL leo walinipa sababu toshaaa za kumkata, na walinipa sababu kuntu pia za kumpeleka Magufuli ikulu!
Kwaheri Lowassa!
 
Kikwete ni Rais Bora na ndio maana Tunayaona Maisha Bora Kwa kila Mtanzania...

Yes Ni rais Bora anaetoka ndani ya CCM na ndio maana anachekea Mafisadi na kutetea Wizi wa Fedha za Umma (Pitia hotuba aliyoitoa kipindi cha Escrow)

Najua Rais kikwete ni Bora kwasababu anatoka ndani ya CCM na ndio maana ankuwa na Vijembe kama 'Usipokubali kuliwa Huli' N.K

Sioni Umuhimu wala ubora wa Kumchagua magufuli kwani Nimekinai kutokana na Uongozi wa Kikwete...
Magufuli hatoweza kuongoza pekeyake hii nchi ni lazima atahitaji mawaziri. So ndani ya CCM mawaziri wengi ni wapigaji.

Muda mwingine hatupaswi kuwa na akili Mgando.
 
kwenye kauli hizi mbili za mwl kuna hoja mbili za msingi; kwanza mabadiliko lazima yatokee ambayo kupiga vita rushwa,udini,ukabila na kwamba tz sio nchi ya matajiri,pili rais bora hawezi toka nje ya ccm ilihali ipo hivyo kuna kipindi kirefu cha ukimya kuitoa ccm hadi muda wa kumpata rais bora
 
Kauli za Mwalimu zisitumike kama hirizi.Je tunayaishi aliyoyahubiri Mwalimu?Watanzani wa sasa wanajitambua
 
Mkuu kauli hizi sio mafumbo.

Kauli zipo wapi zinajieleza. Acha kupotosha watanzania.

Ccm out.
 
"Raisi bora atatoka ndani ya CCM" hii ndio kauli ambayo inaenda kutimia karibuni. Raisi bora ni lazima atoke ndani ya CCM aende upinzani agombee huko na awe raisi. Ndani ya CCM kumejaa mambo mengi machafu na mfumo mbovu. mtu akitaka kuwa raisi atoke ndani ya ccm.Tanzania imekosa raisi bora kwa muda mrefu sasa inaenda kupata raisi bora "aliyetoka ndani ya ccm" na kwenda chadema. Nyerere hakusema Raisi bora lazima awe ndani ya CCM bali atatoka ndani ya CCM
 
Nyerere sio msaafu bali ni mtu kama mimi na wewe. Tunamheshimu kwa kuwa ni baba wa taifa
 
Lowassa hakutoka nje Ya sisiem ndio maana atakuwa RAISI bora.
 
Magufuli ndo kura yangu mimi na familia yangu ya watu 12
 
kwanza kabisa ujui maana ya neno (marehemu)al-marhum mana ungejua usingelitumia pahala hapa

2.ni umbumbumbu kuamini kuwa nyerere alikuwa sahihi kwa kila jambo.

3.umekiri kuwa alitoa kauli tata kama aloitoa siku moja pale habari na maelezo kuwa 'ccm sio mama yangu nikiona haifai nitaondoka' muuliza Mzee Tiddo Mhando alikuwepo pale pamoja nami nilikuwa nafanya fld pale
 
Wanaomsapot lowasa wengi wao wanywa viroba

Ningekuwa mm ccm
Ningetumia 80million kununua viroba nchi nzima
Ili vigawiwe bure kuanzia tarehe 23-26
Hapo najua wanywa viroba wengi ambao n wana ukawa asilimia80
Wangekuwa wapo kwenye usingiz mzto wa viroba
Hivyo kushindwa kumpigia jambaz kura
 
Back
Top Bottom