Kauli hii ya CHADEMA ina athari yoyote kwa yanayoendelea?

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
TAMKO LA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA KUHUSU HALI YA TAIFA



TAMKO LA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU HALI YA TAIFA.


Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika tarehe 29-30 Januari 2011 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa Taifa Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (Mb), pamoja na mambo mengine, imepokea, kujadili na kutolea maazimio Taarifa ya Hali ya Siasa na Taifa kwa ujumla. Maazimio haya yapo katika maeneo matano yafuatayo.

3. Matatizo ya Nishati ya Umeme na Gesi na Malipo kwa Kampuni Hewa ya Dowans

Kamati Kuu imesikitishwa na kupanda holela kwa bei za nishati muhimu za umeme na gesi, pamoja na kushindwa kwa serikali ya CCM katika kuwekeza kikamilifu katika sekta ya nishati hapa nchini. Aidha, Kamati Kuu imesikitishwa na kufadhaishwa sana na uamuzi wa CCM na serikali yake kuridhia kuilipa Kampuni hewa ya Dowans fedha za walipa kodi wa Tanzania zipatazo Shilingi bilioni 94, pamoja na kwamba Kampuni hii ilikwishaharamishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya wananchi.

Kamati Kuu imetambua kuwa sakata la Dowans ni mwendelezo wa vitendo vya kifisadi ndani ya CCM na serikali yake ambavyo vimeligharimu taifa hili kwa miongo mitano iliyopita. Hivyo basi:

  1. Kamati Kuu imewahimiza wana CHADEMA, wabunge na wananchi kwa ujumla kuendelea kupinga kwa nguvu zote malipo ya Dowans
  2. Kamati Kuu imewaelekeza viongozi pamoja na wabunge wa CHADEMA kuendelea kuwahamasisha wananchi kupinga kwa njia mbalimbali za kisiasa na kisheria malipo ya Dowans na ufisadi mwingine hapa nchini
  3. Kamati Kuu imewapongeza na kuwashukuru wanaharakati wa taasisi za kiraia kwa ujasiri na moyo wao wa kizalendo kwa uamuzi wao wa kufungua kesi mahakamani ya kupinga malipo ya Dowans
  4. Kamati Kuu imeiasa Serikali ya CCM kutokuona aibu kutekeleza sera za CHADEMA zilizofanyiwa utafiti kuhusu namna ya kujenga na kuimarisha sekta ya nishati ya umeme na gesi hapa nchini ili nchi yetu iondokane na tatizo la kudumu la umeme.
  5. Kamati Kuu imeiagiza Secretariat yake kuanza maandalizi ya maandamano ya nchi nzima ya kupinga ongezeko la bei ya umeme, gesi na kuilipa Dowans. Na tarehe 24/02/2011 itakuwa siku ya kuanza maandamano kwenye Jiji la Mwanza na miji mingine kadiri ratiba itakavyotolewa.

7. Kuhusu mpango mkakati wa chama 2011-2016.

Kamati Kuu ilijadili na kupitisha mapendekezo ya mpango kazi wa chama kwenye Baraza kuu la chama .Pia ilijadili na kupitisha mpango kazi wa mwaka 2011-2012.

Tamko hili limetolewa leo tarehe 31/01/2011.

Dk Willibrod Peter Slaa
Katibu Mkuu




6773768.jpg
 
umeshashiba pilau la maulid basi mashuzi tuu

ile tarehe kwenye heading ndiyo inaonyesha jinsi gani ulivyo makini kwenye taahira ya ubongo
 
kweli wewe ndiye jk wa ukweli. you sound so desperate hata unatuambia maandamano ya 24/11/2011 yamesababisha milipuko leo? Unatupa ushahidi msivyo makini na ndiyo maana tunataka muondoke
 
umeshashiba pilau la maulid basi mashuzi tuu

ile tarehe kwenye heading ndiyo inaonyesha jinsi gani ulivyo makini kwenye taahira ya ubongo

kweli wewe ndiye jk wa ukweli. you sound so desperate hata unatuambia maandamano ya 24/11/2011 yamesababisha milipuko leo? Unatupa ushahidi msivyo makini na ndiyo maana tunataka muondoke

ni Tarehe 24/02/2011 Mod watanirekebisha Sasa changia HOJA:coffee::coffee:
 
Hivi mkuu uunatumia kalenda ya wapagani nini? Hiyo tarehe 24/11/2011 ishafika kweli? CRAP
 
Wewe ni mpuuzi, unafikiri upuuzi, umejaa upuuzii, unawaza upuuzii, unafanya upuuzi.
Lete hoja za maana!

HOja ndo hiyo haya mabomu yanaendana na maandamano ya tarehe 24/02/2011??????????????????????:twitch::twitch:
 
Kabla ya kuchangia niulize swali,Hivi zile milioni 90 zilizotolewa na Serikali kwa wabunge kununua magari,wabunge wetu wapendwa wanaopigania matatizo ya watanzania hasa wa CDM walizichukua?
 
Back
Top Bottom