Kauli Hii ya Zitto Wapinzani Wote Waitafakari

Tafadhali sana mkuu...

kumfananisha mange kimambi na hao vibaraka wa guma na bashite ni kumshushia hadhi yake ya kimataifa na kumwaibisha...

ni dhambi kubwa sana kufananishwa na mnafiki kama zitto kabwe.

Hivi unajuwa huyo Mange unayemtukuza hata huko Marekani watanzania hawana mpango naye? Mange ni kibaraka wa kina Mbowe na baadhi ya viongozi wasiojitambua ambao wanaamini kuwa Mange yuko level moja na rais wakati she's a nobody. Watanzaia badilikeni jamani, angalieni na sasa mnamtukuza DK. Shika wakati he's a nobody....yaani mnajisahau hata kujiendeleza kushabikia ujinga.
 
Umeshindwa kujadili hoja unamjadili Zitto. Zitto ametoa hoja nzuri sana. Wapinzani waache kulialia, watafute njia za kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wanaowaongoza.

Siyo kama nimeshindwa kujadili hoja, nimemzowea Zitto. Mara ngapi anatoa hoja bila hata yeye mwenyewe kujuwa anasema nini kisha anaishia mitini? Ndiyo maana nikasema huyu jamaa si wa kumtilia maanani. Kama uniamini, muulize alikuwa anamaanisha nini kwa kusema vile, kama hajakugeuka na kusema si yeye aliyesema vile. Huyo ndiyo Zitto. Unafikiri kwa nini viongozi wanamdharau?
 
Kwa nchi zetu za Kiafrika ni ngumu sana hilo. hata Zitto analijua hilo ila siasa zake za Kinafiki tu ndo zimemfanya aandike hilo.
Hapo pagumu ndio penye mpenyo wa kuiondoa ccm, siasa nyepesi tunazozililia za kelele za majukwaani haziwezi kuiondoa ccm.

Vita vya kimya kimya vyenye matokeo ndio vinavyoleta ushindi.

Chama kinachopenda siasa za maneno na kulalamika sana hicho sio chama bali ni kundi la kiharakati.

Kama tumewaamini Kwa ngazi ya ubunge na bado hatuoni lolote la tofauti wanalofanya majimboni tunawezaje kuwaamini Kwa nchi nzima.

Kama chama kinapokea zaidi ya bilioni 3.6 Kwa mwaka na hatuoni output japo ka ofisi tu unawezaje kukiamini kwenye hela za nchi nzima!?

Vyama vyetu kabla ya kuikosoa ccm vijitazame kwanza vyenyewe na vibadilike.
 
(From Zitto FB wallpage.)

Leo nitawapa mfano wa wanasiasa wenzetu wa upinzani katika nchi ya Venezuela, ambapo Rais Mjamaa mwenzetu, ndugu Nico Maduro, kamaradi, amezuia vyama kushiriki uchaguzi. Wakati wa Rais Chavez vyama vya upinzani na wanasiasa wa upinzani walikuwa wanabanwa kweli na Serikali. Hii tunayofanyiwa na Magufuli ya watu kufungwa na kuachiwa, kupigwa, kuzuia mikutano, kukamata watu wanaomkosoa kwenye mitandao ni cha mtoto.

Mwandishi William Dobson aliandika kitabu mwaka 2012 kiitwacho 'Dictator’s Learning curve: Inside the global battle for democracy'. Katika kitabu hiki alimhoji Meya mmoja wa chama cha upinzani katika mji mmoja masikini kabisa kuhusu siasa tofauti. Meya Carlos Ocariz wa Mji wa Petare alimshinda mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na Rais Chavez. Rais Chavez akaamua kukata fedha kwenda kwenye mji huo, akaondoa magari ya takataka na kukata maji.

Meya Ocariz anasema, "sikuanza kulalama na kupiga kelele. NIliamua kufanya tofauti na kutekeleza masuala ya maendeleo yaliyo ndani ya uwezo wangu kwenye mji wangu. Kuhakikisha watu wangu wanapata maji nilitumia magari ya Mji kusambaza maji kwenye nyumba za watu. Nilizuia matumizi makubwa ya ofisi na kupeleka fedha kuzoa taka na kuanza kuwalipa wazazi ili wapeleke watoto shuleni".

Meya Ocariz akaendelea; "Upinzani tunalalamika lalamika tangu mwaka 2000, tunapata nini? Badala yake tuwaonyeshe wananchi tofauti ya siasa zetu na za Kamaradi Chavez. Tutatue matatizo ya watu".

Kwa kimombo anasema; "we must offer true political alternatives to Chavez, solving problems and not just complaining about how we are treated in the system that almost everyone agrees is unfair".

Ndugu wajumbe, sisi tuna maeneo tunaongoza, ama Vijiji, Kata au Manispaa. Sisi pia tumekuwa tukisema kuwa tunataka kufanya siasa tofauti. Je inawezekana tumeshindwa kufanya hivi ndio maana baadhi ya wenzetu wanaondoka na kutuhama? Ninatoa rai kuwa tujitafakari kwa kina sababu za ndani za mawimbi haya ya kisiasa na tupate majawabu ya namna ya kusonga mbele.

My take:
Pamoja na ZZK kutoaminika sana katika siasa zake, lakini falsafa aliyoitamka hapo juu nadhani ndio njia sahihi ya kupambana na uongozi Wa kidikteta pale ambapo Halmashauri zetu zinazoongozwa na wapinzani zinapo nyanyaswa kiuchumi
Kwako ww mwana siasa gani unamwamini
 
Yeye hana mbunge zaidi ya yeye na wala hakuna diwani wake aliyeondoka
 
Hivi in kwa nini vijana WA makarai WA cdm hawampendi Zito utasikia aaminiki ukiuliza kwa lipi hakuna jibu zaidi ya Maneno ya kukaririshwa
Watupe mwana siasa anaeaminika ndani ya chama chao hakuna hata atakuonesha

Nawambia Zito nibmkweli Na ukweli wake ndio hufanya mumchukie
 
kodi za wananchi husika ndizo zinazotakiwa kuboresha mazingira yao wanayoishi, sasa wapinzani watapata wapi fedha za kuboresha hayo usemayo? au wewe unafikiri kuwa haya yanayofanyika fedha zinatoka mifukoni mwa viongozi wa ccm?jiongeze kifikra usiwe kama mtu mpumbavu. kwani fedha zinazotolewa na wananchi kupitia kodi za sehemu husika zikikabidhiwa kwa Halmashauri zinazoongozwa na upinzani watashindwa kuzifanyia maendeleo?
 
Back
Top Bottom